· Februari, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Februari, 2014

Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili

Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es].

Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna, isleño, miskito, pech, tawahka na tolupán, lugha ambazo ndizo zinazotengeneza urithi wa lugha wa nchi hiyo.” 

Kwa mfano, unapotafuta neno la ki-Hispaniola “pan” [es], lenya maana ya mkate, unapata majibu yafuatayo:

Mkate
Chakula kilichotengenezwa kwa unga. Neno hilo hilo linatafsiriwa kwa lugha saba kama ifuatavyo:
Ch. b’or.
G. fein.
I. bread.
M. bred.
P. síra arinayoka.
Ta. wan busna / brit.
To. sen

Theluthi ya Mimba Nchi Burkina Faso Hutungwa Bila Kutarajiwa

Watafiti wa Masuala ya Kijamii wa L’Institut supérieur des sciences de la population (Taasisi ya Sayansi ya Idadi ya Watu) mjini Ouagadougou, Burkina Faso ilichapisha ripoti yenye kichwa cha habari “Grossesses non désirées et avortements au Burkina : causes et conséquences” (Sababu na matokeo ya Mimba zisizotarajiwa na utoaji wa mimba nchini Burkina Faso). Ripoti hiyo inaangazia takwimu chache muhimu [fr]: 

  •  Un tiers de toutes les grossesses ne sont pas intentionnelles, et un tiers de ces grossesses non intentionnelles se terminent par un avortement.
  •  La taille de la famille désirée est en moyenne, de 6 enfants dans les zones rurales, contre 3 à Ouagadougou. 
  • Entre la moitié et les deux tiers de l’ensemble des femmes qui avortent sollicitent des praticiens traditionnels sans compétence particulière

-Theluthi ya mimba zote hazikutarajiwa, na theluthi ya mimba hizi husababisha utoaji wa mimba.
-Ukubwa wa familia inayotakiwa ni wastani wa watoto sita vijijini, ukifananisha na watatu jijini Ouagadougou.
-Kati ya nusu na theluthi mbili ya wanawake wanaotafuta huduma za kutoa mbimba huenda kwa waganga wa kienyeji wasio na ujuzi wa kitabibu unaotakikana. 

Caribian: Namna Vyombo vya Habari Vinavyoathiri Mitazamo

Venezuela na Haiti zimekuwa zikikabiliwa na maandamano ya kupinga serikali. Hata hivyo, ukuzaji wa mgogoro wa Venezuela unaofanywa na vyombo vya habari vya kimataifa na ukimya wake kwa mgogoro wa Haiti, unaibua maswali muhimu kuhusu kuyumba kwa Marekani katika kuimaisha tunu ya haki za binadamu na demokrasia.

Kevin Edmonds anatoa wito kwa vyombo vikuu vya habari.

Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani

Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya zamani ya NASA’, inaandika blogu ya Teknolojia ya Korea Kusini. Blogu hiyo pia inatambulisha toleo la video la picha hiyo linaloonyesha  Korea Kaskazini katika mukhtadha wa eneo lote la Asia Kaskazini. 

Madagaska Bado Inasubiri Waziri Mkuu, Serikali Mpya

Mwezi mzima tangu Rais mteule  Hery Rajaonarimampianina achaguliwe kuwa mkuu wa nchi nchini Madagaska, bado hakuna dalili nani atakuwa waziri mkuu na akina nani wataunda serikali. Ma-Laza anahoji kuwa suala kuu si hasa nani atakuwa waziri mkuu bali atakuwa ana ajenda gani akikabidhiwa ofisi [fr]: 

 Un  technicien hors pair,  rassembleur, capable de mener à bien la politique générale du Président de la République. Ce Premier ministre ne  devrait appartenir à aucune mouvance politique, en principe.Mais il n’est ni contre Rajoelina, ni contre Ravalomanana. Bref, c’est un oiseau rare qui inspire aux bailleurs de fonds la confiance. Cette personne existe-t-elle ?  

