Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Februari, 2015

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Februari, 2015

Kampeni ya Facebook Yampa Mwandishi wa Iran Masih Alinejad Tuzo ya Haki za Wanawake

 

The cover photo from Masih Alinejad's Facebook page "My Stealthy Freedom"

Picha kuu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Masih Alinejad uitwao “My Stealthy Freedom”

Mwandishi raia wa Iran anayeishi London Masih Alinejad ameshinda Tuzo ya Haki za Wanawake kwa mwaka 2015 kwenye Mkutano wa Geneva wa Haki za Binadamu na Demokrasia kutokana na kampeni yake kwenye mtandao wa Facebook iitwayo “My Stealthy Freedom“juma lililopita. Ukurasa huo unawakaribisha wanawake wa ki-Iran kuweka picha zao humo wakiwa wamevalia Hijab, kupinga sheria ya ki-Islam ya Iran inayolazimisha mavazi hayo. Ukurasa huo wenye wafuasi 750, 000, umeonekana kuwa na sura ya harakati za mtandaoni kwa ajili ya wanawake.

Hapa chini kuna video iliyowekwa kwenye ukurasa wake kuonesha hotuba yake ya kupokea tuzo hiyo kwenye Mkutano huo siku ya Jumanne iliyopita: 

Mapendekezo Yanapokelewa kwa Ajili ya Mwezi wa Historia Nyeupe 2015

Likiwa limeandaliwa na blogu ya Africa is a Country [Afrika ni Nchi], tukio la Mwezi wa Historia Nyeupe linajongea mwezi ujao:

Mwezi Machi mwaka jana ndio ulikuwa mwezi wa uzinduzi wa zoezi hilo kwenye blogu hii, na bila kupuliza sana mavuvuzela yetu kw akujisifu, ule kwa hakika ulikuwa ni mwezi mzuri. Tunaahidi kufanya kama tulivyofanya kipindi hicho.

Tutakuwa na mambo kama ngozi ya Kathleen Bomani kutoka Human Skin, Filadefia ya miaka ya 1880 na tutakuwa na mambo mengi, kama vile utawala wa kikatili wa Uingereza kwenye miaka ya 1950 nchini Kenya na hata wakati ule serikali ya Afrika Kusini ilipotuma ujumbe kwenda Marekani kutafuta kujua namna “kuweka nafasi za mahotelini/ndege” kunavyofanyika.

Kama ungependa kushiriki, unatakiwa:

Wasiliana nasi kwa editorial [at] africasacountry [dot] com na tufahamishe kile unachotaka tukiandikie. Angalia kile tulichokiandika mwaka jana kupata wazo la kile tunachokitafuta.

Wachoraji 10 wa Kiafrika wa Vitabu vya Watoto Unaopaswa Kuwajua

Jennifer Sefa-Boakye anasaili orodha ya washindani 10 bora zaidi wa tuzo ya Golden Baobab kwa Wachoraji wa Kiafrika:

Mwaka jana shirika la Afrika lenye makazi yake nchini Ghana, Golden Baobab, liliwatambulisha wachoraji kadhaa wenye vipaji, ambao kazi zao ni kama vile masimulizi ya Ashanti yaliyosukwa kutoka miji ya Moroko na hata wapiga rangi wa ki-Afrika katika vyumba vya kunyolea jijini Durban. Uzinduzi wa tuzo hizo za Glolden Baobab kwa wachoraji wa ki-Afrika ulifanyika mwezi Novemba, na ni moja ya tuzo sita zinazotambua waandishi na wachoraji bora wa ki-Afrika wa vitabu vya watoto wa mwaka.

Vijana wa Naija Wacharuka Kufuatia Shambulizi la Boko Haram huko Bosso na Diffa

Niger youth

Vijana huko Niger – CC-BY-2.0

Kwa mara ya kwanza, Boko Haram kimetekeleza shambulio kwenye mpaka na Naija na vijana wa ki-Naija hakuweza kuvumilia.

Boko Haram walishambulia Bosso na Diffa, miji miwili iliyo kusini mashariki mwa Naija kwenye mpaka wa nchi hiyo na Naijeria lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya Chad na Naija. Boko Haram imepoteza zaidi ya wnaamgambo 100 kwenye mapigano hayo lakini mtu aliyejitolea mhanga alijilipua mjini masaa machache baadae, na kuua watu wasiopungua watano. Kijana mmoja wa Naija alisukumwa kujibu mapigo. Wanafunzi wa shule za sekondari jijini Niamey (mji mkuu wa Naija) walikusanyika pamoja na kulaani shambulio hilo nchini mwao, na kwa kutumia lugha ya ki-Hausa, waliunga mkono vikosi vyao vinavyopambana mpakani:

Ufisadi Uliofanywa na Makampuni Makubwa Katika Kupambana na Ebola Nchini Sierra Leone

Makampuni matano nchini Sierra Leone yanasemekana kutumia fedha zilizokusudiwa kupambana na Ebola kwa njia za kifisadi:

