Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Septemba, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Septemba, 2014

Papa Francis Kutembelea Eneo Lililokumbwa na Kimbunga cha Haiyan Nchini Ufilipino

Official logo for the papal visit to the Philippines in 2015

Nembo rasmi ya ziara ya Papa mtakatifu nchini Ufilipino mwaka 2015

Nembo na tovuti rasmi inayohusiana na ziara ya Papa Francis nchini Ufilipino mwezi Januari 2015 tayari imezinduliwa. Papa Francis atatembelea jiji la Manila ma Tacloban. Tacloban ndiko lilikotokea janga la Kimbunga cha Haiyan kilichochukua maisha ya watu 6,000 kwenye mkoa wa Visayas Kusini. Ukiachilia mambo Timor Leste, Ufilipino ni nchi pekee yenye wa-Katoliki wengi barani Asia.

Tafakari ya Suala la Kuoa Nje ya Tabaka lako Nchini India

Protest March in UK demanding to eradicate the centuries-old caste system that exists on the Indian sub continent and amongst expatriate communities. Image by Paul Davey. Copyright Demotix (19/10/2013)

Maandamano nchini Uingereza kudai kufutwa kwa mfumo wa kuoana kimatabaka uliodumu karne nzima na unaendelea Uhindini pamoja na kwenye jamii nyingine. Picha na Paul Davey. Haki miliki Demotix (19/10/2013)

Karthik Shashidhar, mshauri huru wa utawala na mwanasayansi wa takwimu, anaonesha takwimu kutoka kwenye utafiti wa kitaifa wa Afya ya Familia. Shashidhar anajadili idadi ya wanawake nchini India ambao wameolewa na watu wenye tabia lao wenyewe.Mfumo wa kimatabaka wa kihindi nchini India unaongozwa na amri ya makundi ya makundi ya kuoana wenyewe kwa wenyewe. Ndoa nje ya asili hiyo huchukuliwa kuwa kuvunja mila na desturi za ki-Hindi.

Utafiti huo, ambao ulifanywa kwenye majimbo yote nchini India, uliuliza wanawake ‘waliowahi kuolewa’ ikiwa waliolewa na watu wa familia zao wenyewe au mtu wa tabaka la juu, au mtu wa tabaka la chini. Matokeo yalionesha kwamba wastani wa taifa kwa idadi ya wanawake wanaoolewa na watu wa tabaka lao wenyewe ni 89%.

Serikali ya Marekani Yadai Takwimu za Shirika la Indymedia Athens

Imagen en Flickr del usuario Tim Pierce (CC BY 2.0).

Picha kwenye mtandao wa Flickr na Tim Pierce (CC BY 2.0).

Mnamo Septemba 5, Wizara ya Sheria ya Marekani iliitaka shirika linaloshughulika na masuala ya kuhifadhi tovuti iitwayo  May First kutoa taarifa za mmoja wa wateja wake, ambaye ni Kituo cha Ugiriki cha cha Uandishi Huru Athens, kinachofahamika kama Indymedia Athens. Likiwa limeanzishwa mwaka 2005, May First ni shirika lisilo la kibiashara linalojikita katika kutoa huduma za mtandao wa Intaneti, kama vile kuhifadhi tovuti za watu binafsi na mashirika. Taarifa zinazotakiwa na Idara ya Usalama ni habari maalum kutoka kwenye akaunti ya Indymedia Athens, iliyohifadhiwa kwenye vihifadhi takwimu (servers) za May First.

Katika  tamko, May First ilibainisha kwamba dai hilo linaweza kutafsiriwa kama jaribio la serikali ya Marekani kuisaidia serikali ya Ugiriki. Kadhalika, walibainisha kwamba hawatatoa taarifa zinazotakiwa labda ikiwa Kituo cha Uhuru wa Habari Athens kitazihitaji –wanasema kwamba kukubaliana na agizo hilo ni kuingilia haki ya faragha.

