Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Oktoba, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Oktoba, 2014

Ungana nasi kwa Mkutano wa Global Voices Tunis Novemba 1

gvMeetupTunis
Tunayofuraha kutangaza kwamba mkutano wa Global Voices umepangwa kufanyika nchini Tunis mnamo Novemba 1, 2014 kuanzia saa 3asubuhi hadi saa 7 mchana, kwenye Maabara ya wazi ya uvumbuzi 404 inayomilikiwa na Wakala wa Mtandao wa Intaneti Tunisia (ATI).

Mikutano ya Global Voices ni mikusanyiko midogo ya mahali inayokusudiwa kusaidia kutengeneza mitandao na wasomaji wetu, waandishi au wafasiri watarajiwa, na wengine wanaonesha kuvutiwa na kazi zetu.

Wakati huo huo, mikutano ya namna hii itakuwa ikifanyika kwenye miji ya Accra, Beirut, Dar Es Salaam, na Belgrade. [Mkutano wa Dar es Salaam unafanyika Novemba 2, 2014].

Mkutano huu wa Tunis ni fursa yetu kueleza shughuli na miradi yetu ya Global Voices kwa wasomaji wetu nchini Tunisia. Katika agenda za mkutano, kadhalika, kutakuwa na mada kuhusu vyombo mbadala vya habari na ulinzi wa data binafsi itakayotolewa na Chawki Gaddas kutoka Kitivo cha Sheria, Sayansi ya Siasa na Jamii cha Tunis.

Unaweza kuona agenda kamili za mkutano huo hapa.

Kama unapenda kushiriki, tafadhali jaza fomu ya kujiandikisha. Tukio hili ni wazi kwa wote lakini nafasi ni chache.

Hapa unaweza kuona ramani ya namna ya kufika eneo la tukio.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: abrouafef [at] riseup [dot] net