Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Disemba, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Disemba, 2013

China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”

Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.

Changamoto za Huduma ya Afya kwa Familia Katika Apatou, French Guiana

Henri Dumoulin with a child at the PMI center of Apatou, French Guiana (with his permission)

Henri Dumoulin, mchangiaji wa Global Voices, anakumbuka kukaa kwake huko Apatou, French Guiana,sehemu iliyoko katika msitu wa Amazon. Anaelezea jinsi gani, kama daktari wa mpango wa ulinzi wa Afya ya Mama na Mtoto huko, alivyokuwa akitegemea ushirikiano rasmi na mfumo wa afya wa Suriname na kutizamwa mazingira ya lugha mbalimbali ya jamii :

Nitakuwa eneo la “Apoema tapu gezondheid Zentrum” mnamo Novemba 28, 29 kufanya kazi tena na timu hiyo, kuwapa chanjo watu wote wanaoishi katika pande zote za mipaka katika kisiwa cha franco-Surinamese. Inaonekana kwamba hakuna mtu alikuwa na ufahamu wa kuja kwetu [..] Basi akaunti ya sindano ikawa ndogo kuliko ilivyotarajiwa (109 katika siku moja). Amalia [mratibu] alituma wito kwenye radio Alhamisi asubuhi na watu wakaja kuendelea [..] na wasiwasi kidogo kuhusu majibu ya bosi wangu kuhusu njia yangu ya kusimamia matatizo ya afya mitaa yetu na kuvuka mipaka ..

Cuba: Madiba Alifanya Mengi Mazuri Pamoja na Mapungufu Aliyokuwa Nayo.

Blogu ya Cuba Without Evasion yatanabaisha kuwa, namna pekee ya kumuenzi Nelson Mandela ni kwa “kuiga mfano wake wa kusamehe na Usuluhishi”:

Ninakusamee…kwa urafiki uliokuwepo kati yako na…dikteta aliyekuwa muovu kiasi ambacho watu wangu hawakuwahi kuushuhudia…kwa kuweka mkono wako– kwa ajili ya kuwaokoa watu wako- kwenye mabega yavujayo damu ya yule aliyenitenga na kunilaani mimi.

Kimbunga Haiyan: Hadithi ya Ujasiri Kupitia Filamu Fupi

Kimbunga Haiyan, filamu fupi kwa hisani ya Janssen Powers, inaonyesha hali baada ya dhoruba ambayo mapema mwezi Novemba iliua zaidi ya watu 6,000 katika jimbo la Philippine la Leyte.

“Kwa kawaida, mimi nia yangu ilikuwa kupata habari za uharibifu huo, “Powers aliandika katika maelezo ya kazi yake. “Nilicho pata hata hivyo, ilikuwa habari ya ujasiri.”

Katika maandishi, picha za maafa ni mbadala na mahojiano na waathirika, ambao wanajadiliana juu ya janga na kutazamia siku zijazo.

Kwa hadithi zaidi juu ya Kimbunga Haiyan angalia hapa.

Brazil: Je Unamuenzi Mandela? Basi Saidia Haki za Binadamu

Bango la kuonyesha heshima kwa Nelson Mandela limechukua umaarufu usiojulikana wa kiongozi wa Afrika Kusini nchini Brazil kwa kuwaita wale ambao wanaenzi urithi wake kusaidia haki za binadamu. Ujumbe huo ulienezwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Conectas Human Rights katika Siku ya Haki za Binadamu, Desemba 10, 2013.

Banner publicized by Conectas Human Rights on Facebook

Bango lililotangazwa na Conectas Human Rights kwa mtandao wa Facebook
Tafsiri: “Je, wewe pia kujihisi uliongozwa na urithi wake? Maelfu ya watu duniani kote wanakabiliwa na ukiukwaji wa haki za binadamu kila siku. Wanakuhitaji kufanya zaidi ya kutazama tuu. Fuata mfano wake. Kubaliana na sababu. Kusaidia haki za binadamu. Hapa. Sasa. “Desemba 10, Siku ya Haki za Binadamu. Nelson Mandela (1918-2013)

“Tenda zaidi ya kuongozwa” ni mwito wa shirika katika nchi ambapo kihafidhina na maono hasi kuhusu haki za binadamu inaonekana kuongezeka. Kama baadhi kura za maoni ya hivi karibuni zinaonyesha, 90% ya Wa-Brazil wanaunga kupunguza umri wa miaka kwa jukumu la jinai, na 61% wanaamini kwamba uhalifu unasababishwa na tabia mbaya za watu.

