Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Novemba, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Novemba, 2013

Kufuatilia Kongamano la Dunia la Demokrasia 2013

Kongamano la Dunia la Demokrasia kwa sasa linafanyika mjini Strasbourg, Ufaransa kwa mara ya ppili tangu lianze. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “kuunganisha Taasisi na Wananchi katika Kizazi hiki cha dijitali”. Fuatilia mada nne na warsha 21 za mkutano kupitia alama ashiria #CoE_WFD

logo WFD 2013

Alama ya WFD katika Strasbourg 2013 Picha kwa niaba ya Suzanne Lehn

Mkusanyiko wa Makala za Kuvuliwa Madaraka kwa Mbunge Maarufu Nchini Tanzania

Ben Taylor aweka mkusanyiko wa makala zinazohusiana na kuvuliwa madaraka kwa Zitto Kabwe,mbunge maarufu na kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Zitto:

[…] alivuliwa nyadhifa zote rasmi na viongozi wakuu wa chama mapema siku ya ijumaa asubuhi. Zitto Kabwe hatakuwa tena Naibu katibu Mkuu wa chama wala naibu kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani.

Sababu ni ipi? Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe, alieleza kuwa, Zitto aligundulika kuwa ni miongoni mwa waliohusika na njama za kumpindua mwenyekiti wa chama hicho na kuichukua nafasi hiyo (na bila shaka kuwania kiti cha Rais), pamoja na makosa mengine ya uvunjaji sheria ndani ya chama.

VIDEO: Serikali Yaharibu Misikiti Nchini Angola

Uharibifu wa misikiti isiyopungua 11 katika miezi miwili iliyopita nchini Angola imechochea athari ya hasira kwenye mtandao.

Kwa mujibu wa Voz da América [pt], Mamlaka ya Angola ilisema kuwa sababu ya uharibifu ni ujenzi kinyume cha sheria na ripoti&nyingine kuongeza kwamba mchakato wa kuhalalisha Uislamu na dini nyingine katika nchi haijawahi kupitishwa na Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu, na kwa hiyo, kwa mujibu wa shirika la habari ya mamlaka ya AngolaPress, “mahekalu zao zitafungwa hadi uamuzi mpya katika kesi. “Waziri wa Utamaduni, Rosa Cruz e Silva, alisema kuwa sheria inayohusiana na uhuru wa mkutano wa dini lazima iundwe upya “kama njia ya kupambana kwa ‘nguvu’ kuanzishwa kwa mkutano mpya za kidini ambazo mikutano yao ya dini ni kinyume na tabia zetu na forodha katika utamaduni wa Angola. “

Jumuiya ya Kiislamu ya Angola (CISA) inaona kuwa serikali inafanya mateso ya kidini na kuzuia utekelezaji wa ibada ya kidini. Hivyo imerejelea katika maelezo ya video zilizowekwa katika mtanda wa Youtube Septemba mwaka jana na Coque Manuel ambayo inaonyesha msikiti katika mji wa Moxico ikiharibiwa:

A destruição (…) deve ser imediatamente interrompida e exigimos ao Presidente Angola que peça desculpas aos muçulmanos em todo o mundo. Se não, então gostaríamos de convidar a comunidade Islâmica para realizar manifestações pacíficas em frente dos edifícios das embaixadas angolanas em todo o mundo.

MATOKEO: Tuzo za Kwanza za Uandishi wa Kiraia Kuwahi Kutolewa Uganda

Tuzo za kwanza za uandishi wa kiraia nchini Uganda (SMAs) zilitolewa kwa mara ya kwanza Novemba 15, 2013 kwenye kituo cha Teknolojia kiitwacho The Hub, kwenye mtaa wa maduka ya Oasis jijini Kampala, Uganda.

Social Media Awards 2013 banner.

Bango la Tuzo za Uandishi wa Kiraia za mwaka 2013.

Malengo ya tuzo hizo, ambayo iliandaliwa na BluFlamingo, yalikuwa:

Tuzo hizi za Uandishi wa habari za kiraia za tukio la kwanza linalotafuta kuwaleta pamoja watu binafsi na mashirika ambayo yako mstari wa mbele linapokuja suala la kutumia vyombo vya habari za kiraia kwa minajili ya burudani, kuleta mabadiliko, kubadilishana mawazo, kutengeneza jumuiya na kuwasiliana na wateja mtandaoni.

