Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Aprili, 2015

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Aprili, 2015

‘Kulea Mtoto Ukiwa Mtoto': Idadi Kubwa ya Mimba za Utotoni Nchini Venezuela

Desireé Lozano, anayeblogu kwenye blogu ya Voces Visibles, anatoa mwito kwa ongezeko kubwa la mimba za utotoni nchini Venezuela, ambapo asilimia 25 ya mimba ni za vijana, na kukosekana kwa sera sahihi za kudhibiti tatizo hili na matokeo yake. Takwimu za Venezuela zinaonesha kwamba nchi hiyo ina idadi kubwa ya mimba za utotoni barani Amerika ya Kusini na imekua ya kwanza kwa miaka miwili iliyopita.

Vifo vya watoto ni suala kuu linalohusiana moja kwa moja na mimba za utotoni. Desiree anamtolea mfano Dinorah Figuera, makamu wa rais wa Kamati ya Bunge inayoshughulika na Familia aliyesema kwamba wajibu wa serikali ni kuzuia mimba hizo:

“Una de esas consecuencias es que las madres adolescentes son mujeres que pierden oportunidades para desarrollarse desde el punto de vista profesional y aceptan cualquier tipo de trabajo para tener algún tipo de ingresos. Por esta razón el Estado debe aplicar una gigantesca campaña de concientización para la prevención del embarazo adolescente”, señala la diputada venezolana

“Matokeo moja wapo ya kuwa mama katika kipindi cha utoto ni mwanamke kukosa fursa za kujiendeleza kitaaluma, na hivyo kujikuta akifanya kazi yoyote ile kujipatia kipato. Kwa sababu hii, serikali lazima ifanye kamepni kuba kuzuia mimba za utotoni,” alisema.

Kwa nyongeza, mimba za utotoni zinachangia kuongezeka kwa umasikini wa kipato kwa wanawake. Zaidi, hali hii inaleta hatari kwa afya ya mama, hatari kubwa kuliko kawaida. Kwenye makala yake, mwandishi anakusanya matamshi mbalimbali ya wataalamu kuhusu suala hilo na hivyo kutoa mwanga kuhusiana na tatizo hilo.

Endele kusoma kazi za Desireé Lozano na Voces Visibles hapa au kwenye mtandao wa Twita.

Makala haya ni ya 46 kwenye mfulululizo wetu wa #LunesDeBlogsGV  (Jumatatu ya Blogu GV) mnamo Aprili 13, 2015.

Swali: Wapiganaji Wangapi wa Jihadi Wana Historia ya Jeshi?

Kwa kutumia dondoo kutoka kwenye ripoti ya Der Spiegel kuhusu watu walionyuma ya muundo wa ISIS, mwanablogu wa Palestina Iyad El-Baghdadi anatwiti:

Baada ya habari ya Spiegel kuhusu watu walio nyuma ya uongozi wa ISIS – nimejiuliza wapiganaji wa Jihadi wangapi wana historia ya jeshi?

Der Spiegel anamtaja Iraqi Samir Abd Muhammad al-Khlifawi, aliyeuawa huko Tal Rifaat in Syria mwezi Januari 2014, kuwa ndiye “moyo” wa ISIS, tawi la Al Qaeda ambalo limekuwa na udhibiti wa nchi kama Iraq na Syria, wakiacha hofu, vifo na uharibifu sehemu mbalimbali. Inasema kwamba al-Khlifawi alikuwa kornel wa zamani kwenye kitengo cha ujasusi katika jeshi la ulinzi wa anga enzi za utawala wa Saddam Hussein.

El-Baghdadi anaongeza:

Kamandi kuu ya ISIS ina mafisa wa zamani wa Jeshi la Iraq; nchini Libya maafisa wa zamani wa jeshi la Gaddafi ndio wanaunga mkono ugaidi huu…

Anaeleza:

ISIS nchini Misri (Sinai) pia ina maafisa kadhaa wa zamani wa jeshi la Misri; Mkuu wa Ansar Bayt al Maqdis ni komandoo wa zamani wa jeshi la Misri


Hakiki taarifa hizi:

Tusaidie kufuatilia na kuhakiki habari hizi kuhusu wakuu wa ISIS wenye histori ya jeshi kwenye dawati letu la kuhakiki utaarifa la Global Voices hapa.

