Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Aprili, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Aprili, 2014

Kurekebisha Historia: Sauti ya Wahanga Waliolazimishwa Kuwa ‘Wagumba’ Nchini Peru

Likiwa na lengo la kukusanya saini 3,000, shirika la MujeresMundi limeanzisha madai ya mtandaoni kwenye jukwaa la Change.org likiitaka serikali ya Peru kujenga upya kumbukumbu ya kihistoria kwa sauti ya wahanga wa dawa za ugumba:

[…] kipindi cha pili cha serikali ya Alberto Fujimori; sera ya Taifa ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango ilitekelezwa […] sera hiyo ilikusudia kupunga kasi ya uzazi. Uchunguzi wa hivi karibuni uliwajumuisha wanawake 2,000. Hata hivyo, takwimu na nyaraka zinaonyesha kuwa kardi ya wanawake laki tatu wa vijijini nchini humo walilazimishwa kufanywa wagumba kwa nguvu wakati wa kipindi hicho.

Mashabiki Jijini Skopje Wakusanyika Kubadilishana ‘Stika’ za Soka

Mamia ya watu walikusanyika mchana wa Jumapili kwenye eneo la wazi jijini Skopje kubadilishana ‘stika’ za mkusanyiko rasmi wa picha za Kombe la Dunia la FIFA tarehe 28 Aprili, 2014.

Sticker exchange in Skopje, Macedonia on April 27, 2014.

Watu wa rika zote wakibadilishana ‘stika’ kwenye bustani ya wazi jijini Skopje. Picha: F.S. (CC-BY)

Nchini Macedonia, kama ilivyo kwa nchi nyinginezo za Yugoslavia ya zamani, utamaduni wa kukusanya ‘stika’ una historia ndefu, inaanzia miaka ya 1970 na albamu za ‘stika’ sasa zinauzwa. Watu wazima hushiriki kubadilishana ‘bidhaa’ hiyo sambamba na watoto na matoleo yaliyo maarufu ni pamoja Panini zinazotoka Italia na Kraš (Kundi la wanyama) zinazotoka Kroashia. Mwaka 2006, mtengeneza program za kompyuta aitwaye Goran Slakeski alianzisha tovuti za slikicki.com [mk, en, si] ambazo zimekuwa kitovu cha jamii ya watu wanaopenda kubadilishana ‘stika’, akipanua wigo mara chache kwenda kwenye matukio halisi mtaani kama hili lililofanyika.

Hadhi ya Wanawake Katika Jamii ya Kihindi Leo

Transhuman Collective (THC), mwanafunzi aliyepikwa na Soham Sarcar & Snehali Shah, ni mradi wa taaluma shirikishi unaongozwa na falsafa yaTranshumanism. Katika video hii iliyotengenezwa na kupandishwa kwenye mtandao wa YouTube na Transhumanism inaonyesha kuwa kunakosekana heshima ya msingi kwa wanawake katika jamii ya Kihindi iliyokithiri mfumo dume. Video hii inachangia kwa kiasi kikubwa kubadili fikra na mitazamo ya jamii ya Wahindi.

Changamoto ya Kuhuisha Orodha ya Wapiga Kura

Uchaguzi mkubwa zaidi duniani uko mbioni nchini India na mwanablogu Anuradha Shankar kwenye blogu yake ya “A Wandering Mind” anabainisha changangamoto halisi za kuboresha daftari la wapiga kura tayari kwa matumizi.

Waziri Mkuu wa Zamani wa Malayasia Aitaka Boeing Kuwajibika kwa Ajali ya Ndege MH370

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad ameitaka Boeing kuwajibika kufuatia tukio la kupotea kwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye blogu yake:

Boeing ndiyo imetengeneza ndege hii. Boeing lazima waeleze inakuwaje njia zote za kuifuatilia mwenendo wa ndege hiyo ziweze kuzimwa. Ni ama teknolojia ya Boeing ni duni au haina uhakika. Sitapenda tena kupanda ndege ya Boeing mpaka waeleze kwa nini mifumo yake yote inaweza kuzima kienyeji au kushindwa kufanya kazi.

Boeing lazima wakubali kuwajibika kwa kutengeneza ndege ambayo ingeweza kupotea tu hewani na isionekane tena.