Kudumisha Maadili Muhimu ya Vijana wa Bhutanese

Bhutanese youth playing. Image by Morgan Ommer. Copyright Demotix (15/2/2009)

Vijana wa Bhutanese wakicheza. Picha kwa hisani ya Morgan Ommer. Copyright Demotix (15/2/2009)

Bhutan imebarikiwa na endelevu, urithi tajiri wa utamaduni na watu wa Bhutanese wana fahari katika kuunga mkono idadi ya maadili muhimu ikiwa ni pamoja na maelewano, huruma na uzalendo. Mwanablogu Dorji Wangchuk amekuwa akifanya kazi kurejesha watumiaji madawa ya kulevya na walevi na kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu wa tatizo miongoni mwa vijana wa Bhutanese. Yeye anadai kwamba kuwaelimisha watoto wewe mwenyewe haitoshi, kuna haja ya kufanya kazi ya ziada kwa bidii kuelekea kukuza watoto wa wananchi wenzangu kuwahamasisha wao kuwa binadamu wazuri.

Wanafunzi 3,000 Wafanya Maandamano dhidi ya Mageuzi ya Elimu Nchini Gabon

Mageuzi ya mfumo wa elimu yaliahirishwa [fr] nchini Gabon baada ya walimu na wanafunzi kuandamana pamoja kwa maandamano. Katika mapendekezo ya mageuzi, mitihani ya mwisho ili kupata diploma ya shule ya sekondari itafanyika katika duru moja badala ya mbili na kuingia katika shule ya sekondari zitafanyiwa mtihani wa mwisho badala ya kupita daraja mwishoni mwa mwaka wa mwisho wa katikati ya shule ya sekondari. Charlie M. anaelezea nini kilichoko hatarini :

Kwa kutenda papo hapo bila ya kusubiri ushauri wa namna bora ya kwenda mbele kutoka kwa mtu yeyote, wanafunzi walionyesha kwamba walikuwa na uwezo wao wenyewe, kwa kutambua kwamba ili kukabiliana na hali hiyo, ilikuwa ni muhimu kwao kuingilia kati na kuhamasisha. Hakuna mtu angefanya hivyo katika nafasi yao, hasa si wazee wao ambao hawana uwezo wa hayo. Vijana, tofauti na wazee wao, wanaelewa vizuri kwamba wanademokrasia, bila kujali maoni yao, hawezi kukubali kwamba haki zao zimekiukwa, na kwa hiyo hawawezi kunufaika linapokuja kwa masuala haya msingi kama vile haki ya elimu bora

A young student n in defiance of the security forces in the streets of Libreville, Gabon via le Gabon qui dit non

Mwanafunzi bila kujali vikosi vya usalama katika mitaa ya Libreville, Gabon kupitia le Gabon qui dit non

Ulaya Yamuonya Waziri wa Ufaransa Kuhusu Matamshi Yake Dhidi ya Warumi

Manifestation de Roms à Paris en 2007 photo Philippe Leroyer licence creative commons

“Komesheni Mashambulio” Maandamano ya Warumi mjini Paris – picha ilipigwa na Philippe Leroyer – leseni ya 3.0 ya creative commons

 

 

Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Manuel Valls, yalifufua uhasama uliokuwepo kati ya Ufaransa na Warumi. Bw. Valls alisema katika idhaa ya France Inter radio [fr] tarehe 24, mwezi wa Septemba:

ces populations ont des modes de vie extrêmement différents des nôtres et qui sont évidemment en confrontation [avec les populations locales]”.

Jamii hii ina utamaduni tofauti sana na wetu, na ni wazi kwamba utamaduni wao unahitilafiana na huo wa majirani zao.