(waziri mkuu lazima awe) mtu mwenye wasifu wa weledi, mtu atakayewaunganisha watu na mwenye uwezo wa kushughulikia sera za Rais wa Jamhuri. Kinadharia, Waziri Mkuu lazima asiwe sehemu ya harakati za siasa. Hatakuwa kinyume na Rajoelina, wala  Ravalomanana (marais wawili waliopita). Kwa kifupi, lazima awe mtu nadra atakayewafanya wawekezaji wavutiwe kuja. Swali ni:  hivi mtu wa namna hii yupo kweli?

Sababu 10 Kwa nini Siafiki Shariah Nchini Pakistan

Mmoja wa msemaji wa Taliban alijitoa kwenye majadiliano ya hivi karibuni na serikali ya Pakistan na kudai kuwa ajenda ni pamoja na kuanzishwa kwa sharia kali. Mwanablogu wa Pakistan na Mwandishi wa Habari Beena Sarwar alipinga wazo hilo kupitia tamko aliloliweka katika mtandao wa Facebook lenye kichwa cha habari ‘sababu 10 kwa nini sitaki Shariah nchini Pakistan’ na linapatikana katika mitandao mingine ya kijamii kamaKusitisha Udini Pakistan, harakati za kupinga ukandamizaji, ubaguzi, kuvuka mipaka na uvumilivu na Uchaguzi wa Pakistani linaloendeshwa na Asasi za Kiraia. Hapa ni baadhi ya sababu:

1. Dini na ninavyochagua kuishi ni biashara yangu na ni suala lisiloihusu Serikali.

2. Kutekeleza Shariah hakutanifanya kuwa muislamu bora wala kuboresha hali ya mambo nchini Pakistan. Mataifa yote yaliyoendelea yanatawaliwa na serikali zisizo za kidini.

3. Kukataa wazo kwamba Shariah kwa namna yoyote inaweza kutekelezwa na wale ambao wamebaka na kupora nchi yangu, kulipua shule na misikiti na kukata askari vichwa. Sitawapa wahalifu hawa haki ya kuniamrisha.

4. Sitasalimisha haki yangu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na uhuru wa mawazo na kujieleza, chini ya kivuli cha Shariah..

Rais Yanukovych wa Ukraine ang'olewa madarakani

Baada ya maandamano, vurugu na upinzani dhidi ya serikali uliosababisha vifo vya watu wapatao 100, Bunge la Ukraine hatimaye limepiga kura ya kumwondoa Rais Viktor Yanukovych kama hatua ya kujibu shinikizo la waandamanaji.

Tayari Rais Yanukovych amenukuliwa akisema hana mpango wa kutoroka nchi.

Soma zaidi kupitia kiungo hiki [en]

Wavenezuela Waishio Mexico Wawambia Waandamanaji: “Hamko Pekeyenu”

Hali ya mambo nchini Venezuela yaendelea kuzorota, huku pakiwa na maandamano na mikusanyiko nchi nzima ayalisababisha vifo vya watu kumi na mamia kujeruhiwa mpaka sasa. Wavenezuela duniani kote wanaopinga serikali yao wameandaa mikusanyiko ya amani kupaza sauti zao na kuzifanya serikali za nchi wanazoishi kuelewa mwenendo wa mambo. Mexico haija nyuma.

Mexico City, February 16th

Jiji la Mexico, Februari 16. Picha ya Patricia Acosta, mwandishi wa mwanzo wa makala haya.

Raia wa Venezuela wanaoishi Mexico wametumia mitando ya kijamii kuandaa maandamano Februari 16. Baada ya kukutana kwenye sanamu ya Simon Bolivar (Baba wa taifa la Venezuela) iliyoko kwenye eneo la Polanco, waandamanaji walitembea kupitia kwenye mtaa wa Reforma wakielekea mahali panapoitwa Malaika wa Uhuru. Hapo, wakiungwa mkono na baadhi ya wananchi wa Mexico, Wavenezuela hao walidai uhuru wa habari wakati huu ambapo vyombo vya habari vimezuiwa kutangaza habari na kuimba wimbo wa “uhuru”, “amani” na “hatutaki vifo zaidi”, kisha wakaimba wimbo wa taifa wa Venezuela kama inavyoonekana kwenye video ifuatayo [es]:

Baada ya maandamano haya, Wavenezuela waliandaa mkesha mbele ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Marekani (OAS) jijini Mexico tarehe 18 Februari. 

