Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Oktoba, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Oktoba, 2013

Yemeni: Bundi Atua Nje ya Dirisha Langu

Mwanablogu wa Yemeni, Abdulkader Alguneid amkuta bundi nje ya dirisha lake:

Kupitia mtandao wa Twita, anaelezea tukio hilo ambalo ni nadra sana kutokea:

Namna Wanawake Nchini India Wanavyoweza Kujilinda

Ukatili dhidi ya wanawake umezidi kushika kasi nchini India. Mwandishi na mwanablogu Shilpa Garg aweka bayana dondoo za namna ambavyo wanawake wanavyoweza kuchukua tahadhari na kujilinda.

Baa la Njaa Nchini Haiti

Kwa nini – wakati nchi imepokea misaada ya chakula yenye thamani ya si chini ya dola za kimarekani bilioni moja wakati wa majanga ya matetemeko ya ardhi ya mwaka 1995 na 2010 – bado baa la njaa linaongezeka?

Blogu ya Haiti Grassroots Watch inasaili “malalamiko na tetesi kuhusu matumizi mabovu au hata matokeo yasiyotarajiwa ya misaada ya chakula.”

‘Mwanablogu Mzuri Lazima Awe na Sifa za Asili za Waandishi Wazuri wa Habari’

Dorothée Danedjo Fouba, mshindi wa tuzo ya “Blogu Bora ya Teknolojia Afrika, iliyotolewa Tuzo za Uandishi wa Kiraia za Telkom-Highway Africa 2013“, alizungumza na Dibussi Tande (@dibussi) kuhusu maendeleo yake katika tasnia hii, na sifa zinazohitajika ili kufanikiwa.

Mwenendo wa Mashitaka ya Wanasiasa wa Kenya Mjini Hague

Mashitaka ya Kenya Hague ni mradi wa Dawati la Afrika la Radio Netherlands Worldwide kwa ushirikiano na This is Africa (Hii ni Afrika):

Namna gani ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 na 2008 ziliathiri maisha yako? Unataka kufahamu nini kuhusu haki ya kimataifa? Changia habari ulizonazo, mawazo na maswali hapa, kupitia barua pepe (africa@rnw.nl), kwenye mtandao wa Facebook au Twita kwa alamahabari #HagueTrials.
Makala bora, blogu, video, picha na katuni zitachapishwa. Jisikie huru kuonyesha kama usingependa jina lako lijulikane.

Masuala Matano ambayo Raia wa Brunei Wanahitaji Kuyajadili

Teah Abdullah anaorodhesha masuala matano ambayo raia wa Brunei citizens wanahitaji kuyajadili: Kuimarisha lugha halisi, ngono baina ya ndugu wa damu, maisha ya anasa, ulaji unaozidi kiwango wa “baga” [aina ya mandazi yenye nyama], utegemezi uliopitiliza kwa serikali. Anafafanua kwenye suala la mwisho:

…serikali ni sehemu muhimu katika maisha yetu ya kila siku, lakini kuitegemea sana ni tatizo kwa sababu inakuwa kama hatuwezi kutatua matatizo yetu binafsi. Tunajiongezea matatizo kwa kutegemea kuwa serikali itatatua matatizo madogo yanayotusibu kwenye maisha yetu.

Nani ni Muislamu Halisi? -Hatari ya Madhehebu Madogo ya Waislamu Pakistan

Raza Habib Raja wa Pak Tea House ana maoni haya:

‘Kosa’ kubwa nchini Pakistani ni kuwa kile ninachokiita, Muislamu asiye Muislamu. Kwa hiyo hata ukiwa Ahmedi, Shiite, na hata muumini wa Mtakatifu Sufi bado utaitwa Asiye Muislamu na baadhi ya watu.

Hilo linatuleta kwenye swali “nani ni Muislamu?” Raja anaeleza:

Kuuliza swali hili ni hatari na kujaribu kufafanua maana hasa ya Muislamu kunaweza kuwa hakuna maana yoyote na kunaweza kusababisha kutengwa kwa wengi wasiokuwa dhehebu la mtu anayeuliza swali hilo.

Maandamano ya Wapinzani na wafuasi wa Jeshi Yaandaliwa Katika Viwanja vya Tahrir

Kwenye mtandao wa Twitter, Nancy anauliza kama chama cha FJP cha Muslim Brotherhoodhad kiemtumia bango lililotumika kwenye filamu ya Vita ya Dunia Z: Simulizi la Historia ya Vita ya Zombie, katika kuitisha maandamano yanayopangwa kuwa Oktoba 6:

Tamarod, ambayo inatafsirika kama uasi, pamoja na Muslim Brotherhood wameitisha maandamano mnamo Oktoba 6, ambayo yanaadhimisha tarehe 6 ya Oktoba au Vita vya Yom Kippur, kati ya Waarabu na Waisrael.

