Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Juni, 2015

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Juni, 2015

Wanawake Wanaovaa Nusu Uchi Wataiokoa Sekta ya Utalii Kenya?

Je, kutembea uchi yanaweza kuwa mbinu bora ya kufufua sekta ya utalii nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabaab?:

Seneta mteule, Mbura anasemekana kuwaomba wanawake katika mkoa wa pwani kutembea nusu uchi ili kuwavutia watalii zaidi kuzuru eneo hilo. Wito huo umeibua maswali kuhusiana na thamani ya mwanamke wa pwani. Je, ndicho anachostahili kuwa – chombo cha biashara?

Kwa nini Tarakimu 64, 89 na 535 Hazipatikani Kwenye Mtandao wa Intaneti China?

Leo ni Juni 4, maadhimisho ya 26 ya maandamano ya kudai demokrasia ya Tiananmen mwaka 1989.

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya tarakimu zimepotea kwenye mtandao wa Intaneti nchini China kwa sababu ya udhibiti wa taarifa. Tarakimu hizi ni 64, 89 na 535 —zenye kuunganisha kupata Mei 35, namna maarufu yakukumbuka siku ya Juni 4. Tarakimu hizo hazitafutiki kwenye tovuti za kutafutia taarifa na haziwezi kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Mchora katuni za kisiasa Biantailajiao, kupitia mtandao wa twita, alionesha namna hiyo ya kijinga ya kujaribu kufuta historia:

Kama inawezekana, wanaweza kuifuta kabisa tarehe hii kwenye kalenda.

Ramani Hizi Zaonesha Mahali Walipotesewa na Kuuawa Wanahabari wa Kambodia

harassment_of_media_cambodiaKituo cha Haki za Binadamu cha kambodia kimezindua jarida linaloelezea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa waandishi wa habari nchini Kambodia. Katiba ya nchini Kambodia inatoa uhuru wa kupashana habari lakini wanahabari wanazidi kunyanyaswa na kuuawa, hususani kwa waandishi wanaopasha habari kuhusiana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na maafisa wa serikali pamoja na upashaji habari wa masuala ya kibiashara yanayohusishwa na viongozi wakubwa serikalini.

Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?

Protests in Niamey, Niger via Abdoulaye Hamidou on twitter (with his permission)

Maandamano mjini Niamey, Naija kupitia kwenye ukurasa wa Abdoulaye Hamidou kwenye mtandao wa Twita (kwa ruhusa yake)

Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo. Serikali iliachia ngazi nchini Burkina Faso wakati uchaguzi ukiahirishwa nchini Burundi. Mwezi Mei, wananchi wa Lome waliandamana kupinga matokeo ya urais  yaliyompa ushindi rais Faure Gnassingbe aliyeshinda kwa muhula wa tatu.

Kuhusu Uamuzi wa Mahakama wa Haki ya Kusaidiwa Kufa Nchini Afrika Kusini

Profesa Pierre de Vos anaingia rasmi kwenye mjadala mkali kuhusu uwezekano wa kumsaidia mtu kufa nchini Afrika Kusini baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuamua kwamba mtu anayekufa ana haki ya kusaidiwa kufa na daktari ili aweze kuyahitimisha maisha yake:

Ni muhimu kuona kwamba hukumu hii haimlazimishi mtu kuyakatisha maisha yake au kumsaidia mtu kufanya hivyo. Hilo bado linabaki kuwa uamuzi wa mtu binafsi. Hukumu hii inaweka msisitizo wa sheria ya makosa ya jinai (au, ningeongeza, sheria ya maadili ya Baraza la Watumishi wa Sekta ya Afya Afrika Kusini [HPCSA] kwamba haiwezekani kutekeleza jambo lolote lililo kinyume na misimamo ya kidini au kimaadili kwa mtu yeyote. Hata hivyo, hayo haiwalazimishi wale wenye imani hizo kuweza kuvunja imani zao wenyewe.

Zaidi, kama Mahakama ya Katiba itapitisha hukumu hiyo basi itafaa kwa Bunge kupitisha mfumo utakaowalinda wagonjwa. Bila sheria hizo mgonjwa atapaswa kwenda mahakamani kupata ruhusa ya kusaidiwa kufa.