Watumiaji wa Twita wazungumzao Kifaransa walimjibu, baadhi yao wakiandika kwa kejeli:

Warumi ndio wanaosababisha matatizo yetu yote, wao ndio wanaosababisha zaidi ya 25 % ya vijana barani Ulaya kukosa ajira.

Familia za Warumi zimejikuta mashakani: Ulaya, inayostahimili kuzorota kwa hali ya maisha, inawakataa, na mifumo ya kimafia inazidi kutajirika

Kwa vile alishughulikia suala nyeti lililogusia haki za binadamu nchini Ufaransa, Waziri alionywa na Baraza la Ulaya:

Ce débat perpétue une tendance inquiétante vers une rhétorique anti-roms discriminatoire et incendiaire, et risque de prendre un virage dangereux avec les prochaines élections municipales et européennes.”

Mjadala huu unaendeleza mwelekeo wa kusikitisha: matamshi ya kibaguzi na ya uchochezi dhidi ya jamii ya Warumi. Huenda ukawa mbaya zaidi wakati wa uchaguzi ujao wa ubunge na wa manispaa barani Ulaya.

China: Jukumu la Baba

Mtandao wa Offbeat China umeanzisha kipindi kipya na maarufu cha televisheni kinachojulikana kwa jina la “Baba, tunaelekea wapi?”. Kipindi hicho kinawakutanisha akina baba watano maarufu pamoja na watoto wao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za nje kwa lengo la kushindana na bila ya uwepo wa wake zao. Hapa chini, ni maoni ya raia, mtumiaji wa mtandao wa intaneti yaliyonukuliwa na mwanablogu mmoja:

‘Baba, tunaelekea wapi?’ kimekuwa kipindi kilichojizolea umaarufu sana, siyo tu kwa kuwa kimekuwa cha kuvutia na chenye kuleta mtazamo mpya, jambo la muhimu kabisa ni kuwa kinatupa taswira ya kiu na mategemeo ya kuenedelea kupendwa na kujaliwa zaidi na baba zetu.

Ufisadi: Tishio kubwa kwa uhuru wa kujieleza Barani Amerika ya Kusini

Katika miaka 20 iliyopita, waandishi wa habari 670 wameuawa katika Amerika ya Kusini na Caribbean,kwa mujibu wa wajumbe kutoka muungano wa IFEX-ACL, ambayo hivi karibuni iliwasilisha Ripoti ya Mwaka juu ya Ukatili 2013 iliyosema: “Nyuso na Mabaki ya Uhuru wa Kujieleza Amerika ya Kusini na Caribbean.” Uhalifu – ambao nyingi bado hazijatatuliwa – kufanya ukatili kuwa tishio kubwa kwa uhuru wa kujieleza katika kanda..

Silvia Higuera anatoa muhtasari wa ripoti katika Uandishi wa Habari wa Kituo cha Knight katika blogu ya Amerika. Anaongeza:

Kwa mujibu wa ripoti, Amerika ya Kusini iko katika wakati muhimu kwa uhuru wa kujieleza. Kulingana na mahali, waandishi wa habari wanapata vitisho kutoka kwa makundi ya uhalifu au udhaifu wa kitaasisi. Nchi nyingi pia zinapitia njia ya utata ya taratibu za kisheria ambayo inaweza kupunguza uhuru wa vyombo vya habari. Viongozi wa umma kuendelea kutumia kashfa za kesi za kisheria kunyamazisha vyombo vya habari, na sekta ya kihistoria yenye mazingira magumu — kama vikundi vya wenyeji — bado hawana uwezo wa kushiriki kwa uwazi katika masuala ya maslahi ya umma.

Misri: Picha 27 kutoka Hala'ib

Mwanablogu Mmisri, Zeinobia, amesambaza onyesho hili la picha kutoka Hala'ib, bandari na mji katika mwambao wa Bahari ya Shamu, kwenye Pembetatu ya Hala'ib, karibu na mpaka wa Sudan:

 

Hali ya Uhuru wa Dini Nchini Maldivi

Maldivi ni miongoni mwa nchi za kwanza kwenye orodha ya serikali zinazozuia uhuru wa dini. Ni lazima raia Wamaldivi wawe Waislamu, na hawawezi kufuata dini yoyote isipokuwa Uislamu. Wageni wasio Waislamu hawawezi kupiga kura, kuabudu hadharani, kupata uraia, wala kutumikia umma.