China: Miitikio ya Raia wa Mtandaoni Kufuatia Muswada wa Sheria ya Kurithi Kodi

Watumiaji wa mtandao nchini China walionyesha kutokuridhishwa kwao na muswada wa sheria unaopendekeza uwezekano wa kurithiwa kodi zinazoanzia yuan RMB 800,000 [yuan ni sarafu ya nchi hiyo]. Badala ya kuziba pengo la kipato miongoni mwa wananchi, watumiaji wa mtandao wanaamini kuwa sheria mpya inakusudia kuiba fedha kutoka kada ya wafanyakzi. Zaidi kutoka kwenye mtandao wa Offbeat China.

#EauSecours: AlamaHabari ya Kufanyia Mzaha Tatizo la Maji Dakar, Senegal

Dakar, mji kuu wa Senegal, umekumbwa na uhaba wa maji kwa siku 15 zilizopita  [fr]. Wa-Senegali katika mitandao ya kijamii wanazoea tatizo hili kwa kufanyiana utani na uvumilivu. AlamaHabari (Hashtag) #eausecours (#H2OUT) inatumika hivi sasa kwneye mtandao wa twita na  Facebook kutaniana kuhusiana na ukosefu wa maji safi unaoendelea, kama ilivyoonekana kwenye twiti hii :  

Ninawahisi jamaa zangu wote

 

Maadhimisho ya Miaka 30 ya Maandamano ya Usawa ya Wafaransa

Miaka 30 iliyopita (Oktoba 15, 1983), a maandamano ya usawa dhidi ya ubaguzi wa rangi [fr] yalianzia  Marseille  na watu 32, wengi wao wakiwa wenye asili ya Kiarabu, kwa kuomba haki ya kupiga kura na kitambulizo cha mkazi kwa miaka 10. Maandamano hayo yanayofahamika kama “Beur March” (Beur ni lahaja ya Kifaransa kwa watu wenye asili katika Afrika ya Kaskazini) yaliwasili mjini Paris, Desemba 3 na zaidi ya watu 60,000 baada ya kujiunga katika seti ya awali ya waandamanaji. Matukio mbalimbali yana adhimisha kumbukumbu ya miaka kote nchini Ufaransa, ingawa katika mazingira magumu kutokana na kupanda kwa kasi kwa mbali haki katika Ufaransa. Video zifuatazo ni moja ya makala mengi ya vyombo vya habari kuadhimisha miaka [fr]:

Kampeni ya Mtandaoni ya Kudai Amani Nchini Msumbiji

Blogu ya Mozmaniacos [pt] imezindua kampeni ya mtandaoni ya kudai amani nchini Msumbiji, kufuatia tishio la kuhatarisha amani iliyodumu kwa miaka 20 . Kwa kutumia kiungo habari #MozQuerPaz (#MozWantsPeace), watumiaji wa Facebook, Twitter, na Instagram waanza kuchangia picha zao pamoja na maoni yao kuhusiana na kampeni hii.

Vyuo Vikuu Vingi Mno Nchini Singapore?

Limpeh anabaini ongezeko kubwa la taasisi za eleimu ya juu nchini Singapore. Je, hizo ni habari njema au mbaya kwa nchi ya Singapore?

…kupanuka huku [kwa elimu ya juu] kumekuwa na matokeo mabaya kwa soko? Kwa hiyo wakati kupanuka huku kunaweza kuwa kumeongeza ajira kwa baadhi ya baadhi ya watu (jambo ambalo ni jema), lakini wazazi wangapi wanataka kuona watoto wao wakiishia kwenye vyuo hivi vinavyozalisha watu wasiokidhi mahitaji ya soko…

Fuatilia SafariYaGariAfrika Mtandaoni

Kikundi cha watengenezaji na wabunifu wa teknolojia kutoka Ulaya ambao wanadadisi ukuaji wa vituo vya teknolojia barani Afrika wanaendelea na safari yao ya gari barani humu.

Tazama blogu yao au Tumblr na ufuatilie mjadala kuhusu safari yao kwenye mtandao wa Twita.

Wali Unaonata Haufai kwa Watoto, Akina Mama Waambiwa

@LaotianMama anawakumbusha akina mama wa Lao kutokuwalisha watoto wenye njaa wali unaonata ambao ni chakula cha asili kwao.

Wali unaonata kwa watoto wachanga ni sawa na punje za wali katika utamaduni wa ki-Magharibi. Wazo ni lile lile kuwa kuwapa watoto wachanga chakula kigumu kutawashibisha. Kwa hiyo, kuwaanzishia watoto wachanga chakula ambacho ni kama hakina virutubisho zaidi ya kushibisha tu inaweza kuwa hatari kwa mfumo wa chakula ambao unakuwa bado haujaimarika vilivyo na kunaweza kusababisha matatizo ya mtoto kupata magonjwa yanayotokana na mwili wake “kukataa” chakula [allergies], anaweza kupata udumavu, na hata shida ya kutokunyonya ipasavyo.

