· Agosti, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Agosti, 2013

Iran: Mwanablogu Aliyefungwa Jela Afanya Mgomo wa Kutokula

Hossein Ronaghi Malki mwanablogu anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela alianza mgomo wake wa kutokula kuanzia wiki iliyopita. Kwenye mtandao wa Facebook kampeni imeanzishwa yenye lengo la kummwuunga mkono.

PICHA: Makanisa Yanalia Nchini Misri

Mtetezi wa haki za wanawake nchini Misri Dalia Aziada aliposti twiti hii  baada ya makanisa kadhaa ya wakristo kuteketezwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kufuatia operesheni ya kikatili  iliyofanywa na jeshi Agosti 14 2013, iliyokusudia kuwatoa wafuasi wa chama cha Udugu wa Ki-islamu kutoka makao ya makambi katika mji mkuu wa Cairo, ambapo wamekuwa wakidai kurejeshwa madarakani kwa rais Morsi kwa wiki kadhaa.

Operesheni hiyo ya kuwaondoa wafuasi hao ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 638 kwa mujibu wa serikali ya Misri. Msemaji wa chama cha Udugu wa ki-Islamu amesema watu 2,000 waliuawa katika “mauaji hayo ya halaiki”.

Makumi kadhaa waliuawa mnamo Agosti 16, wakati wafuasi wa Udugu wa ki-Islamu walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama katika “Siku ya hasira.”

 Soma zaidi katika Habari zetu MaalumUmwagaji wa damu nchini Misri.

 

China: Kisasi au Haki?

Kashfa ya ngono ya hivi majuzi inayowahusisha majaji wawili maarufu wa Shanghai iliwekwa hadharani na mfanyabiashara Ni Peiguo anayeamini kuwa mmoja wa majaji hakutoa hukumu ya haki katika kesi ya kampuni anayohusika nayo. Alichukua uamuzi wa kulipiza kisasi kufuatia hasara ya fedha kwa kumfuatilia hakimu kwa mwaka na hatimaye kufichua kashfa yake ya ngono. Mtandao wa China Beat ulisaili maoni ya raia wa mtandaoni juu ya kisasi cha Bw. Ni, ambayo ina ufanisi zaidi kuliko kujaribu kukata rufaa dhidi ya kesi.

Wanaharakati wa Hongkong Walaani Mauaji ya Halaiki Mjini Cairo

Hong Kong activists from League of Social Democrats and Socialist Action protested outside Egypt Consulate and condemned the military over Cairo Massacre on August 14, 2013. Photo from inmediahk.net.

Leo, kundi la wanaharakati wa Hong Kong kutoka Chama cha Demokrasia na Ujamaa (LSDS) waliandamana nje ya ubalozi wa Misri na kulilaani jeshi kwa mauaji ya halaiki mnamo Agosti 14 mjini Cairo. Picha kutoka kwa inmediahk.net.

Makanisa Yashambuliwa Nchini Misri

David Degner aweka picha kutoka makanisa yaliyoshambuliwa na kuchomwa katika sehemu iitwayo Mallawi, Minya, Misri ya Juu hapa.

Anaandika:

Siku ya Ijumaa makanisa mawili katika kijiji cha Mallawi, jimbo la Minya, yalishambuliwa na kuchomwa moto.

Baada ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wa Morsy  ambapo zaidi ya watu 600 walifariki, wafuasi wa Morsy walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa wakavamia na kuchoma makanisa mawili, na baadhi ya maduka yanayomilikiwa na wakristo katika kijiji cha Mallawi.

Watu walikuwa katika makundi pia walishambulia na kuiba vitu kwenye chumba cha makumbusho kijijini humo, na benki, maduka na makanisa mengine 10 jimboni humo.

Anaweka video hii, inayoonyesha Kanisa la Kiinjili, kijijini humo likiwaka moto:

Serikali ya Uzbeki Yatafuta Namna ya Kudhibiti Wanablogu

Serikali nchini Uzbekistan inatafuta namna ya kutumia hatua kali za kudhibiti wanablogu wa nchi hiyo. Alisher Abdugofurov kwenye Registan.net anajadili sababu ya kutokea hali hii katika jamii ambayo haina wanablogu wengi wa kuanzia zoezi hilo.

Iran: Waziri Mpya wa Kigeni Yupo Kwenye Mtandao wa Facebook

Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini  Iran lakini ndio uliotumiwa na wagombea wote wa urais katika uchaguzi uliopita.