Hedhi Sio Siri ya Aibu. Tuzungumzie Siku Zetu kwa Uwazi

“Kwa nini wanawake hawapendi kuzungumzia hedhi?”

anauliza Sourav Kumar Panda kwenye tovuti ya Youth Ki Awaaz na anaendelea kujadili/a> kuwa kwenye siku hizi na zama za leo, kuendelea kuifanya hedhi kuwa suala la kuficha haina maana -wakati umefika kwetu kuvunja kimya na kuacha woga wa mila za jamii zetu kuhusiana na siku zetu.

Gazeti la Kifaransa Lachapisha Chati Inayoonyesha Mataifa Yanayoongoza kwa Uhalifu

Gazeti la Le Progrès la jijini Lyon, Ufaransa ilichapisha chati [fr] yenye jina la “”Délinquance : à chacun sa spécialité – principales nationalités impliquées” (Uhalifu: Mataifa yanayohusishwa zaidi na [kila aina ya uhalifu]) (Ona picha katika mtandao wa twita hapa chini):

Katika machapisho yake ya kila siku, gazeti la Le Progres ilithubutu kuchapisha ulinganisho wa viwango vya uhalifu katika mataifa mbalimbali

Thibeau Perezat anabainisha kuwa gazeti hilo hata hivyo halikutaja vyanzo vya takwimu hizo. Mchangiaji wa Global Voices Julie Owono alisema kwamba gazeti lilishindwa kutofautisha kuwa “Waafrika” au “Roma” si mataifa.

M-Misri Atumia Mtandao wa YouTube Kupinga Kutumikia Jeshi kwa Lazima

Mwanaharakati wa Misri ametumia mtandao wa YouTube kuelezea anavyopinga utaratibu wa kulitumikia jeshi kwa lazima kwa raia wenye umri wa miaka kati ya 18 na 30.

Katika barua pepe aliyoituma kwa Global Voices mtandaoni, Adam anaandika:

Mimi ni Mmisri mwangalifu ninayepinga kwa nguvu zote utaratibu wa kulitumikia Jeshi la Misri lazima kwa sababu nachukia vita na ghasia. Nilirekodi video hiyo kwa lugha ya Kiarabu na kuitafsiri kwa kiingereza. Natumaini mtaiweka katika matangazo ya idhaa ya televisheni yenu ili Wamisri na dunia yote iweze kujua maoni yangu kwa sababu watu kama mimi tunaopinga kujiunga na jeshi kwa lazima hatupewi nafasi ya sauti zetu kusikika kwenye vyombo vya habari. Ni matumaini yangu kwamba mtanisaidia kwa sababu nataka Wa-Misri wawe huru kutoka utawala wa kijeshi na utawala wa dini. Naunga mkono demokrasia ya Magharibi.

Katika video hii, tafsiri ya maandishi katika lugha ya Kiingereza, Ahmed (Adam) anasema:

Mimi ni Ahmad (jina la utani Adam) kutoka Misri. Nitakueleza namna utaratibu wa kulazimisha kutumikia jeshi unavyofanyika nchini Misri. Napinga kwa nguvu zote utaratibu huu, na ninakataa kutumika katika Jeshi la Misri kwa sababu ni jeshi la jinai linalowauwa maelfu ya waandamanaji na watu wasio na hatia katika barabara ya Mohamed Mahmoud na Tahrir Square jijini Cairo na maeneo mengi katika Misri.

Anaongeza:

Kutumikia jeshi kwa lazima ni udhalilishaji, utumwa, na kazi ya kulazimishwa kwa maelfu ya Wamisri maskini ambao kila mwaka wanalazimishwa kufanya kazi katika biashara binafsi na mashamba ya majenerali wa jeshi la Misri bila malipo yoyote au mshahara. Askari yeyote ya Misri [ambaye] ametumikia katika jeshi anajua vizuri sana mikopo mikubwa majenerali wa jeshi inayoingizwa kwenye akaunti zao za benki. Pia, majenerali wa jeshi wanamiliki mali halisi ya mali isiyohamishika waliyoipata kwa njia haramu. Wanaiba utajiri wa nchi na mali.

Adam anaelezea:

Kulitumikia jeshi kwa lazima ni utaratibu usiokuwepo kokote kwa ajili ya maendeleo, iwe kwenye nchi yoyote ya Magharibi, wala Marekani.