Filamu ya Malawi Yawasaidia Wakulima Kujikinga na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Filamu ya “Mbeu Yosintha” ilitengenezwa kuwasaidia wakulima na wanavijiji kujikinga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, hususani kubadilika kwa majira ya mvua kwenye ukanda wa Afrika Kusini Mashariki. Filamu hiyo ni tamthlia inayowatumia wasanii wa ndani ya nchi hiyo na iliandaliwa na mwandishi wa Kimalawi Jonathan Mbuna baada ya utafiti wa kina uliofanywa na Asasi Sizizo za Kiserikali zinazojishughulisha na kilimo nchini Malawi.

Kulinda Taarifa Binafsi Nchini Ajentina Bado Kuna Safari Ndefu

Cloud Computing - Photo by Quinn Dombrowski on Flickr. (CC BY-NC-SA 2.0).

Ulinzi wa taarifa za kompyuta – Picha na Quinn Dombrowski kwenye mtandao wa Flickr. (CC BY-NC-SA 2.0).

Kwenye makala iliyoandikwa kwa ajili ya gazeti la mtandaoni Haki za Kidijitali: Amerika Kusini & Visiwa vya Caribbean, No.21Mmwanasheria wa ki-Ajentina Valeria Milanés anaeleza kwamba hata kama Marekani ni kiranja wa dunia kwenye kuchakata taarifa (data), bado haina sheria ya kulinda taarifa za watu. Marekani pia inachukuliwa kama nchi yenye “kiwango kisichofanana cha ulinzi kwenye viwango vya kitaifa na kimataifa.”

Bahati mbaya, katika bara la Amerika Kaskazini na nchi nyingine, mabadiliko ya teknolojia yamezidi kwa mbali kutengenezwa kwa sheria zinazodhibiti matumizi yake. Milanés anaeleza hali ilivyo nchini Ajentina na kuitaja Kurugenzi ya Taifa ya Kulinda Taarifa za watu na Sheria ya Taarifa Binafsi, D.N.P.D.P., (Sheria 25.326 na 26.343), ambayo ni kati ya “masuala muhimu zaidi ya ulinzi wa taarifa.” Tatizo ni utekelezaji wake:

…en 2012, y luego de doce años de funcionamiento, la D.N.P.D.P. tenía registradas 20.000 bases de datos, contra 1.600.000 que tenía registradas a la misma fecha y en similar plazo la Agencia Española de Protección de Datos.

…mwaka 2012, baada ya miaka kumi na mbili ya utekelezaji, taasisi ya D.N.P.D.P. imeandikisha ‘database’ 20,000, ukilinganisha na ‘database’ 1,600,000 zilizoandikishwa katika kipindi hicho hicho na Wakala wa Ulinzi wa Taarifa nchini Uhispania.

Milanés anasema kwamba mfumo wa kulinda taarifa kwenye kompyuta unaleta changamoto mpya:

…las grandes empresas multinacionales prestadoras de los servicios de nube pública se caracterizan por utilizar contratos de adhesión, que por lo general no contienen las especificaciones requeridas en la ley 25.326 y en los que hasta la ley aplicable y jurisdicción prefijada corresponde al país en los que estas empresas tienen sus domicilios legales –por lo general, ciudades de Estados Unidos–. Es más, inclusive los servidores en los que se almacena la información pueden no encontrarse en Argentina.

…lwatoa huduma wakubwa wa kimataifa wanaolinda taarifa za watumiaji wnaafahamika kwa kuheshimu mikataba, ambayo mara nyingi huwa na masuala mahususi yenye misingi ya Sheria 25.326 na ambayo sheria zinazotumika na mamlaka ya kisheria ni yale ya nchi ambazo makampuni hayo yanatoka, na mara nyingi ni miji ya Marekani. Zaidi, hata vifaa vya kuhifadhia taarifa [servers] mara nyingi hazipo nchini Ajentina

Kwa hiyo, uzoefu wa wa-Ajentina hautofautiani na ule wa nchi nyingine kwenye ukanda wa Amerika Kusini, pamoja na kuwa na sheria za kulinda taarifa binafsi na makampuni bado safari ni ndefu.