Tuzo hizo zinalenga kuwatuza watu na mashirika yanayofanya jitihada za dhati kuupa nguvu uandishi wa kiraia ili kuhusika na kujenga jumuiya mtandaoni kuanzia kwa watumiaji wa mtandao wa Facebook mpaka watumiaji wa mtandao wa twita na wanablogu wanaojituma.

Tukio la kwanza kama hili lilifanyika Novemba 15 2013 na liliwaleta si tu watu wanaojua masuala ya kidijitali, lakini pia mashirika makubwa yaliyo mstari wa mbele katika uandishi huu mpya na wale walioshiriki katika kukuza uandishi wa habari za kiraia nchini Uganda.

Washindi wa kila kundi walikuwa kama ifuatavyo:

Tovuti bora ya burudani – BigEye
Mwandishi bora wa Burudani – Moses Serugo
Mwanablogu bora – Beewol

Kampuni kubwa bora – MTN Uganda

News & kampuni ya habari – NTV Uganda
News & habari za watu – Songa Stone

Huduma za Umma bora – Mamlaka ya Jiji la Kampala
Ubunifu bora – Matatu
Huduma bora za wateja – Airtel Uganda

Haki za jamii – Wanasheria pekupeku Uganda
Tuzo ya Udhibiti ya Majanga – Shirika la Taifa la MajiSafi na MajiTaka
Shirika bora la kuchapisha habari – The Red Pepper

Radio bora – Power FM
Runinga bora – NTV Uganda
Mtu maarufu – Anne Kansiime

Upigaji picha – Echwalu Photography
Kampeni bora ya uandishi wa kiraia – 40 & tabasamu 40
Chaguzo la Jaji – Proggie Uganda

Washindi walipendekezwa kupitia upigaji kura wa mtandaoni na baadae walichaguliwa na jopo la Majaji watano.

VIDEO: “Wao Hufanya kazi na kufa”, Ugonjwa Usioeleweka Yawaua Wafanyakazi wa Miwa wa Amerika ya Kati

Wafanyakazi ambao hukata miwa na mazao mengine katika tambarare ya pwani ya Amerika ya Kati na wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu:

Kutoka Panama hadi kusini mwa Mexico, wafanyakazi wamashikwa na na maradhi ya kushindwa kwa figo katika viwango vya ghaibu amabavyo havijaonekana mahali popote duniani. Familia na vijiji imekumbwa na hasara ya vizazi karibu yote ya watu.

Tangu mwaka 2000, ugonjwa sugu wa figo imeua zaidi ya watu 24,000 katika El Salvador na Nikaragua, nchi mbili ambazo zimeathirika zaidi na janga hilo.

Uchunguzi zaidi wa kisayansi umeanza tu katika jamii zilozo adthiriwa na ugonjwa, na ukweli mchache kuanzishwa, lakini wanasayansi nwamezindua kile wanachokiamini kuwa wazo la kuaminika. Wanasema kuwa chanzo cha ugonjwa kuonekana mdomoni asili kwa kazi inayofanywa na waathirika wake.

Esteban Félix, mpiga picha wa Peru kutoka Shirika la vyombo vya habari, anatoa kumbukumbu ya athari za janga katika Chichigalpa, Nicaragua, moja ya jamii kuathirika zaidi.

Shukrani kwa kazi yake, Félix alipokea tuzo la uandishi wa habari la Gabriel García Marquez  [es] mwaka huu katika uandishi wa habari kitengo cha picha.

Katika video hii, iliyo haririwa na (@albamoraroca) na muziki kwa niaba ya Dan Bality, Félix anaelezea hadithi nyuma ya picha ambazo yeye alichukua wakati wa kukaa kwake katika Chichigalpa. Kwa maneno yake mwenyewe, Félix anatoa muhtasari::

Uno trabaja para vivir, pero en realidad esta gente trabaja para morir.

Baadhi ya watu kufanya kazi kwa kuishi, lakini hapa, watu kufanya kazi kufa.

Sukari chungu: Ugonjwa wa ajabu kutokaAlba Mora kwenyeVimeo.

Wasanii wa Brazil Waungana Kuwahifadhi Simba Nchini Kenya

Leo Vultus by Murillo Martinsfor the campaign Run4Run4Lions.

Leo Vultus kwa niaba ya Murillo Martins kwa kampeni ya Run4Run4Lions.