Asilimia 20-40% ya Fedha Katika Sekta ya Maji Barani Afrika Hupotelea kwa Utoaji Rushwa

Upatikanaji wa maji ni haki ya binadamu. Chanzo: actionaid.org kwa ruhusa

Mustapha Sesay, Balozi wa Uadilifu wa Afrika Magharibi aliandika kuhusu ufisadi katika sekta ya maji kwenye mtandao wa Waandishi wa Habari wa WASH wa Afrika Magharibi :

Suala la upatikanaji wa maji safi na kwa bei nafuu ni haki ya kibinadamu lakini hii haijapewa kipaumbele inavyohitajika sana. Utoaji rushwa katika sekta ya maji ni jambo la kawaida na inahusisha madaraja yote ya watu kuanzia mtu wa kawaida, wanasiasa, Wakuu wa Taasisi ya Maji na hata mashirika yasiyo ya serikali wanaofanya kazi katika hii sekta. Ripoti juu ya “Utoaji rushwa katika sekta ya maji” kupitia mtandao wa Uadilifu wa maji katika kitabu chenye jina la “Mafunzo ya Mwongozo wa Uadilifu wa maji ” inasema kwamba katika jangwa la Sahara Afrika, asilimia arobaini na nne (44%) ya nchi haina uwezekano wa kufikia lengo la Maendeleo ya Milenia la upatikanaji wa maji ya kunywa, asilimia themanini na tano (85%) hawana uwezekano wa kufikia kipengele cha usafi wa mazingira. Makadirio ya ripoti ya Benki ya Dunia inaonyesha kwamba asilimia (20 – 40%) ya fedha za sekta ya maji zinapotea kupitia mazoea ya udanganyifu.

Tetemeko la Ardhi la Ukubwa wa 6.2 Latokea Nchini Nicaragua

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ukubwa wa 6.1 lilitokea Nicaragua mnamo Alhamisi Aprili 10, 2014. Kulikuwa na taarifa [es] za watu kujeruhiwa na kuanguka kwa nyumba shauri ya mtikisiko mkubwa.

Kitovu kilikuwa kilomita 20 Kaskazini ya mji mkuu Managua, karibu na volkano ya Apoyeque, wa kina cha kilomita 10. Katika mtandao wa Twita, watumiaji waliripoti tetemeko dogo na kusimamishwa kwa shughuli za shule:

Tetemeko la tano baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 nchini Nicaragua: MANAGUA, Nicaragua.- Angalau…

Shughuli za shule kusimamishwa katika Managua na León kutokana na tetemeko la ardhi..

Robert Antoni Ashinda Tuzo ya Boca 2014 ya Fasihi ya ‘Caribbean’

Mwanablogu wa Jamaika aishiye ughaibuni Geoffrey Philp anataarifu kuwa Robert Antoni, mwandishi wa kitabu cha “As Flies to Whatless Boys”, ameshinda Tuzo ya One Caribbean Media Bocas 2014 kwa Fasihi ya Nchi za ‘Caribbean’ wakati blogu ya ‘Repeating Islands’ ikichapisha pitio la kitabu riwaya yake hapa.

Namna ya Kutafuta Chumba cha Kupanga Nchini China

Chengdu Living anawafundisha wasomaji wake namna ya kutafuta chumba cha kupanga nchini China bila kwenda kwa dalali kwa kutoa mwongozo wa hatua tano.

Bob Marley – Ni Mungu Mpya wa Vijana wa Bhutan?

Bob Marley ghafla amegeuka mungu miongoni mwa kizazi kilichochanganyikiwa. bendera ya Rastafari, ikiwa na ama Bob mwenyewe au jani la bangi, inapatikana kokote. Kwa mtu aliyekufa mwaka 1981 na kuendelea kutawala akili za watoto wanaonekana kuwa na akili tena wa karne ya 21 ni jambo gumu kuamini.

