Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Juni, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Juni, 2014

Puerto Deseado, Ahera ya Pwani

DDSC_3624

Picha imepigwa na Laura Schneider, imetumiwa kwa ruhusa.

Kwenye blogu yake Viajes y Relatos, Laura Schneider anasimulia uzoefu wake alipotembelea Puerto Deseado, mji ulioko kwenye Jimbo la Santa Cruz, Ajentina. Katika siku yake ya sita ya safari yake ya kupiga picha, alitembelea na kupiga picha za mji huo mzuri katika maeneo ya karibu:

Yendo por la ruta 3, luego de pasar Comodoro Rivadavia y Caleta Olivia a 300 km, nace una ruta que desvía a Puerto Deseado. Ciudad costera y portuaria de la patagonia con acantilados, una gran biodiversidad de aves y mamíferos y varios circuitos costeros que nos lleva a la famosa Ria.

Pingüinos magallánicos, pingüinos de penacho amarillo, lobos marinos, delfín austral, cormoranes, toninas, ostreros y gaviotines es la gran variedad que se puede avistar. Pero mas allá de la fauna, Puerto Deseado es una ciudad rica en historia dado por su tren.

Nikiwa usawa wa kilometa 3, 300 baada ya Comodoro Rivadavia na Caleta Olivia, kuna njia panda inayokupeleka Puerto Deseado. Huu ni mji wa pwani na bandari jimboni Patagonia wenye miamba, ndege wakubwa na utajiri wa viumbe na mfululizo wa safari za pwani unaokufikisha kwenye eneo linalofahamika vizuri zaidi la Ria.

Ndege wa Magellanic, rockhopper, simba wa baharini waitwao Patagoni, nyangumi wa Peale, waishio kwenye mto, na aina mbalimbali za wanyama ni sehemu ya utajiri wa wanyama unaopatikana kwenye eneo hili. Lakini zaidi ya hayo, Puerto Deseado ni historia ya jiji tajiri shauri ya miundo mbinu ya gari moshi.

Unaweza kumfuatilia Laura kwenye mtandao wa Twita.

Posti hii ni sehemu ya saba ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV)tarehe 16 Juni, 2014.

Umuhimu wa Haki kwa Wanablogu wa Ethiopia

Justice Matters ni blogu inayoripoti kuhusu kesi ya wanablogu wa Zone9 waliokamatwa na waandishi wa habari nchini Ethiopia kwa ajili ya kutoa maoni yao:

Blogu hii ina habari zaidi za hivi karibuni kuhusu jitihada za utetezi, ripoti za vyombo vya habari, na hadhi ya kisheria ya wanablogu wa Zone9 nchini Ethiopia. Imejitolea kutoa taarifa juu ya kesi ya wanablogu na waandishi wa habari wasio na hatia. Tunaamini katika nguvu sahihi na taarifa sahihi ya hali ya wanablogu kutoka eneo kamili.

Hadithi ya Wakimbizi wa Njaa kutoka Niger katika Algeria Mashariki

Katika wiki chache zilizopita, mamia ya wahamiaji mwa Jangwa la Sahara kutoka Mali au Niger wamehamia miji ya Algeria katika mpaka wa Mashariki. Liberté Algérie anasimulia hadithi ya wale ambao waliamua kuhama na kwa nini [fr]

Les conditions de vie au hangar de la cité Bourroh sont inhumaines. A l’intérieur du hangar, les Subsahariens ont dressé des tentes, une soixantaine environ. A l’intérieur de chaque tente, trop exiguë, vivent, serrés les uns contre les autres, tous les membres d’une même famille. [..] Meriem et Aïcha sont deux sœurs âgées respectivement de 10 et 12 ans. Avec leur mère, elles ont fui leur pays d’origine, le Niger, à cause de la pauvreté. “Nous avons quitté notre pays, parce que nous n’avions plus quoi manger. Meriem et Aïcha sont deux sœurs âgées respectivement de 10 et 12 ans. Egalement originaires du Niger, Sakina, sa fille Asma et ses deux petits-enfants s’étaient réfugiés à Aïn Guezzam, dans la wilaya de Tamanrasset, à l’extrême sud du Sahara. Dans un arabe approximatif, notre interlocutrice nous apprendra qu’ils font partie d’un groupe qui a fui la faim au Niger.