Baada ya uchapishaji wa pamoja #sobreontem (kuhusu jana) katika kusaidia harakati [pt] ambayo ilianzishamaandamano haya Juni iliyopita mjini São Paulo, wasanii wa Brazil sasa wanajiunga pamoja kwa sababu mpya. Wakati huu, kazi yao ni dhidi ya kuuawa kwa simba katika mkoa wa Samburu, Kenya.

Wenyeji wa mkoa wanatumia sumu na silaha nyingine dhidi ya simba ambao huwashambulia mbuzi wao. Kuongeza kuelewa kwa umma kuhusu suala hili, katika mwaka 2010 Mradi wa Ewaso wa Simba uliandaa mbio za nusu-marathon kwa lengo la “kutuliza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori kwa kushirikisha jamii katika uhifadhi wa simba.” Kwa waandaaji, sehemu ya ufumbuzi wa tatizo ni “mbuzi za bure zaidi”, na ni kwamba katika tukio la kwanza mwaka 2010, zawadi ya kushinda mbio walikuwa mbuzi.

Sasa mradi unafanya maandalizi ya mashindano ya pili na kampeni crowdfunding #Run4Run4Lions, ambayo itakusanya fedha kwa ajili ya mbio za nusu-marathon mwaka wa 2014. Michoro ya awali ya Wasanii wa Brazil (ambayo baadhi ya vipande tayari vimeuzwa) inayotolewa kama fidia kwa wale ambao wanasaidia mradi.

Kujifunza zaidi kuhusu kampeni

Ecuador: “Harakati ya Kiasili Itaendelea”

“Serikali inaweza kuendelea na jitihada zake za kutufanya sisi kutosikika, lakini mapambano yetu hayawezi kushindwa. Bora kuna ukosefu wa haki, na kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya mijini na vijijini kubaki, harakati ya kiasili itaendelea.”

Manuela Picq alizungumza na Carlos Pérez Guartambel, kiongozi wa sasa wa Ecuarunari [es] (Shirikisho la Kichwa la Ecuador), katika tukio lililo fadhiliwa na NACLA (North American Congress on Latin America) na CLACS (Center for Latin American and Caribbean Studies at New York University). NACLA imechapisha nakala ya mazungumzo.

Tajikistan: Wapiga Kura Wana Haki ya Kujua Kama Wagombea “Wameshiba’ au ‘Wana Njaa’

Kama mtandao wa Sauti za Dunia ulivyoripoti, baadhi ya raia wa mtandaoni wanasema watampigia rais anayemaliza muda wake wakati wa uchaguzi wa Novemba 6 katika Tajikistan kwa sababu “kiongozi aliyeshiba ni bora kuliko aliye njaa”. Kutafakari juu ya hili, Salimi Aioubzod anadokeza [tj] ni “huzuni” kuwa wapiga kura katika nchi wasiwasi wao zaidi ni kuhusu “shibe” au “njaa” ya mgombea urais= kuliko kuhusu jukwaa la mgombea. Hata hivyo mwanablogu anasema kuwa kama wapiga kura wanataka kujua namna mgombea wao “alivyoshiba” basi wana haki ya kujua hayo:

…itakuwa vizuri kama Tume ya Mpito ya Uchaguzi na kura ya maoni ya Tajikistan (CCERT) kuwataka wagombea wote wa urais kutangaza mapato yao ya kila mwaka na vyanzo vyake …

Kutangaza kwa umma mapato ya mgombea na asili yake, mali yao halisi, na akaunti ya benki yao itaruhusu [wapiga kura], ili kuona kama mgombea ni “kashiba” au “njaa” tupu…

Udadisi wa Sami Anan

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais?

Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.

FIFA Yazipiga Faini Croatia na Ugiriki kwa Tabia ya Mashabiki ya Ubaguzi wa Rangi

Mnamo Novemba 2013, Croatia ilijiunga na orodha ya kuongezeka kwa timu za taifa za kandanda ambazo FIFA imezipiga faini kwa ajili ya tabia za ubaguzi wa rangi ya mashabiki wao au wajumbe wa timu. Mwezi Mei 2013, FIFA ilianza kutekeleza vikwazo vikali dhidi ya ukabila na ubaguzi. Rais wa FIFA Sepp Blatter alisema hivi karibuni kwamba chama cha kimataifa zinazosimamia asasi lazima zitoe adhabu kali kupambana na masuala haya, na kuongeza kuwa FIFA kwa sasa iko tayari “kuondoa timu kutoka ushindani au kupunguza pointi” kufuatia athari hiyo. Al Jazeera inaripoti maelezo zaidi kuhusu faini iliyotolewa kwa vyama kitaifa vya soka vya Croatia na Ugiriki:

FIFA ililipiga faini Shirikisho la Soka la Croatia 35,000 faranga ya Uswisi ($ 38,000) kwa ajili ya matukio wakati wa kushindwa kwake kwa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji nchini Zagreb Oktoba 11.