Kwa maoni ya Mwanahabari Hilath Rasheed, huenda nchi ya Maldivi ikashindwa kuegamisha uhuru wa dini katika miaka 50 ijayo, hadi kubadilika kwa mawazo ya vizazi vipya vya Wamaldivi.

Mandela na Mao, Hawakushabihiana sana.

Jeremiah kutoka katika studio ya Granite atoa maoni yake kwenye Televisheni ya Taifa ya China, CCTV akitaka kuonesha uhusiano uliokuwepo kati ya Mandela na Mao Zedong:

Mandela hakushabihiana sana na Mao. Mao alikuwa muumini wa udhanifu kama tafsiri ya neno linavyotanabaisha, mtu aliyeamini kuwa, mchakato wa utendaji wa jambo ndilo jambo la msingi sana kuliko matokeo yake, mara nyingi hata kama matokeo yanakuwa mabaya. Katika harakati zake, Mandela mara zote alikuwa akipigania usawa. Mara nyingi alionesha utayari wake wa kutumia mbinu mbadala za kuhakikisha ndoto yake ya usawa nchini Afrika Kusini inafikiwa.

Uruguay yawa Nchi ya kwanza Kuhalalisha Soko la Bangi

Baraza la Seneti la Urugwai lilipiga kura 16 kwa 13 kuhalalisha uzalishaji na uuzaji wa bangi.. Rais Mujica anatarajiwa kutia saini sheria, ambayo itakuwa na ufanisi kuanzia mwaka ujao.

Mimi ninaunga kuhalalishwa kwa bangi, lakini itakuwa vizuri kugonga vichwa vya habari duniani kote kwa sababu ya usalama wetu na elimu.

Ignacio de los Reyes, mwanahabari wa BBC Argentina na Southern Cone, alitwiti mnamo Desemba 10:

Stay tuned for more citizen reactions.

“Mimi ni Mchuuzi Mjerumani Mjini Dakar”

Muda mfupi baada ya kuwasili kwangu Senegal, nilikutana na kijana. Alinieleza hamu yake ya kuondoka Senegal katika mkutano wetu wa kwanza. Nilitaka kuelewa yaliyosababisha hamu yake ya kuondoka na hali ya maisha yake ya kila siku ili nipate kufahamu maelezo ya kijamii na ya kiutamaduni ya kutaka kwake kuondoka. Alikuwa mchuuzi. Kwa hivyo, siku moja nikamwomba ruhusa niandamane naye ili nimtazame akishughulikia pilkapilka zake za kawaida, naye akakubali. Kwanza, akanizungusha mitaani nikiuza bidhaa zake, eti nipate mafunzo. Aliifurahia faida aliyoipata [ ..] Kazi yangu mpya ikanipa uelewevu bora zaidi wa sekta isiyo rasmi nchini humu. Inajulikana kama “door waar,” na ina umuhimu wa kimsingi katika maisha ya vijana Wasenegal. [ ..] Mara nyingi nilikabiliana na mshangao kuhusu asili yangu. Watu wengi sana hawakuamini kwamba mzungu angeweza kushughulikia kazi za aina ile nchini humu. Mara kadha, watu walidhani kwamba nilikuwa mwaminifu kuliko wachuuzi wengine, na bidhaa zangu zilikuwa bora kuliko zao. Ilionekana kama kwamba watu wengi walidhani kuwa bidhaa za mwuzaji mzungu lazima ziwe za hali ya juu.