Hali ya maisha katika majengo ya mji wa Bourroh si ya kibinadamu. Ndani ya jengo, wahamiaji wa Jangwa la Sahara wameweka mahema karibu sitini. Ndani ya kila hema (ndogo sana), wao wote wanaishi pamoja, dhidi ya kila mmoja, washiriki wote wa familia moja. [..] Meriem na Aisha ni dada wawili wenye umri wa miaka 10 na 12. Na mama yao, walikimbia nchi yao ya asili, Niger, kwa sababu ya umaskini.. “Tulihama nchi yetu kwa sababu hatukuwa na chakula cha kutosha ‘Meriem anasema. Pia kutoka Niger, Sakina, binti yake Asma na wajukuu wake wawili ni wakimbizi katika Ain Guezzam katika Wilaya ya Tamanrasset, kusini mwa jangwa la Sahara. Akisita kwa lugha ya Kiarabu, Sakira alituambia kwamba wao ni sehemu ya kundi ambao walikimbia njaa kubwa nchini Niger.

Sababu za Kuishangilia Kodivaa kwenye Kombe la Dunia

CostadeMarfil

Timu ya Taifa ya Kodivaa wakati wa Mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA, mwaka 2010, nchini Afrika Kusini. Picha ni ya mtumiaji wa mtandao wa Flickr, Merah Chhaya. CC BY 2.0.

Kwenye tovuti ya LaMula.pe, Juan Carlos Urtecho anaeleza sababu zake za kuishangilia Kodivaa kwenye mpambano wa Kombe la Dunia kati ya nchi hiyo na Kolombia siku ya Alhamisi, Juni 19:

Desde que les ganaron a Japón en su debut, los marfileños se han vuelto mis preferidos en este mundial. […] Uno escoge a sus engreídos de la manera más simple. Costa de Marfil, ubicado en la costa occidental de África, con un PBI de 19 mil millones de euros y un per cápita de 967 euros es el tercer país más pobre de los que están en el mundial después de Honduras y Bosnia. La economía de Japón (PBI de 5 billones de euros y 30 mil per cápita) es la segunda detrás de Estados Unidos. Costa de Marfil es un país que intenta recuperarse de una sangrienta guerra civil que dejó a decenas de miles de muertos y cientos de miles de desplazados entre el 2002 y el 2007. Japón, es… bueno, Japón.

Tangu wakati waliposhinda Japan katika mechi yao ya awali, hawa jamaa [Wakodivaa] wamekuwa timu yangu pendwa kwenye mashindano haya ya Kombe la Dunia […] Unachagua mayai viza kwa njia rahisi. Kodivaa, nchi iliyoko Afrika Magharibi yenye Pato la Nchi la Euro milioni 19 na wastani wa Euro 967 kwa kila Mkodivaa, ni nchi maskini zaidi kati ya nchi zinazoshiriki kwenye mashindano hayo, baada ya Honduras na Bosnia. Uchumi wa Japani (Pato la Taifa la Euro bilioni 5 na wastani wa Euro milioni 30 kwa kila Mjapani) ni wa pili baada ya Marekani. Kodivaa ni nchi inayojikakamua kupata nafuu baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua makumi ya maelfu ya watu na kuwahamisha malaki ya watu kutoka kwenye makazi yao kati ya mwaka 2002 na mwaka 2007. Japan, ni…aha, ni Japan.

Salamu, Brazil: Mashabiki wa Kiislam wa Kandanda na Kombe la Dunia la FIFA

futbol muslim

Picha imepigwa na Willard kwenye mtandao wa flickr. CC BY-NC-ND 2.0.

Raia wa Colombia aliye na makazi yake katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Marcelino Torrecilla anatuhabarisha [es] kuhusiana na upekee wa mashabiki wa kiislamu wa mpira wa miguu kwenye Kombe la Dunia la FIFA, 2014 :

Katika Kombe la dunia, waislamu 50,000 wamesili kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile Irani, Naijeria, Aljeria, Marekani, Uingereza, Malaysia na wengine wengi wanaotarajiwa kutoka katika Ghuba hii. kwa hakika, wataweza kuijaza takribani misikiti 80 iliyo katika maeneo mbalimbali ya nchi hii kubwa kabisa;

Aliendelea kusema kuwa:

Nchi sita kati ya 32 zinazoshiriki shindano hili, hiki ni kiwango kikubwa cha ushiriki wa waislam. Miongoni mwa nchi hizi, tunazo, Bosnia-Herzegovina, Kameruni, Irani, Code Ivar na Naijeria.

Unaweza kumfuatilia Marcelino kwenye mtandao wa Twita.

Posti hii ni sehemu ya sita ya mpango wa #LunesDeBlogsGV [Jumatatu ya blogu kwenye GV] siku ya Juni 9, 2014.