Milanés anahitimisha kwa kusema kwamba suala hili linahitaji “kuchukua hatua za utekelezaji adhubuti unaoendana na sheria za sasa na kutumika kwa mifano bora ya kibiashara inayoruhusu, kwa kiasi kikubwa, faragha ya taarifa binafsi na kutoa uhakika wa usalama unaotakikana.”

Umoja wa Ulaya Hautatoa Nafuu ya Kodi ya VAT kwa Vitabu ya Kidigitali

Imagen compartida por Blog de sinerrata editores    usada con permiso

Bendera ya Umoja wa Ulaya. Picha ya Sinerrata Editores, imetumiwa kwa ruhusa.

Mnamo Machi 5, 2015, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwamba punguzo la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) lililotolewa kwa vitabu vinavyochapishwa halitahusisha vitabu vya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kila kinachosambazwa au kutolewa kwa mfumo wa kieletroniki au kwa mtandao wa intaneti ni huduma. Amalia Lopez anahoji hukumu hiyo kwenye blogu ya Sinerrata Editores:

Lo que más me ha llamado la atención es que refuerzan la decisión utilizando el argumento del soporte, […] que igual tuvo sentido en algún momento del pasado pero hoy en día me resulta completamente absurdo. Es verdad, el libro electrónico es un archivo no un objeto pero, ¿es un libro menos libro porque lo guardo en mi ordenador o mi lector electrónico en vez de en la estantería? ¿Cuándo leo un libro digital la experiencia cultural es menor que cuando es un libro de papel? Es decir, lo que este tribunal ha sentenciado (o esa es mi interpretación) es que lo que hace de un libro un producto cultural y por tanto merecedor de un impuesto reducido (y un menor coste para los consumidores) es el papel en el que está impreso.

Kinachonishangaza ni kwamba walitumia mfumo wa kitabu kama hoja ya kufanyia maamuzi yao, […] jambo linaloweza kuwa na mantiki kwa kipindi cha nyuma, lakini leo, ninaona huu ni sawa na upuuzi. Ni kweli, kitabu cha kidijitali ni faili tu na sio kitu, lakini je nikikiweka kitabu kwenye kompyuta yangu au kifaa kingine cha kukisomea badala ya kukiweka kwenye kabati, hiyo inakifanya kisiwe na hadhi ya kitabu? Ninapokisoma kitabu kilicho kwenye mfumo wa kidijitali, uzoefu wa kitamaduni ninaoupata unakuwa pungufu ya ule ninaoupata nikiwa nakisoma kitabu kwenye karatasi? Ndio kusema, kilichoamuliwa na mahakama (au, angalau, hiyo ni tafsiri yangu tu) ni kwamba kinachofanya kitabu kiwe zao la utamaduni, na hivyo kustahili kupata punguzo la kodi (na hiyo maana yake ni punguzo la bei kwa wateja), ni karatasi linalotumiwa kuchapishia kitabu hicho.

Uamuzi huo unahusisha vitabu vinavyopakuliwa au kutazamwa mtandaoni na inahusisha mifumo kama kompyuta, simu za kisasa na vifaa vingine vya kusomea.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu mada hii kwenye makala ya  Amalia Lopez kwenye mbogu ya Sinerrata Editors, na kuwafuatilia kwenye mtandao wa Twita: @Sinerrata.

Makala haya ni sehemu ya 43 ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV) mnamo Machi 2, 2015.

Mpigania Amani wa Uganda awa Miongoni mwa Watakaoshindania Tuzo ya Amani ya Nobeli

This is Uganda (ThisIs256) ni jukwaa la waandishi waliobobea kutoka Uganda walio na utayari wa kuandika habari makini za kuihusu nchi yao, wakilenga kutokomeza uanahabari uchwara, njaa, Ebola, ukabila, pamoja na mambo mengine. Wanachojaribu kukifanya ni kuanzisha aina ya utafiti kuihusu Uganda ambao ni halisi, makini, wa kweli na usio wa kiupendeleo ambao kamwe usingalikuwa rahisi kuuona kwenye vyombo vikuu vya habari vya magharibi.