“Wafuasi wa Kikroeshia walionyesha saluti ambazo zilitumika wakati wa Vita Kuu vya II na harakati mabavu ya Ustase,” kundi la mashabiki la ufuatiliaji liliripoti kwa FIFA.

FIFA iliipiga faini shirikisho la Kigiriki 30,000 faranga ya Uswisi ($ 32,500) kufuatia taarifa ya mabango yaliyoonyeshwa wakati Ugiriki iliwashinda Slovakia 1-0 mjini Athens Oktoba 11.

Onesho la Mitindo Nchini Japan na Kauli Mbiu ya Kusitishwa kwa Matumizi ya Nguvu Dhidi ya Wanawake

Image from last year's fashion show. The two models look like

Picha ya maonesho ya mitindo iliyopigwa wakati wa onesho la mwaka jana. wapenzi hawa wanaonekana kwa nje wanafuraha, lakini mkono wa mwanamke huyu umefungwa pamoja na mkono wa mwanaume. Mkono wa kushoto wa mwanaume, ameshika bunduki isiyo halisi. Picha hii iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Umoja wa Wanawake wa Asia (AWA).

The Umoja wa Wanawake wa Asia, shirika lisilo la kimaslahi la kutetea haki za wanawake, linategemewa kusimamia ; onesho la mitindo  [ja] siku ya tarehe 1 Desemba, 2013 likiwa na kauli mbiu isemayo “Mtindo wa Kukabiliana na Mfumo Kandamizi” yenye lengo la kuvuta hisia za watu katika kukabiliana na suala la matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake. Onesho zima la mwaka jana linaweza kutazamwa hapa.

Wanasayansi Kutoka Duniani Kote Wakusanyika Nchini Brazil

World Science Forum

Kongamano la Dunia la Sayansi

Jukwaa la Sayansi Duniani (WSF) linajumuisha mamia ya wanasayansi kutoka duniani kote wiki hii nchini Brazil, kujadili wajibu wao katika karne ya 21 na kusisitiza umuhimu wa ushauri wa kisayansi katika maamuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Brazil imekuwa mwenyeji wa matukio kadhaa ya kujadili kuondoa umaskini na maendeleo endelevu kutoka katika mtazamo wa makundi mbalimbali ya kijamii, mara kwa mara maadui, kama vile Rio +20, na mkutano wa watu na Kongamano la Kijamii DunianiMtandao katika lugha ya Kiingereza, lugha rasmi ya tukio hilo, na itajumuishwa katika mitandao ya kijamii kupitia alama ashiria #WSFBRAZIL.

Iran: Mwanablogu Aliyefungwa Jela Ahitaji Huduma ya Matibabu ya Haraka

Mwanablogu aliyefungwa jela,Hossein Ronaghi Maleki anahitaji huduma ya matibabu ya haraka. Alihukumiwa kifungo cha jela cha miaka 15. Laleh alitwiti

Sera ya Taarifa ya Uwazi Yahitaji Kuboreshwa zaidi Nchini Japan

Open Data Index

Screenshot of Open Data Index

Pamoja na kuwa serikali ya Japan inajitahidi kupiga hatua katika uboreshaji wa sera yake ya uwazi, nchi hii bado ina safari ndefu, kwani imeshika nafasi ya 30 kati ya nchi 70, kwa mujibu wa orodha liyoandaliwa na Asasi ya Ujuzi Huru. Masahiko Shoji wa Asasi ya Ujuzi Huru nchini Japani aandika:

日本は、政府支出、企業登記情報、交通時刻表、立法の分野で低い評価を受けました。また、どの項目もオープンライセンスの採用については「Yes」の評価を得ませんでした。これらの課題は6月に発表されたG8諸国における速報の時点と同じであり、日本の取り組みが大きくが進んでいないことを表しています。

Taaarifa huru za Japani kuhusiana na matumizi ya serikali, usajili wa makampuni, ratiba za usafiri na vyombo vya mahakama vilipata uungwaji mkono usioridhisha. Sehemu za taarifa hizi hazikupata tathmini ya “ndio”. changamoto kama hizi zinafanana na zile za viwango vya wanachama wa kundi la G8 vilivyotolewa mwezi Juni mwaka huu na Asasi ya Ujuzi Huru inayoonesha kuwa juhudi za Japani za kuboresha sera ya uwazi bado ni ndogo.