Haya hapa makampuni matano yaliyokuwa yameingia mikataba mikubwa ya kusambaza vifaa na kutoa huduma katika kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone kama yalivyoorodheshwa kwenye Taarifa ya Ukaguzi ya Fedha za Kupambana na Ebola kwa kipindi cha kuanzia Mei – Oktoba 2014. Mikataba ifuatayo hakukidhi sheria na sera za manunuzi za nchi na nyaraka za kuthibitisha namna [makampuni haya] yalivyoshinda tenda hizo hazionekani, na hakuna anayeweza kutoa maelezo. Hali hii inafanya uwepo uwezekano wa kutokea vitendo vya kifisadi, upotevu na hata matumizi mabaya ya fedha na hivyo kuzorotesha uwezo wa taifa hilo kupambana na janga hilo.

2015 Mwaka wa Kufanyika Chaguzi Huru na Haki Barani Afrika

Wekesa Sylvanus anataraji kwamba 2015 utakuwa mwaka wa chaguzi huru na haki barani Afrika:
https://wekesasylvanus.wordpress.com/2015/02/18/will-2015-be-a-year-of-free-and-fair-elections-in-africa/

Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika, ushindani nyakati za uchaguzi umekuwa suala la kufa na kupona kwenye nchi nyingi za ki-Afrika. Chaguzi barani Afrika ni suala lenye hatari zake na katika nyakati za hivi karibuni, chaguzi zimekuwa kichocheo cha migogoro. Kenya na Ivory Coast ni mifano mizuri ya namna kutokusekana kwa utaratibu mzuri wa uchaguzi kunavyoweza kuiingiza nchi kwenye machafuko. Karibu nusu karne baada ya uhuru, nchi nyingi za ki-Afrika hazijaweza kuwa na taratibu sahihi kufanya chaguzi zilizo huru na haki. Mwaka 2015 utashuhudia nchi nyingi zikiingia kwenye uchaguzi. Chaguzi za Rais na/au wabunge zitafanyika kwenye nchi za Naijeria, Sudan, Ethiopia, Burundi, Tanzania, Zambia, Togo, Ivory Coast, Mauritius, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Burkina Faso, Naija, Guinea, Chadi, na Misri na labda Sudani Kusini kutegemeana na makubaliano ya amani yanayotarajiwa kuwekewa saini. Nyingi za nchi hizi zimepambana kutaasisisha utendaji wa kidemokrasia katka siku za hivi karibuni. Mwaka 2015 unaleta fursa kubwa kwa nchi hizi kuionesha dunia kwamba sasa zimekomaa kidemokrasia.

Filamu: ‘Sanaa ya Ama Ata Aidoo’

The Art of Ama Ata Aidoo ni filamu iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu Yaba Badoe:

The Art of Ama Ata Aidoo, inasaili mchango wa kisanii wa mmoja wa waandishi wanawake mashuhuri barani Afrika, anayeongoza kizazi hiki kwa kipaji kipya cha pekee.
Dokumentari hii inasaili safari ya ubunifu ya Ama Ata Aidoo ya miongo saba kuanzia enzi za Ghana inayotawaliwa na wakoloni, kupitia nyakati za uhuru, mpaka Afrika ya leo ambako ubunifu wa vipaji vya wanawake hauonekani kiwepesi.

The Art of Ama Ata Aidoo (Teaser) from Big Heart Media kwenye mtandao wa Vimeo.

Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini

Northern Cameroon border, where Boko Haram operates

Mpaka wa Cameroon Kaskazini, ambako where Boko Haram hufanya kazi zao

Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon, baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika kufa na Wizara ya Ulinzi. Shirika la Haki za Binadamu nchini humo linaamini kwamba karibu watu 370 wameuawa. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kwamba miili kadhaa ilipatikana kwenye mitaa ikiwa imechinjwa makoromeo.  Mji wa Fotokol umekuwa ukikabiliwa na vita kati ya Boko Haram na majeshi ya Cameroon na Chadi kwa siku za hivi karibuni: Machi 2014, Agosti 2014 na Oktoba 2014. Mwanablogu wa Cameroon Noelle Lafortune anaripoti kwamba shambulio hilo linaonesha kwamba Boko Haram inaweza kuwa inaanza kupoteza nguvu katika eneo hilo:

Au front, la peur est en train de changer de camp. L'entrée en scène de l'armée tchadienne en appui aux armées camerounaise et nigériane semble être décisive, eu égard à la panique qui s'est emparée de Boko Haram.  La puissance de feu des forces coalisées a mis en déroute Shekau et sa bande. 

Kwenye mstari wa mbele, wasiwasi unakumba pande zote. Kujitokeza kwa jeshi la Chadi uunganisha nguvu na majeshi ya Camerron na Naijeria kuonekana kuwa na maamuzi sasa, imeleta hali ya tahayaruki kwa kikundi hicho cha kigaidi cha Boko Haram. Mapigano ya majeshi hayo ya pamoja yalimng'oa Shekau (kiongozi wa Boko Haram) na genge lake.