Passang Tshering, Mwanablogu wa Bhutan na mwalimu wa kompyuta kwenye Shule ya Sekondari Bajothang, Bhutan, anashangazwa kwa nini Bob Marley anachukuliwa kuwa alama ya vijana wa Kibhutan leo. Badala yake, angependa kuwaona wakitafuta watu 12 ambao picha zao amezitundika kwenye ukuta wa maabara yake ya kompyuta ya shule hiyo

na anashangaa wamewezaje kufanya walichokifanya. Shangaa, Kubali, na Hamasishwa

Magonjwa ya Afya ya Akili Hayapewi Kipaumbele Nchini Cambodia

Akiandika kwa niaba ya Southeast Asia Globe, Denise Hruby aliripoti jinsi wagonjwa wa akili katika maeneo mengi ya vijijini vya Cambodia wanavyofanyiwa:

…Wagonjwa wa akili bado hutibiwa na waganga wa jadi, ambao lengo lao ni kuwatoa pepo wabaya kwa kuchoma ngozi, au kwa wafanyakazi wasio na ujuzi wa chumba kimoja cha kliniki za afya ambao huwapa kila kitu kutoka vidonge vya dawa ya kupunguza maumivu hadi dawa ya kikohozi.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Phay Siphan, afya ya akili si kipaumbele:

Serikali imeipa kipaumbele afya ya uzazi na ugonjwa wa malaria. Kwa afya ya akili, najua kwamba serikali inazo fedha za kugharamia, lakini sisi tu maskini.

Msiyalaumu Mataifa ya Magharibi kwa Matatizo ya Afrika

Gershom Ndhlovu anasema kuwa viongozi wa Afrika wanafanya kosa kuzilaumu nchi za Magharibi kwa matatizo ya Afrika:

Kwenye mkutano wa hivi karibuni wa Umoja wa Ulaya ulifanyika nchini Ubeligiji, rais wa Zambia Michael Chilufya Sata alijibu mapigo kwa kile kile ambacho viongozi wengine wa Afrika walikisema huko nyuma kuhusu Nchi za Magharibi kuchangia vita barani humu kupitia biashara ya sialaha na vifaa vingine vya kivita. Akinukuliwa na Eil D’Afrique, Sata aliuambia mkutano huo kuwa Afrika haikuwa na kiwanda cha silaha zinazochochea migogoro na kwamba Ulaya inahusika moja kwa moja na migogoro inayotokea barani humu kwa sababu silaha zinazotumika kwenye migogoro zimezalishwa kwenye viwanda vilivyoko kwenye nchi za Magharibi. “Askari wengi watoto na masikini wanaohusika na migogoro hii barani Afrika wanabeba silaha zilizozalishwa Ulaya zenye kugarimu maelfu ya dola. Watoto hawa masikini hawawezi kuwa na fedha za kununulia silaha hizi,” alisema Sata.
Katika kipindi cha baada ya uhuru, Afrika imekuwa na mchango wake wa kutosha kwenye mapinduzi na visasi vya kupindua waliopindua pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ni kweli, kuwa mapinduzi mengi yalipangwa kwenye vyumba vya faragha ambapo wanadiplomasia wa nchi za Magharibi walikutana na maafisa wa kijeshi huku wakigida mvinyo na pombe ghali, wakiwafanya si tu wawe na tamaa ya kudhibiti raslimali za taifa kama watang’oa viongozi wenye misimamo mikali dhidi ya nchi za Magharibi lakini pia kuwafadhili mtaji. Hivi ndivyo madikteta kama Mobutu Sese Seko walivyoweza kupanda na kung’ang’ania madarakani.
Lakini kuzilaumu nchi za Magharibi na viwanda vya silaha barani Ulaya kwa migogoro yote au mingi ya migogoro hiyo ya hivi karibuni ni kutokuwa wakweli na kwa hakika ni sawa na kuficha vichwa mchangani, kama afanyavyo mbuni. Ni aibu kuwa leo bado nchi za Afrika zinawalaumu mabwana zao wakoloni wa zamani kwa uchumi uliozorota ambao kwa hakika kabisa kunasababishwa na ufisadi, udhibiti mbovu wa raslimali na kukosa uwezo.

Wito wa Kuacha Ujenzi Nchini Taiwan Ili Kuwalinda Chui

A small leopard cat. Photo is taken by the Wildlife First Aid Station and reprinted by leopardcatgo. CC BY-NC 2.0

Chui mdogo. Picha kwa hisani ya stesheni ya huduma ya kwanza ya Wanyamapori imechapishwa na leopardcatgo.