Vigil, Tuesday February 18th

Mwaliko kwenda kwenye mkesha wa Februari 18

 
Wakipepea vitambaa vyeupe na kukeba mishumaa, Wavenezuela hao walifanya maombi kwa ajili ya wanafunzi waliouawa tarehe 12 Februari. “Huu ni ujumbe wangu kwa Venezuela: Hamko peke yenu”, alisikika mwanamke mmoja kwenye mkesha huo. 

In Mexico City

Mkesha wa Mexico City, Picha ya Patricia Acosta, mwandishi wa mwanzo wa makala haya.

Wamalagasi Wajadili Kivazi na Maoni ya Mlimbwende wa Kigeni Kuhusu Madagaska

Picha ya Tangazo la Kivazi cha Kuogolea 2014 iliyopigwa eneo la (kisiwa cha) Nosy Iranja, Madagaska:

Nosy Iranja ni kisiwa kinachofahamika kama Turtle kwa sababu viumbe waitwao Hawksbill Turtles walikuja ufukweni kutaga mayai yao. Kisiwa hicho pia kinafahamika kwa mchanga wa pekee unaounganisha visiwa hivyo viwili.

Nosy Iranja, Madagascar - Public Domain

Nosy Iranja, Madagaska – Kwa matumizi ya umma

Mlimbende mashuhuri wa ki-Rusi Irina Shayk na mke wa msakata kandanda Cristiano Ronaldo alisema kwamba ana uhusiano maalumu na Madagaska:

Nilipokuwa mwanafunzi niliripoti kuhusu Madagaska, na tangu wakati huo imekuwa ni ndoto yangu kubwa kwenda kule [..] Watu (Malagasi) wanaishi na kutembea kila siku kwenye barabara, wakiishi maisha ya kawaida, na bado wanafuraha. Ni uzoefu unaokufanya uwe mnyenyekevu, na kuyatafakari mambo katika kina chake.

Rakotonirina Miaro anashangaa kwa nini ulimwengu nje ya Madagaska wanaonekana kuvutiwa mno na utajiri wa kisiwa hicho laini raia wa Kimalagarasi hawaonekani kujali [mg]:

Ny olon-kafa maita ny hatsaran'ny Nosin-tsik fa ny tompony jay no tsy mahafatatra fa tsar i Gasikara! Tsara daholo ny mannequin naka sary é!

Wageni wanajua ni kwa jinsi gani kisiwa chetu kina uzuri wa asili lakini sisi, tunaoishi hapa, hatuonekani kuvutiwa na raslimali zetu wenyewe. Ndio, na picha za nguo za kuogelea hazikuwa mbaya kuzitazama hata hivyo

Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal

Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75), rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.

Mbinu za Uvuvi Endelevu kwa Wavuvi wa Dhivehi

Mwanablogu wa MaldiviHani Amir anaandika kuhusu mbinu za uvuvi asilia ikiwa ni pamoja na kukamata mamia ya samaki kwa mikono yao, badala ya kutumia nyavu au fimbo. Mwanablogu huyo pia anatoa mwangaza kuhusu namna wanavyonnyonywa na wamiliki walafi wa hoteli wnaojaribu kuwaibia kwa kutokuwalipa kile wanachostahili.

Orodha ya Waliouawa Katika Maandamano ya Venezuela Yapatikana kwa Lugha Tano

Katika blogu ya Panfleto Negro [es], John Manuel Silva na Emiliana Duarte wanafuatilia orodha ya vifo vilivyotokea kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Venezuela. Orodha hiyo -ambayo awali ilikuwa kwa lugha ya Kihispania-imetafsiriwa kwenda lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kiitaliano/a> na Kifaransa.

Pakistan, Usiingilie Vita vya Ndani ya Syria

Siku moja baada ya dondoo ndogo ya habari yenye kichwa cha habari, “Saudi Arabia ‘inatafuta uungwaji mkono kwa waasi wa” ilipoonekana kwenye magazeti ya Pakistani, mwanablogu wa siasa Ahsan Butt aliposti tahadhari kali kwa watunga sera ya mambo ya Kimataifa wa nchi ya Pakstani kuachana na mambo ya ndani ya Syria.