Kwa sasa, wanasheria wa Electronic Frontier Foundation, ambao wanaiwakilisha May First, wanawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Marekani. Wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, maafisa wa serikali wa Marekani hawajatoa maelezo yoyote kuhusu malengo hasa ya takwimu zinazodaiwa.

Uchafu Kutoka Viwandani Waua Mamia ya Ndege wa Porini Nchini Mongolia

Zaidi ya ndege wa majini 500 wameonekana wakiwa wamekufa katika eneo la maziwa nchini Mongolia tangu kuanza kwa majira ya kipindi cha joto kutokana na maji kuchafuliwa. Maji hayo machafu, kama ilivyotaarifiwa na wafugaji wa maeneo hayo, maji haya yaliyochanganyikana na taka sumu yalitoka katika eneo la viwanda. Annie Lee kutoka tovuti ya China Hush aliandika habari picha ya hali halisi ya tukio hili.

Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Liberia Wawekwa Shakani Kufuatia Vita Dhidi ya Ebola

The body of a victim of Ebola virus is seen covered with a sheet at the back of a truck inMonrovia, Liberia -Public Domain

Mwili wa mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa ebola ukiwa umefunikwa kwa shuka ukiwa umepakizwa katika gari huko Monrovia, Liberia -Public Domain

Umoja wa wanahabari wa Liberia wasikitishwa na hali ya kukosekana kwa uhuru wa upashanaji habari kufuatia hatua ya serikali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola. Umoja huu ulimwandikia barua Waziri wa sheria kumtaka kutafakari upya madhila wanayokabiliana nayo waandishi wa vyombo vya habari. Ufuatao ni muhtasari wa barua yenyewe:

Lengo la Umoja wa Vyombo vya habari wa Liberia umejikita haswa katika mambo ambayo siyo tu yanawakwamisha waandishi wa habari katika jukumu lao la kutafuta na kusambaza habari na taarifa muhimu kwa jamii, lakini pia, bila shaka yoyote, jambo jingine ni hili la kuhatarisha ushiriki wa vyombo vya habari katika vita ya kidunia ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola. Ni dhahiri kuwa, tasnia ya habari nchini Liberia imekuwa moja ya mshiriki mkuu katika harakati za kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madhara na changamoto zitokanazo na ugonjwa huu wa kuambukiza. Licha ya kupoteza mapato kufuatia mlipuko wa kushtukiza wa ugonjwa huu pamoja na athari zinazokabili maisha ya kila siku, vyombo vya habari vimeendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Kwa bahati mbaya, vikwazo kadhaa kutoka kwa watendaji wa serikali dhidi ya vyombo vya habari, hususani katika kipindi hiki, umetoa mwanya wa kuongezeka kwa hali ya sintofahamu kuhusiana na ugonjwa huu, na pia kuendelea kuongeza hali ya jamii kutokuamini uwepo wa ugojwa huu. Tunaamini kuwa hali hii haileti usawa na wala siyo sahihi.

Uimarishaji wa Amani ya Kudumu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wakati Umoja wa Mataifa ukizindua mpango wake wa kulinda amani kwa kutuma wanajeshi 1,500 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wafuatiliaji wachache wanajiuliza ni kwa nini uamuzi huu ulichukua muda mrefu pamoja na kuwepo kwa wahanga wengi wa machafuko. Les Cercles nationaux de Réflexion sur la Jeunesse (CNRJ) ni shirika lisilo la kiserikali mjini Bangui , Jamhuri ya Afrika ya Kati, linalojibidisha katika kuimarisha msingi wa amani ya kudumu nchini humo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Bangui. Ifuatayo ni video inayoonesha kwa kina kile kinachoendelea katika mkakati huu:    

Jinsi Wanablogu Walifikia Gerezani kwa Kuandika Kuhusu Haki za Binadamu Nchini Ethiopia

Melody Sundberg anachambua uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia baada ya wanablogu wa Ethiopia waliokamatwa kukaa siku 100 gerezani:

Ethiopia ina idadi ya watu 94,000,000 na ni nchi ya pili yenye wakazi wengi katika bara la Afrika. Hata hivyo, hailingani na mahojiano ya Endalkhachew Chala kupitia Global Voices, kuwa na gazeti huru la kila siku au vyombo vya habari huru. Kulikuwa na haja ya sauti mbadala na kwa hivyo Zone 9:ers walianza kublogu na kutumia vyombo vya habari vya kijamii kwa kuandika juu ya mada zinazohusiana na haki za binadamu. Jina la kundi, Zone 9, inawashiria maeneo ya sifa mbaya za gereza la Ethiopia Kality, ambapo wafungwa wa kisiasa na waandishi wa habari wamefungiwa. Gerezani ina maeneo manane, lakini “eneo” la tisa inawashiria Ethiopia. Hata kama ni nje ya kuta za gereza – hauko huru kamwe; mtu yeyote mwenye fikira huru anaweza kukamatwa. Wanablogu walitaka kuwa sauti ya eneo hili la tisa.

Katika mahojiano, Endalkachew anasema kwamba kundi lilikuwa na kampeni kuhusu kuheshimu katiba, kuacha udhibiti na kuheshimu haki ya kuandamana. Kundi pia lilitembelea wafungwa wa kisiasa, kama vile waandishi wa habari Eskinder Nega na Reeyot Alemu. Walitaka kuleta tahadhari kwa umma kwa kutumia vyombo vya habari vya kijamii.

Habari Mpya za Mgogoro wa Kisiasa Lesotho Kupitia Twita

Mfuatilie @nthakoana (Nthakoana Ngatane) kupata habari mpya zinazohusu mgogoro wa kisiasa nchini Lesotho. Nthakoana Ngatane ni mwandishi, msemaji, mwimbajii, mwigizaji na mwakilishi wa SHirika la Habari la Utangazaji la Afrika Kusini nchini Lesotho.

Mnamo tarehe 30 Agosti 2014, Waziri Mkuu wa Lesotho Tom Thabane alidai kulikuwa na jaribio la kumpindua kijeshi dhidi yake. Baade ilimbidi kwenda Afrika Kusini akihofia kupoteza maisha yake.

Nzige Wavamia Mji Mkuu wa Madagaska

Watumiaji-mtandao wa Twita na Facebook kutoka mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wamepachika picha kadhaa za nzige wakivamia mji. Uvamizi wa nzige sio tukio la ajabu nchini Madagaska, hasa baada ya dhoruba za kitropiki, lakini sio kawaida katika miji mikubwa. Nzige wanaweza kuwa na madhara makubwa kwa mazao, hasa katika nchi ambayo imekumbana na baa la njaa katika miaka iliyopita.

Kolombia: Hapana kwa Utalii wa Ngono Mjini Medellín

NoTurismoSexual

“Hapana kwa utalii wa ngono “. Picha mnato ya video iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube.

Kufikia katikati mwa mwezi Julai 2014, ukurasa wa Facebook Hapana kwa utalii wa ngono ulianzishwa, kwa lengo la kukuza uelewa kuhusu utalii wa ngono nchini Kolombia. Wikipedia inatafsiri dhana hiyo:

… una forma de turismo con el propósito de mantener relaciones sexuales, normalmente de varones con prostitutas hembras, pero también, aunque menos, hay mujeres turistas sexuales y turismo sexual homosexual masculino.

Utalii wa ngono ni safari zinazohusisha vitendo vya gono, hususani na kahaba. Shirika la Utalii Duniani , chombo maalum cha Umoja wa Mataifa, unatafsiri utalii wa ngono kama “safari zinazofanywa ndani ya sekta ya utalii au nje ya sekta hii lakini kwa kutumia muundo na mtandao wake, kwa lengo kuu la kuathiri kwa namna moja au nyingine uhusiano wa ngono za kibiashara kati ya mtalii na mkazi wa eneo analokwenda kulizuru “.