Kujua zaidi kuhusu vigezo vinavyozingatiwa katika kuweka viwango, tafadhali tembelea here

Je, Ni Mipango Ipi Xi Anayo kwa Vyombo vya Habari Nchini China?

David Bandurski kutoka mradi wa vyombo vya habari nchini China anaangalia jinsi sera ya vyombo vya habari ya uongozi mpya wa Chama cha Kikomunisti ya Kichina, hasa baada ya mkutano wa Tatu wa Plenum. Dhidi ya kinyume cha hali ya mazingira mapya ya kitaifa ya usalama wa kamati, swali la kushughulikiwa ni:

Jinsi gani chama kuifanya upya na kutafsiri mfumo wake kwa mtandao na vyombo vya habari vya kijamii katika mwanga wa kubadili mtazamo wake kwa usalama wa taifa?

Wimbi la Ukatili Dhidi ya Waandishi wa Habari Nchini Guatemala

Mwandishi wa habari wa Guatemala Carlos Alberto Orellana Chávez alipigwa risasi mnano Jumatatu Agosti 19, 2013, yeye ni mwandishi wa habari wa nne kuuawa nchini Guatemala mwaka huu.

Katika makala ya maoni [es] iliyochapishwa katika gazeti la Guatemala Prensa Libre, mwandishi maalum wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uhuru wa kujieleza Frank La Rue alishutumu “wimbi la hivi karibuni la ushambulizi dhidi ya waandishi nchini,” kama Alejandro Martinez anavyoripoti katika Uandishi wa Habari wa The Knight Centre katika blogu ya Amerika:

La Rue alikosoa utawala wa Rais Otto Perez Molina kwa kushindwa kuzuia uhalifu nchini, kipendeleo kwa maslahi binafsi, kutesa viongozi wa kijamii na kutolinda waandishi wa habari kutoka unyanyasaji wa mahakama, kesi za kisheria, vitisho, ushambulizi wa kimwili na mauaji.

“Leo vurugu imegeuka kuelekea sekta ya vyombo vya habari ambayo inashikilia nafasi muhimu kuelekea wale walio katika madaraka, kwa sababu ya kazi yao ya kijamii ya kuchunguza na kutoa taarifa, lakini kiwango cha mwaka huu cha ushambulizi hakijaonekana katika muongo mmoja,” alisema La Rue, ambaye alielezea vurugu kama “hatua ya nyuma kwa ajili ya demokrasia na (nchi) mchakato wa amani.”

PICHA: Mkutano wa Chama Kikuu cha Upinzani Msumbiji cha Shambuliwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia

The arrival of two cars with officers from the Rapid Intervention Force (FIR) of the Police of the Republic of Mozambique (PRM) interrupted the final rally of the campaign of opposition party MDM in Beira. Photo @Verdade newspaper (CC BY 2.0)

Kuwasili kwa magari mawili na walinzi kutoka kwa Jeshi la Kutuliza Ghasia (FIR) na Polisi wa Jamhuri ya Msumbiji (PRM) kulileta ghasia katika mkutano wa hadhara wa mwisho wa kampeni ya chama cha upinzani cha MDM katika Beira. Picha @Verdade newspaper (CC BY 2.0)

Mkutano wa hadhara wa mwisho kwa kampeni ya umeya wa chama cha upinzani cha MDM katika Beira ulimalizika kwa watu watatu kuuawa na kadhaa kujeruhiwa – waliojeruhiwa ni pamoja na mwana wa mgombea – kufuatia mashambulizi ya polisi wa kutuliza ghasia ambao walitumia mabomu ya kutoa machozi na kufyatua risasi kwa hewa.