Katika makala ya “Hii siyo vita yetu (Toleo la Syria)” kwenye blogu ya Five Rupees, Ahsan anaandika:

Kile ambacho Pakistani inakifanya kinyume cha Syria ni moja wapo ya mambo ya kijinga kabisa kuwahi kufanywa na Pakistani kwa muda mrefu, na ambalo linatuma ujumbe muhimu. Vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria, hatika hali mbaya ilivyo, haihusu Pakistani kwa vyovyote vile. Pakistani haina maslahi yoyote kwenye mgogoro huo. Hakuna.

Saudi Arabia iko kwenye mazungumzo na Pakistani ili kutoa ndege na roketi za kivita zilizotengenezwa Pakistani. Ahsan anaonya:

Hivi ni busara na inashauriwa kweli kujiingiza kwenye vita vya ndani ya nchi iliyo kwenye umbali wa maili elfu mbili?[…]

Hebu saili mwenendo wa ghasia hizi katika muongo uliopita.

Anaeleza kuwa hatua yoyote ya kuingilia mambo ya Syria itailazimisha serikali ya Pakistani kuanza kutazama kwa makini kukua kwa ghasia za kidini ndani ya nchi:

Yepi ni madhara yanayowezekana kutokana na sera za aina hiyo linapokuja suala la ghasia za kidini nchini Pakistani? Je, inawezekana ikachochea misuguano ya kidini au kinyume chake?

Ahsan anaorodhesha maswali manne ya kufikirisha zaidi ambayo unaweza kuyasoma hapa.

PICHA: Vyama vya Wafanyakazi na Asasi za Kiraia Vyaandaa Mgomo

Huku ukiwa umepangiliwa ufanyike mwanzo wa kipindi cha pili cha Rais Park Geun-hye madarakani, takribani wa-Korea elfu 40 (polisi wanadai ni elfu 15) walifanya mgomo nchini kote. Mgomo huo, ulipangwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Korea, ukiwa na wito wa kusitishwa kwa kudhibitiwa kwa vyama vya wafanyakazi, hatua ya serikali kubinafsisha sekta ya umma na kufunikwa skandali ya wizi wa kura katika uchaguzi wa rais. Mwandishi wa habari za kiraia anayeheshimika Mongu alitwiti picha ya maandamano (imewekwa hapa chini). Picha zaidi zinaweza kupatikana kwenye ukurasa wa Facebook wa chama cha wafanyakazi [ko].

Mgomo mkubwa, kwenye Ukumbi wa Seoul City Hall Plaza. Ulijaa vilivyo.

Shirika la UNICEF Latoa Wito wa Kutokuweko kwa Watoto Katika Maandamano Nchini Thailand

Baada ya mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono nakuwauwa watoto watatu katika maandamano ya kupambana na serikali katika eneo la Bangkok, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa lilitoa wito kwa serikali na viongozi wa maandamano kuwalinda watoto na kuwaweka mbali na maandamano. Bijaya Rajbhandari, Mwakilishi wa UNICEF nchini Thailand, ametoa wito huu:

(UNICEF) inalaani vurugu ambayo ilisababisha maafa haya na vifo vya kipumbavu na majeraha kwa watoto. Matukio haya kusisitiza haja ya haraka ya kuweka watoto nje ya njia ya madhara ili kuhakikisha usalama wao. UNICEF inataka Serikali, na viongozi wa maandamano dhidi ya serikali na wazazi wote kuhakikisha kuwa watoto hawaingii katika maeneo ya maandamano na kutunzwa vizuri mbali na maeneo yote ya maandamano..

Sinagogi Pekee Lililobaki Myanmar

Lilijengwa miaka 120 iliyopita, Sinagogi la Musmeah Yeshua lililoko eneo la Yangon ni Sinagogi pekee la wayahudi lililoyobaki katika eneo linaloongozwa na waumini wa dini ya Kibudha waishio nchini Myanmar. Mbali na kuwa kivutio cha utalii, pia limetajwa kama jengo la urithi la mambo ya kale katika mji huo.