Hivi karibuni, ukurasa huo wa Facebook uliweka video hii, kama sehemu ya kampeni iliyowekwa na Mfuko wa Pazamanos kwa lengo la kuwakataa watalii wa ngono ambao mara nyingi hutembelea jiji la Medellín.

Kuhoji Kimya cha Vyombo vya Habari Siku za Wikiendi Kuhusu Habari za Ebola

“Ni lini Habari za Ebola zitatangazwa kwa masaa 24 siku saba za wiki?,” anauliza Profesa Crawford Kilian wa Marekani na Kanada:

Nimezoea kusikia habari mpya zikisitishwa kutangazwa nyakati za wikiendi. Vyombo vya habari, mashirika ya serikali, Asasi za Kiraia vyote vikiishia kutangaza habari siku ya Ijumaa mchana na kuibukia siku ya Jumapili asubuhi kwa mara nyingine.

Lakini baada ya majuma kadhaa ya Ebola, ninapoteza uvumilivu na jamaa wanaoishi kwa kutangaza habari za maradhi ya Ebola. Ndio, ni sawa kwao kwa makubaliano yao ya pamoja yanayowapa masaa manane kwa siku, bila kujumuisha wikiendi, siku za mapumziko na manufaa bora ya kiafya. 

Lakini kama Ebola haikubaliki kama anavyosema Dk Chan, vipi kuhusu kutafuta fedha za kuwalipa hawa jamaa kutumia muda wa ziada ili habari za ebola ziendelee kutangazwa hata muda wa Wikiendi (bila kutaja siku za mapumziko)? Unaweza kuona mazingira ambayo habari za Pearl Harbor zinasubiri mpaka mwandishi mmoja aje na ahabari zake siku za Jumatatu, Desemba 8, 1941? Au habari za kifo cha JFK zisitanagzwe mpaka siku ya Jumatatu inayofuata ya Novemba 25, 1963?

Lakini vyombo vya habari vya Afrika Magharibi, ukiacha vichache, vimekuwa vikipotea kuanzia siku ya Ijumaa mchana, na kuzinduka muda wowote siku za Jumatatu. Ndivyo yanavyofanya Mashirika kama WHO na mashirika mengine ya afya. Ninajua vizuri sana kwamba wanahangaika na kukosekana kwa mafungu ya fedha kutoka serikalini na hivuo vinafikiri nidhamu ya matumizi ni njia pekee ya kukabiliana na mdodoro wa mwaka 2008.

Filamu Yaonesha Namna Kabila Dogo Linavyojaribu Kuwazuia Wakata Misitu Kuharibu Mazingira

selungoSunset Over Selungo ni filamu ya dakika 30 inayoonesha namna kabila la wenyeji la Penan linavyopigania kutunzwa kwa misitu ya asili kwenye kisiwa cha Borneo nchini Malaysia. Borneo ni kisiwa kikubwa zaidi barani Asia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji huru wa filamu wa Kiingereza, Ross Harrison

Ushiriki Mkubwa wa Umma katika Mafunzo ya Tetemeko la Ardhi Nchini Mexico

Mnamo Septemba 19, 1985, kwenye maeneo ya kati, Kusini na Magharibi mwa Mexico, hususani kwenye Wilaya ya Shirikisho, yalikumbwa na tetemeko kubwa, linalosemekana kuwa baya zaidi katika historia ya Mexico inayojulikana. Wakikumbuka miaka 29 tangu tukio hilo litokee, Katibu wa Ulinzi wa raia wa Wilaya ya Shirikisho aliandaa mafunzo ya tetemeko, kwa ajili ya kuwasaidia watu kujua namna ya kuchukua hatua yanapotokea matukio kama haya. Watu walishiriki kwa kiasi kikubwa, katika jiji kuu la nchi hiyo pamoja na majiji mengine.

Tulifanya mazoezi ya uokoaji katika tukio ya tetemeko, tukikumbuka kile kilichotokea mwaka 1985 huko Mexico City.

Majengo yanayokadiriwa kuwa 17,000 yalifanyiwa uokozi wakati wa mafunzo hao.