Simulizi la Kusikitisha la Ibrahim na Djouma wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ibrahim and Amadou - screen capture of UNHCR video on YouTube

Ibrahim na Amadou – picha iliyopigwa kwenye video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia wakimbizi (UNHCR) kwneye mtandao wa YouTube

Djouma na Amadou Moussa ni wazazi wa Ibrahim. Djouma na Ibahim ni wahanga wa shambulizi la kikatili lililofanywa na  wanamgambo waaasi, tukio lililokatisha maisha ya ndugu watano wa damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Kameruni. Wanamgambo hao walikuja wakati  Amadou Moussa akiwa mbali na nyumbani kwake. Djouma, 30, anakumbuka tukio hilo baya

Walinikuta nikiwa na wanangu nyumbani kwangu; waliwakusanya watoto wote wadogo na kuwachinja kwa panga. Waliua watu sita, ikiwa ni pamoja na watoto mbele yangu [..] Ibrahim alikuwa kati ya watoto sita waliowachukua. Walimkata na panga, wakadhani amefariki.

Kama inavyoonekana kwenye video hii, Ibrahim ana kovu kubwa kichwani kwake lililosababishwa na panga. Hata hivyo Ibrahim alipona, pamoja na tukio hilo baya. Hadithi ya Ibrahim ni mfano wa madhila ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wakimbizi 20,000 wamevuka mpaka tangu kuanza kwa vita. Ombi maalum limetumwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kumkumbusha kuchukua “hatua stahiki za kuhakikisha  kwamba mikakati ya kurejesha amani inatengewa fedha kwa mwaka wa 2015.”

  

 

Umuhimu wa Hisabati katika Elimu

Carlos Thompson wa blogu ya Chlewey anaandika [es] juu ya umuhimu wa kufundisha Hesabu nchini Colombia kutokana na nchi hiyo kufanya vibaya kwenye vipimo ya kimataifa vya ubora wa elimu [es]:

Las matemáticas dan mucho más que la capacidad de contar las vueltas en una tienda; o las destrezas específicas para entrar a una facultad de ingeniería. Las matemáticas generan una estructura mental que benefician también al médico, al comunicador social o al sociólogo, no específicamente para tener éxito en su profesión sino cómo ciudadano en una democracia y como una persona que influye en una sociedad.

Hesabu huwezesha zaidi ya uwezo wa kutoa ‘chenji’ dukani, au uwezo maalum wa kuweza kuajiriwa katika Shule ya Uhandisi. Hesabu huzalisha muundo wa akili ambao pia humfaidisha daktari, mwasilianaji wa kijamii au mwanasosholojia, si kumfanya awe na mafanikio katika taaluma yake, lakini kuwa raia katika demokrasia na kama watu binafsi wenye ushawishi katika jamii.

Posti hii ilikuwa ni sehemu ya nne ya #LunesDeBlogsGV [Blogu za Jumatatu katika GV] mnamo Mei 26, 2014.

Taarifa ya Maendeleo ya Kiteknolojia Barani Afrika

Erik anatushirikisha taarifa 5 kuhusu mwenendo wa teknolojia barani Afrika:

Nimeendelea kutamani kuandika makala za blogu kuhusu taarifa hizi moja baada ya nyingine, nyingi zikihusu Afrika, lakini inaonekana sitaweza. Badala yake, nitaweka kiungo cha kila moja wapo, inayoonekana, na maneno machache ya kwa nini ni muhimu kuzisoma.
1. Taarifa ya Akamai kuhusu “Hali ya Mtandnao wa Intaneti” ya mwaka 2013.

[Pakua [download] Taarifa ya Akamai, PDF]

Ina taarifa nzuri kuhusiana matumizi ya intaneti duniani, pamoja na mwenendo wake. Katika bara la Afrika, hata kama kuna maendeleo zaidi nchini Kenya, wote tunaona maendeleo pia yanayoonekana katika nchi za Afrika Kusini, Misri na Moroko. Hata hivyo, kuna mchoro wa Ericsson kuhusu matumizi ya mtandao wa si-waya.

Ucheshi na Harakati Kutoka Mexico

comedia

Picha na laranggio kwenye mtandao wa flickr. CC BY-NC-SA 2.0.

JM Casanueva, mwandishi wa blogu ya SocialTIC, anapitia mwelekeo mpya wa harakati nchini Mexico kwenye blogu na kwenye mitandao ya kijamii ambayo inatumia utani kuwafikia watu wengi zaidi:

El humor siempre ha sido una táctica exitosa para transmitir causas de manera empática (sí, que alguien que no seas tú o tus colegas activistas entiendan la problemática) y llegar a públicos más amplios (sí, más allá de lxs [sic] grupos de sospechosos comunes que siempre te retuitean). El activismo mexicano de 2014 ha tenido una muy buena dosis de humor por parte de comediantes que han aprovechado sus talentos, agudeza y compromiso social para buscar impactar en la sociedad.