India: Saa Nzuri Kapata Huduma za Afya Hospitalini kwa Punguzo la Bei

Kamayani wa mtandao wa Kracktivist anasema kuwa dhana ya saa nzuri kupata punguzp la bei, ambayo ni maarufu sana kwenye vilabu vya pombe, mahotelini na hata kwenye majengo ya sinema, imeingia hadi kwenye sekta ya afya nchini India. Hospitali binafsi iliyoko Bangalore siku za hivi karibuni imekuwa ikitoa punguzo la bei kati ya asilimia 30-75 kwa huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na uchunguzi, kufanyiwa vipimo vya x-ray na hata ushauri, wakati wa masaa yasiyo yasiyo na shughuli nyingi. Hosptali nyingine zinajiandaa kufuata mkondo huo hivi karibuni.

Hong Kong: Video Inayosambazwa Mtandoni Yamwonyesha Jamaa Akipigwa Makofi Mara 14 na Rafiki Yake wa Kike


Kama inavyoelezwa na Tom Grundy, mpita njia aliwaita polisi na mwanamke huyo aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumpiga vibao rafiki yake wa kiume aliyekuwa amepiga magoti mbele yake akimwomba msamaha kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani.

Korea Kusini: Mwandishi Msafiri, Utamaduni Tofauti, na Jamii ya Wageni

John Bocskay, mwanablogu asiyeandika mara nyingi sana alifanya mahojiano na mwandishi wa utalii Rolf Potts aliyetumia miaka kadhaa kwenye jiji la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini, Pusan, anasema:

Kila mtu niliyeonana naye katika vilabu vya wageni alidai kuwa mwandishi au msanii, lakini hungeweza kuona maandishi mengi au sanaa. Ilikuwa inaudhi na kuumiza, na sikuanza kuandika kuhusu Korea kwa namna ya maana mpaka nilipojifunza kuisogeza jamii hiyo ya wageni (marafiki na wafanyakazi wenzangu) karibu nami ili kuniwezesha kujifunza jiji hili, kwa mtazamo wa Kikorea.

Kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko la Balochistan

Zaidi ya watu 300,000 wameathirika kufuatia tetemeko la hivi karibuni katika wilaya sita za Jimbo la Balochistan nchini Pakistan. Kashif Aziz wa mtandao wa Chowrangi anatoa habari za namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la Balochistan.

Madaktari 400 wa Cuba Waenda Brazil

Daudi Oliveira de Souza, daktari na profesa wa Taasisi ya Utafiti wa Hospitali ya Sirio-Libanés, alituma barua ya wazi kwa madaktari zaidi ya mia nne wa Cuba ambao hivi karibuni waliwasili nchini Brazil wanaoanzisha kundi la kwanza la jumla ya madaktari 400 ambao wanatarajiwa kuja nchi hii kabla ya Desemba mwaka huu.

Maternal home in Cuba. (Foto: Randy Rodríguez Pagés)

Nyumba ya Wajawazito nchini Cuba. (Picha: Kurasa za Randy Rodríguez)

Chapisho la Missive, linalochapishwa na Folha kila siku kutoka Sao Paulo, linasema:

Karibu, madaktari wa Cuba. Mtakuwa muhimu sana kwa ajili ya Brazil. Ukosefu wa madaktari katika maeneo ya mbali kijijini umewafanya watu wetu kuwa katika hali ngumu. Msijali kuhusu uadui kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wetu. Mtapata fidia sana kwa makaribisho mazuri katika jamii ambazo mtatoa huduma kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa Oliveira de Souza, katika majimbo kama Sergipe, ni rahisi kuhama kutoka mji mkuu hadi miji ya Ndani, lakini hata hivyo kuna mamia, ya nafasi za kazi zisizotumika hata katika vitengo vya afya vyenye vifaa na vilivyoko katika hali nzuri.

Kabla ya upungufu wa madaktari 14,500 katika taifa la Amerika ya Kusini, serikali ya Dilma Rousseff ilipitisha sera ya “Mais Medicos” (mpango wa Madaktari Zaidi), ambayo itaweka mikataba na madaktari kutoka Hispania, Ureno, na Cuba, kati ya mataifa mengine.

Hivi karibuni, mmojawapo wa wakosoaji wakubwa wa makubaliano hayo na wa-Cuba anasema kwamba “walikuwa wanatumiwa bila faida.” Kwa hoja hii, Oliveira de Souza anasema:

Ni mapema mno kuongelea kama wao watafanya kazi kama watumwa. Panamerican Health Organization (PHO), yenye karne ya uzoefu, watakuwa washirika wazuri, tangu kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano na serikali ya Brazil. Nyuso zao za furaha katika viwanja vya ndege zilionyesha matumaini. Kwa lugha ya kijijini kwetu, kufuatia idadi kubwa ya madaktari wetu, naweza kusema tu kwa imani: nawakumbatia kindugu na asante sana.