Kuwa mchuuzi mitaani si kazi rahisi, hasa nchini Senegali. Hata hivyo hilo ndilo chaguo alililofanya Sebastian Prothmann, Mjerumani asilia, baada ya kuwalisi Dakar, Senegal miezi michache iliyopita. Video hii inamwonesha Prothmann akiwa kazini[fr]:

Prothmann anaeleza katika mahojiano na blogu ya Dakaroiseries namna alivyojikuta akifanya kazi hii isiyo ya kawaida [fr] katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi:

Au début de mon séjour j’ai rencontré un jeune homme qui a lors de notre premier contact manifesté son désir ardent de quitter le Sénégal. J’étais curieux de comprendre son ‘’monde vécu’’ pour aboutir à des interprétations socio-culturelles sur  son envie  d’émigrer. Il était marchand ambulant. Donc, un jour je lui ai demandé si je pouvais l’accompagner dans sa routine quotidienne. Ce qu’il a accepté. Il m’a donc fait faire un premier tour, soi-disant pour mon apprentissage.  Il en  était réjoui, car on a fait de bons bénéfices [..] Avec cet engagement, j’ai eu plus des prises de conscience dans le secteur informel, communément appelé aussi « Dóor waar », qui joue un rôle fondamental pour la jeunesse sénégalaise. [..] j’étais souvent confronté à une incrédulité frappante quant à mes origines. La plupart des personnes n’ont pas cru qu’un homme blanc peut s’investir dans un tel travail. Plusieurs fois j’étais aussi confronté à une confiance plus élaboré á mon égard. Il y avait des considérations selon lesquels moi en tant que Blanc devait vendre des produits de bonne qualité.

Sababu za Ajali Barabarani Mjini Bangkok

Cha kushangaza, polisi mjini Bangkok, Thailand wanadai kwamba asilimia 30 ya ajali za barabarani husababishwa na ‘magari yasiyostahili kuwa barabarani’ wakati yanayo endeshwa kasi ni asilimia 5 ya ajali. Mwandishi Thitipol Panyalimpanun anabainisha kuwa katika nchi nyingi, ajali za barabarani hulaumiwa kwa makosa dereva na si juu ya magari.

Misri: Kampeni kwa Ajili ya Haki za Watu Wenye Mahitaji Maalum

Wamisri pembezoni wenye mahitaji maalum wamekuwa wakifanya maandamano kwa haki zao kabla na tangu mapinduzi ya #Jan25. Hata hivyo, malalamiko yao bado hayajatatuliwa. Wakati Kamati ya watu 50 wanapiga kura juu ya rasimu ya hivi karibuni zaidi ya Katiba ya Misri, kampeni ya Zayee Zayak, ambayo hutafsiriwa kuwa “Mimi ni kama wewe” lugha ya Kiarabu cha Misri kisicho rasmi, ilianza katika Misri kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya haki za kikatiba za watu wenye mahitaji maalum katika nchi.
Sensa ya 2006 ilionyesha kuwa karibu Wamisri milioni walikuwa na aina fulani ya ulemavu, lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yenye ari na mashirika ya kimataifa yanakadiria kuwa idadi yao haipungui milioni 8.5. Wanaharakati wa Zayee Zayak wanathmini kwamba Wamisri wapatao milioni 17 wanayo mahitaji maalum:

Unaweza kufuata mijadala kupitia kundi lenye ari, ‘Uelewa wa Ulemavu katika Jamii za wa-Misri’ (En).

Taiwan: Maandamano Dhidi ya Sheria Juu ya Usawa Kwenye Ndoa

Wabunge wa Yuan nchini Taiwan walipitisha muswada wa kwanza ya “Usawa kwenye Ndoa“ [zh] mnamo Oktoba 25, 2013. Novemba 30, zaidi ya watu 300,000 walipinga muswada huu, hasa dhidi ya pendekezo juu ya ndoa za jinsia moja. J. Michael Cole, mwandishi wa habari wa kujitegemea mkaazi wa Taipei, alielezea kile yeye alichokiona katika maandamano hayo katika blogu yake.

Kuwa na Mabadiliko – Shiriki Habari za Harakati za Kiraia

Kuwa na Mabadiliko ni tovuti mpya kwa hisani ya CIVICUS kwa watu kushiriki hadithi ya harakati zao wenyewe ili kuhamasisha wengine au kutafuta usaidizi.