Habari yao ya hivi karibuni ni ya kumhusu Victor Ochen,aliyekuwa mmoja wa wakimbizi wa ndani, aliyependekezwa na American Friends Service Committee (AFSC), ambayo ni taasisi ya utetezi wa haki za kiraia, kushindania Tuzo ya Amani ya Nobeli.

Kwa kipindi cha nyuma, AFSC iliwapendekeza akina Desmond Tutu, Martin Luther King Jr., na Rais wa Marekani, Jimmy Carter, ambao wote walifanikiwa kushinda tuzo hii. Taasisi hii mara kadhaa ilimpendekeza Mahatma Gandhi, ambaye hata mara moja hakufanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli, pamoja na kupendekezwa kuigombea mara tano kati ya miaka ya 1937 na 1948.

Ochen, mwenye umri wa miaka 33, alianzisha taasisi ya African Youth Initiative Network, mnamo mwaka 2005 iliyo na mskani yake huko Lira, Uganda, taasisi iliyo na jukumu la kuwasaidia watu kurudia katika hali yao ya awali wakiwemo wale walioungua kwa moto, ukeketaji wa namna mbalimbali, ubakaji, pamoja na unyanyasaji wa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha vijana katika masuala ya uongozi. Hadi sasa taasisi hii imeshapanuka kiasi cha kuwa mtandao wa kimataifa wa wataalamu wa tiba ambao jukumu lao ni kuwasaidia wahanga kujenga upya makazi yao na maisha yao. Kwa mujibu wa This is Uganda:

Kwa kile Victor alichokifanya kwa moyo wake wa dhati wa kujitolea, ndicho kilichomfanya kuwa mmoja wa watu waliopendekezwa kuwania tuzo hii iliyo ya heshima ya hali yajuu. Akiwa kijana mdogo katika kambi ya Abia iliyokuwa na watu zaidi ya 40,000, kambini hapo, aliweza kuanzisha kikundi cha amani akiwa na wenzake. Mkakati huu uliwakasirisha wazee kiasi cha kumuuliza “Kwa nini unaongelea amani ambayo hujawahi kuiona?” Alijitolea; alihatarisha maisha yake kwa kuchoma mkaa ili apate ada ya shule. Baadae alijiunga na elimu ya sekondari ambapo ni mara chache sana alipata muda wa kufanya biashara yake ya mkaa, hivyo alilazimika kuwa fundi viatu, alikuwa akirekebisha viatu vya watoto shuleni. Wakati fulani Victor alijipatia kazi nzuri ya kufanya maboresho ya viatu vya timu ya shule ya mpira wa miguu, kwa bahati mbaya fedha aliyoipata iliibwa. Kusoma kwake kwa bidii na kupendwa kwake na walimu kulimuwezesha kusoma elimu ya upili

Victor alionesha uzalendo wa kweli kwa nchi yake hata pale alipokuwa akifanya kazi na taasisi ya straight talk foundation ya Kampala, alipokuwa akikutana na watu katika shughuli zake aligundua kuwa watu wa Kaskazini mwa Uganda kuna mengine zaidi walistahili na walihitaji mbali na vipeperushi. Na hili ndilo lililomfanya akaacha kazi yake na kuanzisha Mradi wa Mtandao wa Vijana wa Kiafrika (African youth initiative Network). Mradi huu unazikutanisha jamii na hususani vijana ili waweze kudumisha amani pamoja na kulinda haki za binadamu na kuleta maridhiano. Wanatoa msaada wa saikolojia ya inayohusiana na matatizo ya kijamii, wanatoa msaaada kwa wahanga wa migogoro iliyotokea kipindi cha nyuma, wengi wao wakiwa ni wale walio na maumivu makali ya kihisia na wanaohangaika kupata msamaha, pia wameshasaidia zaidi ya watu 5000 waliokuwa wanahitaji upasuaji wa kurekebisha sehemu za mwili hususani kwa wanawake ambao midomo yao ilikatwa. Mradi huu ambao pia unawawezesha vijana katika shughuli mbalimbali za kuwapatia kipato, umesaidia pia kuaanzishwa kwa klabu 100 amani kaitka mashule na kwenye vyuo vikuu Kaskazini mwa Uganda na zaidi ya vijana 6000 wameshahudhuria mafunzo ya kuimarisha amani na upatikanaji wa waki.