Utani mara zote umekuwa ni mbinu inayofanikiwa sana kufikisha ujumbe (ndio, kwamba mtu fulani ambaye sio wewe au mwanaharakati mwenzako anaelewa tatizo) na kuifikia hadhira kubwa zaidi (ndiyo, zaidi ya makundi ya mtandaoni ya watu wanaokuhisi na kusambaza ujumbe wako). Wanaharakati wa Kimexico mwaka 2014 wamekuwa na dozi ya kutosha ya ucheshi kutoka wachekeshaji wanaotumia vipaji vyao, umakini na kujichanganya kwao na jamii kuleta manufaa kwa jamii.

Unaweza kufuatilia SocialTIC kwenye Twitter.

Posti hii ni sehemu ya saba ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV) tarehe 16 Juni, 2014.

Mapigano Dhidi ya Waislamu Yaendelea Nchini Sri Lanka

Yametimu majuma mawili tangu ghasia dhidi ya Waislamu kwenye majiji ya pwani nchini Sri Lank- Aluthgama na Beruwala. Ingawa hali imetulia baada ya kulaaniwa sana kila sehemu, bado ghasia hizo dhidi ya Waislamu zinaendelea katika maeneo tofauti ya Sri Lanka.

Mwanablogu Abdul Khaleq anatwiti kuhusu tukio moja huko Ratmalana sehemu ya wilaya ya Colombo:

Msikiti ulioko barabara ya Ratmalana Borupona umechomwa moto saa 7 usiku. Moto ulioanza mapema ulizimwa.

Mwanablogu D. B. S. Jeyaraj ana habari zaidi kuhusu jaribio lililoshindwa la kushambulia msikiti wa Thalayan Bawa Jumma uliopo kwenye barabara ya Borupane mjini Ratmalana masaa ya asubuhi Jumapili iliyopita, tarehe 29 Juni, 2014.

Uhamaji wa Watoto Wachukuliwa kuwa ni Baa la Kibinadamu

Kutoka Mexico, Katia D'Artigues, ambaye ni mwandishi wa blogu ya Campos Elíseos (Champs Elysées), aandika kuhusiana na watoto kulazimika kuhama wao wenyewe [es], hali inayompelekea kuiita hali hii kuwa ni “baa la kibinadamu”:

Son niños que son orillados a cruzar la frontera solos. No lo hacen por aventura, sino porque muchas veces no les queda de otra, por pobreza; porque buscan reunirse con un familiar quizá su padre o su madre que ya está en Estados Unidos. Su número crece día con día. Ya se cuentan en miles y al menos un centenar son detenidos todos los días de acuerdo a cifras no oficiales.

Ni watoto wanaolazimika kusafiri hadi nchi nyingine peke yao. Hawafanyi hivyo kwa sababu za kitalii, sababu kubwa ni kuwa hawana namna nyingine, ni umasikini, ni kwa sababu wanajaribu kuwatafuta ndugu zao ili waungane nao tena, yawezekana ni baba au mama zao ambao tayari wameshafika Marekani. Idadi ya wahamiaji watoto inaongezeka siku hadi siku. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, maelfu ya watoto husafiri na idadi isiyopungua mia moja hukamatwa kila siku.

Anaongeza kuwa:

Cómo están estos niños? Independiente de su estatus y nacionalidad son niños y tienen derechos. […] Lo cierto es que ya se estipuló que se les asignará un abogado gratis para ver su proceso que, como es obvio, es único en cada caso. Ahora, son solo 100 abogados que comenzarán a trabajar en diciembre de este año o enero de 2015.
No van a alcanzar.

Vipi kuhusu hao watoto? bila kujali hali yao na uraia wao, bado ni watoto na wana haki. […] Imekwisha fahamika kuwa, watoto hawa, kila mmoja atapewa mwanasheria wake. Hadi sasa wameshapatikana wanasheria 100 tu ambao wataanza kazi mwezi Disemba mwaka huu au mwezi Januari, 2015.
Hawatatosha.