Serikali ya Yucatán inayoongozwa na Rolando Zapata iliendesha mafunzo hayo kwenye ikulu ya nchi hiyo.

Tlalnepantla anashiriki mafunzo makubwa ya kupambana na matukio ya tetemeko la ardhi yaliyoongzwa na na serikali ya Mexico.

Mafunzo hayo yalikuwa si tu kuwakumbuka wahanga wa tetemeko la ardhi, bali kushughulikia jamii na taratibu za kirasimu za uendeshaji wa shughuli za serikali.

Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino

philippine_health_researchIkiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health) inalenga kuweka kumbukumbu na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo.

Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili kutoka porini katika kujikinga au kujitibu magonjwa yao. Lakini uharibifu wa mazingira na kushambuliwa vikali na tamaduni kuu za jamii zinazoishi mabondeni hivi sasa kunatishia mila hizo za tiba.

Wanabogu wa Togo Wamtania Rais Kufuatia Ujumbe wa Bango Barabarani

Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi/a>”. Raia wa Togo waliguswa na kuvutiwa na ujumbe huo. Waliingia kwenye mtandao wa Twita kuchekeshana kuhusiana na bango hilo na kutengeneza alama habari #merciPapaFaure (Asante sana Baba Faure). 

Sawa, vipi cheka kidogo na alama habari #mercipapaFaure ? 

Picha hiyo juu imesambaa mno kwenye mtandao wa Twita. Adzima anatoa maelezo kidogo kuhusu hali ya mambo ilivyo kwa watoto wa Togoshuleni.

Majadiliano na Picha za Mkutano wa Highway Africa 2014

Mkutano wa Highway Africa 2014 ulifanyika kuanzia tarehe 7-8 Septemba, 2014 kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini. Maudhui ya mkutano huo yalikuwa Mitandao ya Kijamii -kutoka pembezoni kwenda kwenda kwenye vyombo vikuu vy habari. Angalia picha na mzungumzo kuhusiana na mkutano huo hapa.

Je Kulikuwa na Jaribio la Mapinduzi Nchini Lesotho?

Sikiliza sauti inayoelezea kile hasa kinachoendelea nchini Lesotho kufuatia madai ya mapinduzi ya kijeshi:

Waziri mkuu amekimbilia nchini Afrika Kusini na anasema ni mapinduzi ya kijeshi. Jeshi la Lesotho linasema sio mapinduzi. Siasa zinazua utata. African Defence Review inazungumza na KRISTEN VAN SCHIE wa SADC na mwandishi DARREN OLIVIER kuuliza ni nini hasa kinachoendelea, na ni kiasi gani kulingana na zamani?

Watu 12 Hufa na Waniger 27,000 Huachwa Bila Makazi Kutokana na Mafuriko

Flooding in Niamey in Niger - Public Domain

Mafuriko mjini Niamey, nchini Niger – Miliki ya Umma

Mvua kubwa na mafuriko nchini Niger yamewaua watu 12 na kuacha maelfu bila makazi. Mito katika Niamey na maeneo ya karibu imefurika na kuharibu maelfu ya nyumba. Katika kanda, uharibifu wa ardhi na kilimo pembezoni mwa ardhi huzidisha hatari ya kwamba matukio yaliyokithiri yanaweza kubadilika kuwa maafa ya asili. Baadhi ya masuluhisho ya kujiandaa dhidi ya mafuriko yalikuwa yanatekelezwa na mamlaka za kitaifa:

ANADIA Niger ina malengo ya kuendeleza mbinu na zana za kutathmini hatari ya mafuriko, kutegemeza mipango kwenye viwango tofauti vya uamuzi, kuzidisha ujasiri wa jamii, na kuendeleza uwezo mkubwa zaidi wa kutabiri na kuitikia. Kwenye muktadha huu, uundaji wa hifadhidata ya mafuriko utachangia katika uamuzi wenye ufanisi mkubwa zaidi.