Kufuatia Shambulizi la Garissa, Jamii ya Wazungumzaji wa Kifaransa Waungana na Wakenya

Twitter users show support for Garissa victims via Arnaud Seroy on twitter

Watumiaji wa Twita waonesha mshikamano wao na wahanga wa tukio la Garisa kupitia Arnaud Seroy katika Twita

Kwa mujibu wa Kituo cha Kitaifa cha Kukabiliana na Majanga cha nchini Kenya (KRCS), mnamo Aprili 2, 2015, watu wasiopungua 147 waliuawa kwa kufyatuliwa risasi katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya. Kituo hicho pia kilitaarifu kuwa  watu 79 walijeruhiwa na wengine 587 walifanikiwa kutolewa kutoka katika eneo la tukio.

Mtuhumiwa mkubwa wa mauaji haya ya halaiki ni kikundi cha wanamgambo wa Al-Shabaab kilicho na maskani yake nchini Somalia kilichotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Maelezo kutoka kwa wahanga wa tukio hili zilichochea watu kuonesha mshikamano wao kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kote. Jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kifaransa, bado wakiwa na kumbukumbu ya shambulizi la Charlie Hebdo, walionesha mshikamano wao na wahanga wa shambulizi la Garissa kupitia mitandao ya kijamii katika kiungo habari #JesuisKenyan (kama taswira ya kiungo habari cha hashtag #JesuisCharlie). Hii ilikuwa ndio mada ya pili kwa mvuto kuliko nyingine yoyote katika Twita nchini Ufaransa mnamo Aprili 3.

Yafuatayo ni baadhi tu ya machapisho hayo:

Watu 147 wamepoteza maisha katika shambulizi la kutisha la kigaidi dhidi ya wanachuo vijana wa taifa la kesho. Tuoneshe mshikamano wetu#JesuisKenyan

Haitoshi kuzungumzia shambulio hili la kigaidi lililotokea katika chuo kikuu cha Kenya kwenye mitandao ya kijamii, watu 147 ni wachache?! Inatisha sana #JesuisKenyan

Timu ya Uokoaji ya Mexico Yaomba Michango Iende Kusaidia Nepal

Michango inahitajika mara moja kwa waokoaji 25 kwa njia ya paypal: donativos@brigada-rescate-topos.org CLABE Santander:01418092000709294 simu.5554160417 #ToposANepal (Topos to Nepal)

Kikosi cha Uokoaji Topos México Tlatelolco kimeanza kampeni ya kuomba michango ili kuweza kuungana na jitihada za uokoaji zinazoendelea baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 7.8  kuitikisa Nepal Jumamosi iliyopita, na kukatisha maisha ya watu zaidi ya 4,000 na wengine 7,000 wakijeruhiwa.

Kundi hili lilizaliwa wakati watu wanaojitolea kujitokeza kusaidia baada ya tetemeko lililoikumba Mexico mwaka 1985. Kundi hilo zamani lilikuwa likiratibiwa na asasi ya kiraia kwa zaidi ya miongo mitatu tangu mwezi Februari 1986, na kimesaidia jitihada za uokoaji kwenye majimbo ya Tabasco, Chiapas, Oaxaca, Jimbo la Mexico, Veracruz na Mexico City, yote yakiwa nchini Mexico na kwenye nchi nyinginezo duniani ikiwa ni pamoja na Haiti, Indonesia, El Salvador na Chile.

Topos México hawapokei malipo yoyote kwa kazi zao ka sababu kazi zao zinafanyika kwa mtindo wa kujitolea. Nyakati nyingi, serikali za mitaa au serikali kuu ya shirikisho nchini Mexico huwalipia gharama za usafiri na nchi wanazokwenda huwapatia visa na kuwawekea mazingira ya kufika kwenye eneo la tukio..

Video ifuatayo inaonesha mhutasari wa kazi za Topos.

Je, Blogu Zinaelekea Kutoweka?

Makala haya ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (#JumatatuYaBloguGlobalVoices) siku ya Machi 23, 2015.