Chui wameorodheshwa kama wanyama wanaoishi kwenye mazingira magumu [zh] nchini Taiwan. Kwa kuwa chui wakubwa huishi misituni na mwituni katika maeneo tambarare na yale yenye milima na makazi yao ni aina tofauti sana. Makazi yao nchini Taiwan yanasumbuliwa kwa sababu ya miradi mipya ya ujenzi. Kamati ya tathmini ya mazingira ya Taiwan ilikuwa imekataa kwa muda ombi kutoka Serikali ya Miaoli kuendeleza barabara mbadala katika Miaoli inayopita katikati ya makazi ya chui mnamo Aprili 16 2014 baada ya kusambaa maandamano na malalamiko ya kusitishwa mradi huo. Hata hivyo, mradi huu wa maendeleo haukusimamishwa, na miradi ya maendeleo zaidi katika eneo hili inaendelea kubuniwa. Ukurasa wa facebook [zh] ulianzishwa ili watu ambao wanaotaka kuwalinda chui nchini Taiwan waweza kupata taarifa vizuri na kuhamasishwa.

Mashirika ya Kimataifa, Wanaharakati na Waandishi dhidi ya #LeyTelecom

Mashirika kadhaa ya kimataifa ya haki za digitali zilitumia kongamano la Mexico barua kuonyesha msaada wa kimataifa [es] kwa ajili ya kutetea uhuru wa kujieleza na uhuru kwenye mtandao nchini Mexico. Barua imetiwa sahihi na Electronic Frontier Foundation, Vía Libre, Digital Rights NGO, miongoni mwa wasomi wengine na wataalam.

Kwa mujibu wa waliotia sahihi, kila kanuni inakusudia kulazimisha kanuni za mawasiliano ya simu na utangazaji zilizopitishwa na kongamano la Mexico kuzingatia kanuni za kikatiba na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu iliyotiwa saini na Mexico. Pia walitoa wito kwa maadhimisho ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya faragha katika zama za digitali juu ya sheria ya lazima ya mawasiliano ya simu, tamko la pamoja juu ya mipango ya ufuatiliaji na athari zake katika uhuru wa kujieleza kanuni 13 [es] kuhusu haki za binadamu , ili kuhakikisha heshima ya haki za binadamu katika mtandao inakuwepo.

Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska

Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza[fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao wa Twita:

Namuwasilisha Roger Kolo (@kolo_roger) kama waziri mkuu mpya. Shukrani nyingi kwa Malagasies wote #Madagascar

Mgogoro Usiopewa Uzito Stahiki Nchini Burundi

Wakati nchi jirani ya Rwanda inagonga vichwa vya habari na maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 na kuongezeka kwa mvutano na Ufaransa, Burundi imeharibiwa katika kupuuzwa kwa mgogoro wa kisiasa na dalili za vurugu zinazoweza kusababisha mapigano mapya ya Wahutu na Watutsi. Tshitenge Lubabu nchini Burundi anatoa maoni kwamba mzizi hasa wa mgogoro ni viongozi wa sasa wa kisiasa:

 La plupart de nos dirigeants, bien ou mal élus, malgré de longues années de pouvoir, se sont illustrés par leur impéritie [..] Tous les mensonges sont bons pour confisquer le pouvoir. Quand leurs mandats, limités par la Constitution, arrivent à terme, des courtisans zélés, jamais repus, les supplient de ne pas partir. Comme si, sans eux, le soleil risquait de ne plus apparaître 

Wengi wa viongozi wetu, waliochaguliwa vyema au sivyo, licha ya kukaa muda mrefu madarakani, ni wazembe [..] uongo wowote ni mzuri kumfanya akwae madaraka. Wakati majukumu yao yanafikia mwisho kama ilivyoainishwa katika Katiba, wasaidizi wao wenye bidii, wasioridhika kamwe, huwaomba wasiachie madaraka. Ni kama wanafikiri bila wao, jua halitawaka kesho.

Niger Yapata Kituo Chake cha Kwanza cha Reli Baada ya Kusubiri kwa Miaka 80

Aprili 7, Niger ilizindua katika mji mkuu wa Niamey kituo chake cha kwanza cha treni kuwahi  [fr]. Mamlaka tayari ilikuwa na makadirio ya ujenzi wa kituo cha treni miaka 80 iliyopita lakini mradi kamwe haukuanzishwa. Tukio hilo litaanzisha ujenzi wa reli kati ya Niger, Benin, Burkina Faso na Côte d'Ivoire. Mtumiaji Twita Tanoussou katika Niamey aliweka picha kwenye mtandao ya kituo hicho cha reli:

 

Photos postsVideo posts