Wakati ghasia zinaanza, Meya anayemaliza muda wake Daviz Simango alikuwa anajianda kwenda kwenye jukwaa kutoa wito kwa umati wa watu kupigia kura kwa mara nyingine tena chama kikuu cha upinzani MDM (Mozambique Democratic Movement), ili kishike madaraka ya mji mkubwa wa pili kwa ukubwa nchini Msumbiji, pia mji mkuu wa jimbo la Sofala.

Machafuko katika mji huo wa Beira yalianza Novemba 16, na ya pili siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa manisipaa nchini Msumbiji. Uchaguzi utafanyika Novemba 20, 2013. @ Verdade gazeti linakusanya taarifa za kiraia katika tovuti maalum kwa ajili ya uchaguzi.

"Unrest set in and citizens tried to flee in disarray while FIR agents kept shooting. "

Machafuko yalipoanza na wananchi walijaribu kukimbia eneo hilo wakati kikosi cha FIR kikiendelea kufyatua risasi. “Picha kwa hisani ya gazeti @ Verdade kwenye Flickr (CC NA 2.0)

After the attack of the riot police, the crowd started to burn tires in the roads that lead to Beira´s neighborhood of Munhava.

Baada ya mashambulizi ya askari wa kutuliza ghasia, umati ulianza kuchoma matairi katika barabara inayoelekea mji jirani wa Beira Munhava (16/11/2013). Picha kwa niaba ya Miguel Mangueze gazeti la @Verdade (CC BY

India: Watu Zaidi ya Milioni 60 Wanaugua Ugojwa wa Kisukari

Ikiwa na watu zaidi ya milioni 60 wanaougua ugojwa wa kisukari [pdf] na wengine wanaokadiriwa kufikia milioni 77 walio katika hatihati ya kuugua ugojwa huu, nchi ya India inajikuta katika vita kali ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa kisukari. Katika siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 14 Novemba, India imedhamiria kukabiliana na janga la kuongezeka kwa wagonjwa wa kisukari ambao kwa sasa ni tishio nchini humo.

Mwandishi na mwanablogu Prem Rao, aweka bayana dalili anuai za ugonjwa wa kisukari na apendekeza kuwa, kwa wale wote ambao hawajapima kiwango cha sukari/ ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha miezi sita iliyopita, bila kupoteza muda, wakapime.

Misri: “Morsi Hatarudi Madarakani”

Aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hatarudi madarakani, anasema mwanablogu wa Misri Alya Gadi, kwenye mtandao wa Twita. Kuufanya ujumbe wake wazi, ametafsiri kwa lugha mbalimbali:

Mwezi Julai, utawala wa Morsi wa mwaka mmoja ulikatizwa , baada ya maandamano makubwa kote Misri kutoa wito ajiuzulu ulioanza Juni 30.

Serbia Yaibua Maswali Ikiwa Kanisa Lastahili Kusamehewa Kodi

Nchini Serbia ripoti ya uchuguzi uliofanywa na shirika la Serbia la kila siku liitwalo Blic ikiwa Kanisa la Kisabia la Orthodox, ambao viongozi wao hivi karibuni wamekuwa katika vyombo vya habari mara nyingi kutokana na ripoti ya matumizi ya anasa yaonyesha sasa lazima kuanza kulipa kodi. Kanisa la Kisabia la Orthodox taasisi zingine zote za kidini yana msamaha wa kutolipa kodi nchini Serbia na mamlaka ya serikali ya kodi hawajawahi kukagua fedha ya jamii yoyote iliyosajiliwa kidini nchini humo. Faida hizi, hata hivyo, hutumika tu kwa bidhaa na huduma zinazotumika kwa ajili ya shughuli za kidini, wakati Kanisa la Serbia la Orthodox inajulikana kuwa na aina mbalimbali za magari ya gharama kubwa katika umiliki wa Kanisa, zinazotumiwa na viongozi wake na wafanyakazi. Katika uchaguzi wa umma uliofanywa na Blic mapema mwezi Novemba 2013, 83% ya washiriki walisema Kanisa la Kisabia la Orthodox wanapaswa kulipa kodi.

Takribani makadirio, inayotokana na kauli ya vigogo wa kanisa, inaonyesha kuwa tu kutoka kwa VAT kwenye mauzo ya vitabu na bidhaa nyingine katika maduka ya kanisa, kama vile faida ya kodi, bajeti ya Jamhuri inaweza kuwa tajiri kwa dinar zipatazo bilioni 10 (€ 6,400,000 / dola milioni 8.5).