Kwenye #LunesDeBlogsGV (#JumatatuyaBloguGlobalVoices), tunajitahidi kuzitunza blogu mithili ya “viumbe wanaoelekea kutoweka”, kwa kushughulikia changamto zinazokabili uwepo wa blogu kwenye ulimwengu wa kidijitali. Jitihada kama hizi zinamfanya mwanablogu Iván Lasso kuchambua mustakabali wa kublogu na matatizo yanayowakabili wanablogu leo, wakati ambao maudhui yao yanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupotea kufuatia wingi wa aina na ubora wa viwango vya taarifa zinazopatikana kwenye mtandao wa intaneti. Hali wanayoendelea kukumbana nayo wanablogu mtandao, Lasso anasema, inakaribiana na ile ya “Daudi na Goliathi”.

Lasso anazungumzia suala kubwa kwa wanablogu leo:

A raíz de la popularización de la web, de unos años para acá hay mucha más audiencia potencial disponible. Pero sospecho que gran parte de esa audiencia nunca podría ser tuya (tuya, mía… de blogs pequeños, vamos). Es audiencia que acude a la red en busca de simple entretenimiento y que si quiere información más “dura”, acude a los medios tradicionales que ahora ya están en la web.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuongezeka kwa matumizi makubwa ya Mtandao, kuna hadhira kubwa ya wasomaji inayofikika. Lakini nina wasiwasi kwamba hadhira hii inaweza isimsaidie mwanablogu. Sababu ni kwamba hii ni hadhira inayokuja mtandaoni kutafuta habari nyepesi za burudani na wanapohitaji taarifa ‘muhimu’, wanazitafuta kwenye vyombo vikuu vya habari ambavyo navyo vinapatikana mtandaoni.

Lasso anatoa ufumbuzi kwa changamoto hizi wanazokabiliana nazo wanablogu:

Hoy día, para que un blog independiente alcance un cierto grado de éxito (reconocimiento, reputación y visitas) debe convertirse en un rayo láser que apunte a aquello en lo que quiere destacar:
¿Quieres dar noticias? Tienes que darlas lo antes posible, más rápido que nadie.
¿Quieres hacer análisis u opinión? Tienes que profundizar más que nadie.
¿Quieres ser didáctico? Tienes que explicar mejor que nadie. Y también con más detalle que nadie.

Siku za leo, kwa blogu huru kuwa na mafanikio ya kiasi fulani (kutambuliwa, heshima, na hata kutembelewa), lazima ujifunze kujua wasomaji wanahitaji nini na ukizingatie:

  • Unataka kutoa habari kupitia blogu yako? Zitoe mapema kadri inavyowezekana, mapema kabla hazijaonekana kwingineko.
  • Unataka kufanya uchambuzi na kutoa maoni yako? Nenda ndani zaidi kuliko wengine.
  • Unataka kutoa elimu? Elezea mambo kwa ufasaha kuliko wengine. Na zungumzia masuala mahususi yanayowagusa watu.

Endelea kusoma makala ya Ivan Lasso hapa, na mfuatilie kwenye mtandao wa Twita.

 Hii ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (#JumatatuYaBloguGlobalVoices) mnamo Machi 23, 2015.

Magazeti Maarufu Iran Yataka Kusitishwa kwa Mashambulio ya Anga Nchini Yemen

Magazeti mawili yenye umaarufu mkubwa leo katika kurasa za mbele yalihanikizwa kwa habari za kushindwa kwa Saudi Arabia. Habari zili zimetokana na tangazo la Saudi Arabia la kusitisha mashambulizi ya anga dhidi ya Yemen mapema Jumanne hii. Kayhan, gazeti lililo na uhusiano na kiongozi mkuu wa Kidini, Ayatollah Khamenei, katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha picha ya kijana wa Yemen wa Kihouthi akiwa amekalia kitu ambacho kilionekana kama mabaki ya roketi yaliyotokana na mashambuli ya anga ya ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji wa Houthi. Kichwa cha habari kinasomeka, “Wapiganaji wa Yemen wa Ansar Hezbollah waidhalilisha Israel na Marekani.” Nchini Iran, Wahouthi wa Yemen kwa kawaida hujulikana kwa jina la Ansar Hezbollah”.