Jinsi Mabadiliko ya Hali ya Hewa Yanavyowaathiri Wakaazi wa Vijiji Nchini Benin

Mbenin, Alain TOSSOUNON, alipachika muhtasari wa ripoti kwenye blogu ya Mtandao wa Afrika Magharibi wa Waandishi wa Habari Unaohusu Maji na Usafi wa Mazingira (WASH). Ripoti yenyewe ilishughulikia tathmini ya mahitaji ya baada ya maafa nchini Benin kufuatia mafuriko makubwa ya hivi karibuni. Maafa hayo yalisababisha vifo vya karibu watu hamsini na uharibifu uliokadiriwa kuwa FCFA bilioni 7.83 (karibu dola milioni 160) [fr]:

Siku hizi, wakati wowote ambapo mvua huanza kunyesha, ninaanza kuhisi hofu na wasiwasi,” Elizabeth Kpossou, mkaazi wa kijiji, anasema. Naye rafikiye na jiraniye, Alice Codjo, anahisi hivi. Hata hivyo, miaka michache iliyopita, mafuriko ya mara kwa mara yalikuwa matukio ya kawaida kwenye jamii hizo zenye amani. Na mbali na kuwa mapigo, mafuriko hayo yalipoisha, yaliacha udongo wenye rutuba. Nao wakaazi wa vijiji walichukua fursa kuutumia udongo huo. Sasa, siku hizo zimepita. “Kila kitu kikabadilika,” mkuu wa kijiji, Samuel Boton, anasema. “Sasa, mafuriko yanasababisha uharibifu mkubwa zaidi” [..] Kweli, kama ilivyo kwenye kijiji hiki cha Adjohoun chenye wakaazi 56,455, nchi nzima imekumbwa sana na maafa. Kote nchini, idadi ya vifo na kiasi cha uharibifu kilikuwa kikubwa mno. Kulikuwa na vifo 46 na zaidi ya nusu ya manispaa ziliathirika (manispaa 55 ziliathirika kati ya 77 zilizoko nchini Benin).

Maandamano Makubwa Yafanyika huko Guangzhou, China

Mamia ya wakazi wa Guangzhou jana mchana walikusanyika huko Sanyuanli kupinga hatua ya polisi ya kutaifisha mali binafsi za watu kwenye bohari kama sehemu ya harakati za kukabiliana na majanga ya moto. Waandamanaji walijikuta wakikabiliana vikali na polisi, na baadae, wakati wa vurugu hizo, waandamanaji walifikia hatua ya kupindua magari ya polisi. Charles Liu kutoka nanfang.com anayo habari kamili.

Tovuti 50 Zilizotembelewa Zaidi Nchini Kenya

Je, unajua ni tovuti gani maarufu zinazotembelewa zaidi nchini Kenya? Soka posti ya James Wamathai kwenye blogu yake kufahamu zaidi:

Mengi yamebadilika tangu mwezi Januari, wakati nilipotoa orodha ya tovuti maarufu zaidi nchini Kenya. Tovti ya Budget airline Jambo Jet ilizinduliwa, gazeti linalomilikiwa na kampuni ya NMG liitwalo Nairobi News lilizinduliwa na kufanikiwa, tovuti ya burudani ya izvipi nayo ilianzishwa na Sauti Sol ilitoa video ya wimbo wao mpya iliyoibua mjadala mkali, lakini ilijipatia umaarufu, ‘Nishike”.

Kwenye orodha ya tovuti maarufu, kuna mabadiliko kadhaa kama unavyoona hapa.

Kenyan Post imeipiku Ghafla kama blogu maarufu zaidi nchini Kenya
Jumia, KRA, Career Point Kenya, Helb na Techweez zimepanda chati.
Niaje, The Star, Orange na Michezo Afrika zimeshuka umaarufu.
Ben Kiruthi, KU, Kenya Today na Kopo Kopo zimeingia kwenye orodha ya 50 bora.

Twiti za Moja kwa Moja za Kesi Dhidi ya Mwanasheria wa Haki za Binadamu na Mwandishi wa Habari Nchini Swaziland

MISA-Swaziland anatwiti moja kwa moja mwenendo wa mashitaka dhidi ya mwanasheria wa haki za binadamuThulani Maseko na mwandishi wa habari Bheki Makhubu bila ruhusa ya mahakama nchini Swaziland. Wawili hao walikamatwa mnamo Machi 17, 2014.

Maneno Yasiyotafsirika Yafafanuliwa kwa Michoro

Tovuti ya Pijamasurf [es] inazungumzia “orodha ya maneno 30 yasiyotafsirika” ambayo msanii mchunguzi Anjana Iyer [en] alijaribu kuyachorea mchoro wenye kuchekesha kidogo. Kwa mfano:

Bakku- shan (Kijapani)
Msichana mzuri…almuradi tu anaangaliwa kutokea nyuma.

Unaweza kuipata orodha hiyo hapa.