Upasuaji wa Kwanza wa Moyo Kongo Brazzaville

Child awaiting heart surgery via La chaine de l'espoir with their permission

Mtoto akingojea upasuaji wa moyo. Picha kwa hisani ya La chaine de l'espoir imetumiwa kwa ruhusa yao

Mtandao wa kimataifa wa Afya La Chaîne de l’Espoir (Maana yake Kiungo cha Matumaini) unaripoti kuwa watoto saba wa ki-Kongo waliokuwa na hali mbaya wamenufaika na upasuaji wa moyo [fr] uliofanyika Februari 14 mjini Brazzaville, Kongo. Kwa msaada wa Msaidizi wa Kongo Shirika lenyewe, Prince Béni na Maya, wote wakisumbuliwa na maradhi ya moyo walifanyiwa upasuaji kwa masaa kadhaa kama ripoti ifuatayo inavyosema [fr]:

Elle a dix ans et ne pèse que quinze kilos. Son cœur fonctionne mal. Il l'empêche de s'alimenter et donc de grandir. La petite fille doit être opérée le plus vite possible. L'intervention dure six heures.

(Mayala) ana umri wa miaka kumi na ana paundi 15. Moyo wake haufanyi kazi ipasavyo. Unamzuia kupeleka virutubisho kwenye seli zake na hivyo kuleta matatizo ya ukuaji hafifu. Msichana huyu alihitaji upasuaji wa haraka. Na upasuaji huo ulifanyika kwa masaa sita.

Vyombo Vikuu vya Habari Vyaihujumu Facebook

Mwanablogu wa Teknolojia Amitha Amarasinghe anadai kwamba mtandao wa Facebook unapewa taswira hasi na vyombo vikuu vya habari nchini Sri Lanka kwa vichwa vya habari kama “Mwanafunzi ajiua shauri ya picha iliyowekwa Facebook”, “Mapenzi ya Facebook yaishia na kifo” na kadhalika.

Ghafla tu, kuna mwongezeko mkubwa wa maudhui yanayotoa taswira hasi ya mtandao wa Facebook na Mitandao mingine ya kijamii. Kama ukichunguza habari hizi, [utagundua kuwa] vyombo vya habari vya hapa vinaitumia “Facebook” kama sehemu ya “habari”, lakini vikishindwa kuoanisha sababu za kijamii, kitamaduni, na kisiasa zinazosababisha matukio hayo.

Tafakuri kwenye Mkutano Mkubwa Zaidi wa Blogu Nchini India

#WIN14, mkutano mkubwa zaidi na tuzo zinazoongoza nchini India, unaoandaliwa na BlogAdda, ulifanyika Februari 89, 2014. Mwanablogu Dk. Roshan Radhakrishnan, aliyeshinda tuzo ya blogu bora ya uandishi wa ubunifu nchini India, anatoa maoni na picha zake.

Waandishi wa Habari za Kiraia, Jiandikishe Kupata Video Bure

Spilno.TV

Jukwaa linalokusanya video kadri zinavyowekwa mtandaoni linaloitwa Ustream linalota fursa ya kujiandikisha kufungua anuania mpya na pia kuzitangaza kwa ajili ya kuzitumia video hizo kwa ajili ya habari zinazotokea, uanaharakati na hata kwa matumizi ya mengine ya faida kwa jamii.

Hivi karibuni Ustream imesaidia chaneli tatu za moja kwa moja kutoka kwenye maandamano ya Ukraine , ikiwa ni pamoja na chaneli maarufu ya Spilno.tv.

“Tulitengeneza Ustream kwa Mabadiliko kutambua jitihada za watengenezaji hawa mahiri wa video za kijamii, na tunatumaini kuwatia moyo wengine kufikiri nje ya kuta na kukuza nguvu ya video za moja kwa moja,” anasema Brad Hunstable, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Ustream.

“Ustream inaunga mkono kwa dhati kabisa uhuru wa Mtandaoni, jamii zilizo imara na demokrasia changa. Teknolojia yetu inatoa namna ya kuufikia uwazi kwa pende zote za kamera, na tunatarajia kuunga mkono kwa dhati wale wanaoongoza harakati za kuleta mabadiliko chanya,” anasema.