Kayhan news reacts on its Thursday April 23, 2015 frontpage to the end of Saudi airstrikes.

Gazeti la Kayhan likiwa na maoni kupitia ukurasa wake wa mbele wa tarehe 23 Aprili, 2015 kufuatia Saudi Arabia kutangaza kusitisha mashambulizi ya anga nchini yemen.

Vatan Emrooz, gazeti jingine lenye msimamo mkali lilikisimamia kidete chama cha ‘Peydari Front,’ ambacho ni chama cha kisiasa kilicho na uhusiano na walinzi wa kiuanamapinduzi na majeshi ya Basij katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha picha ya kutengenezwa iliyokuwa inamuonesha Mfalme wa Saudi Arabia akiwa ameanguka kwenye kifusi cha jengo lililoharibiwa na ikiwa na maneno, “Pumzi ya Saudi imekufa!”. Unaposema pumzi ya mtu imekufa, huu ni msemo maarufu wa kiajemi unaoonesha kushindwa kwa mtu. Maelezo ya chini yanasema, “Kampeni ya ‘Kimbunga Yakinifu’ yamalizika mara baada ya siku 27 za uhalifu na mauaji ya vichanga na bila ya kufikia hata moja ya matazamio yake”

Vatan-e Emrooz

Gazeti la Vatan Emrooz likiwa na maoni yake ukurasa wake wa mbele wa tarehe 23 Aprili, 2015 kufuatia Saudi Arabia kutangaza kusitisha mashambulizi ya anga nchini yemen.

Fuatilia habari za Yemen katika Global Voice hapa.

Angalizo Kutoka kwa Mwandishi: Huu siyo uchambuzi kamili wa vyombo vya habari vya nchini Iran. Kuvitazama vyanzo vya habari vilivyo na msimamo mkali kama vile Kayhan au Vatan Emrooz kunafanana na kufuatilia Fox News nchini Marekani.

Nini Tofauti ya Kusoma na Kuelimika?

Pedro Muller anatafakari kuhusu matatizo yanayoukabili mfumo wa shule, taasisi anayosema ilimaanisha mazingira tofauti ya kihistoria. Kwa kusema hayo, anabainisha umuhimu wa dhana hizi mbili zinazofanana lakini zikimaanisha nyakati mbili tofauti: “Kusoma” na “kuelimika”:

El educar se va más allá de memorizarse un par de nombres y olvidarlos al siguiente día, consiste en aprender tener la curiosidad de preguntarse qué hay detrás de lo obvio, es adquirir habilidades, ejercitar tu pensamiento lateral un pensamiento divergente o como muchos dicen “fuera de la caja”, educarse también es crear y hacer convertir nada en algo, innovar.

Nosotros aprendemos mejor en grupo es parte de nuestra naturaleza, discutir, pensar y reflexionar sobre un tema en específico sacar conclusiones, como muchos dicen la mejor manera de educarse es aprender.

TKuelimika kunaenda mbali zaidi ya kukariri majina kadhaa na kuyasahau siku inayofuata. Kuelimika ni kuwa na udadisi na kuhoji yale yaliyofichika nyuma ya kinachoonekana kuwa mazoea, ni kuwa na ujuzi, kuutumia uwezo wa kufikiri tofauti, fikra mbadala tunazoweza kuziita “kufikiri nje ya boksi”. Kuelimika ni kujifunza kuwa mbunifu na mgunduzi.

Tunajifunza vizuri kwenye makundi; ni sehemu ya asili yetu kujadili, kufikiri na kutafakari mada mahususi na kufanya mahitimisho. Inasemekana kwamba namna nzuri ya kuelimika ni kujifunza.

Muller anawakaribisha wasomaji wake kutazama video ifuatayo iliyo katika Kiingereza, ambako Logan LaPlante anazungumzia dhana ya “kuidua elimu” au “dukuaelimu”, anayosema ni mchakato wa kujifunza kwa kikundi, kwa mtindo wa kujaribu na, zaidi, umuhimu wa ubunifu.

Endelea kusoma makala ya Muller hapa, au mfuatilie kwenye mtandao wa Twita.

Makala haya ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (JUmatatu ya blogu ya GV) mnamo Machi 23, 2015.

Mwizi Akamatwa, Aomba Msamaha na Kusamehewa

Captuira de pantalla de video en YouTube del usuario KDNA15TV.

Picha ya video kwenye mtandao wa YouTube iliyowekwa na mtumiaji KDNA15TV.

Labda alidhani ingekuwa vyepesi kuiba shampoo mali ya mmiliki wa duka nchini Peru, lakini mambo yalimwendea mrama mwizi huyu.

Mtu mmoja akiwa ameongozana na mwenzake waliingia kwenye duka lililoko kwenye jiji la Huancayo nchini Peru, wakisema walikuwa wanataka kununua pombe, na mmiliki alipokuwa amepumbazwa kidogo, jamaa walibeba boksi la shampoo. Mmiliki aligundua mchezo wao na kuwaarifu walinzi. Ili kuzuia tukio hilo lisifike mbali, mmoja wa wezi hao alipiga magoti na kuomba msamaha. Mmiliki wa duka, aliyekuwa mwanamke, aliguswa na kitendo hicho na akaamua kuachana na mpango wa kuwachukulia hatua. Mwenzake na mwizi huyo aliyeomba msamaha naye alinufaika na msamaha huo, ingawa hakuwa ameomba msamaha.

Jamaa huyo alidai hatarudia tena kufanya kitendo kama hicho.

Blogu ya Noticias Huancayo Perú ilisimulia mhutasari wa tukio hilo:

Se arrodilló y pidió perdón a la anciana manifestando que era la última vez que robaría. La agraviada […] al aceptar sus súplicas del ladrón negó en denunciar el hecho.

Lipiga mgoti na kumwomba mwanamke wa umri wa makamo amsamehe, akimsihi kwamba hiyo ndiyo itakuwa mara yake ya mwisho kuiba. Mama huyo […] kwa kukubali ombi la mwizi wake, aliamua kuachana na mpango wa kutoa taarifa ya tukio hilo.

Mtumiaji KDNA15TV aliweka video zinazozungumzia tukio hilo:

Mwizi apata msamaha baada ya kupiga magoti kuomba msamaha kwa kuiba boksi la shampoo. Alikuwa na rafiki yake waliyekuwa wameambatana…

Upigaji Kura Unaendelea Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2015

Sehemu ya kupiga kura kwenye Tuzo za Blogu Nchini Kenya inaendelea mpaka Aprili 30, 2015:

Tuzo za Blogu Nchini Kenya hutafuta kuwatuza wanablogu wanaoandika mara kwa mara, wanaoandika madhui yanayosaidia, na wenye ubunifu na ugunduzi. Tuzo hizi ni jitihada za Chama cha Wanablogu Kenya (BAKE) katika kukuza ubora wa maudhui yanayochapishwa mtandaoni. Waandaaji wa tuzo hizi ni wanachama wa Chama cha Wanablogu Kenya (BAKE), jumuia inayowakilisha kikundi cha wazalishaji wa maudhui mtandaoni kinachotaka kukuza uzalishaji wa maudhui na kuboresha kiwnago cha maudhui yanayowekwa mtandaoni.

Jiandae kwa Mkutano wa MozFest Afrika Mashariki 2015

MozFestEA ni tukio litakalofanyika kuanzia Julai 17 – 19, 2015 kwenye Chuo Kikuu cha Victoria, Kampala, Uganda likiwa na maudhui makuu, “Kutafuta Majibu ya Changamoto za Afrika, kwa pamoja mtandaoni”:

MozFest Afrika Mashariki ni tukio la kila mwaka linalowaleta pamoja wataalam wa elmu, wabunifu, wasomi na mafundi wa Afrika Mashariki kujaribu kujadili namna ya kujenga mtandao kwa pamoja kwa kuweka msingi wa ukuaji wa mtandao wa intaneti na teknolojia ya habari barani Afrika.

Tukio hili limeenea Afrika nzima kusaidia kukabili changamoto za teknolojia zinazolikabili bara la Afrika kwa kutumia mifumo mizuri ya ushirikiano.