Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Julai, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Julai, 2014

Honduras Yazalisha Ajira kwa Kuhamasisha Shughuli za Jamii

Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandes amezindua mpango wa “Desarrollemos Honduras” (Tuiendeleze Honduras), na maofisa na jamii walishiriki katika tukio hilo. Hernandes alieleza kwamba kama nyumba imebomoka au sakafu yake ni ya udongo, matengenezo lazima yafanyike kwa kutumia sementi; au kuweka vipaumbele kulingana na mahitaji ya familia, na:

Cambiar los fogones tradicionales por los ecofogones. Yo sé que en muchos lugares, tal vez no sea el caso de las casas aquí, es triste preguntarle a la gente cuánto paga por la leña y la gente no sabe, hay que explicarle (…) A veces a la gente se sale más cara la leña que la comida.

Kununua majiko ya kisasa badala ya mafiga za kizamani. Ninajua kwamba kwenye maeneo mengi, huenda sio hapa, inahuzunisha kuuliza kiasi gani cha pesa watu hutumia kununua kuni na hawajui, sisi ndio twapaswa kuwaeleza (…). Mara nyingine, watu hulipa fedha nyingi kununua kuni kuliko wanavyogharamia chakula.

Watumiaji wa mtandao wa Twita waliweka picha na maoni yao:

TUIENDELEZE HONDURAS ilianza leo kwenye jamii ya El Reparto. Mpango huo wa kuendeleza majirani utatengeneza nafasi 150 za vijana wanaotoka kwenye jamii hizo.

Hii kwa kweli inafaa, sote tushirikiane ili mambo yawe bora zaidi. Tuiendeleze Honduras.

Highway Africa 2014 Yasogeza Mbele Tarehe ya Mwisho ya Kujiandikisha

Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha kwa ajili ya Mkutano wa 18 wa mwaka wa Highway Africaimesogezwa mbele mpaka Ijumaa, Agosti 08 2014:

Kutokana na kuongezeka kwa shauku ya watu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa 18 wa Highway Africa, tarehe ya mwisho ya kujiandikisha imesogezwa mbele mpaka Ijumaa, 08 Agosti 2014.

Mkutano huo mkubwa wa mwaka wa Waandishi wa Kiafrika unafanyika kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini, kuanzia Septemba 7 – 8 2014.

Mkutano huo ukiwa na kauli mbiu, “Mitandao ya Kijamii – kutoka pembezoni mpaka kwenye vyombo vikuu”, utakuwa ukichambua namna mitandao ya kijamii ilivyoathiri maeneo yote ya maisha yetu katka kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Hotuba ya Ushindi ya Rais Mteule wa Indonesia

Rais mteule wa Indonesia Joko Widodo or Jokowi alitoa hotuba ya ushindi akitambua moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wananchi:

Uchaguzi huu wa rais umechochea mtazamo mpya chanya kwetu, na kwa taifa letu kwa ujumla. Uhuru wa watu na uwajibikaji wa kisiasa vinashamiri katika nyoyo za kizazi kipya. Moyo wa kujitolea uliopotea siku nyingi umerejea tena kwa ari mpya.

Na katika kutangaza “kushiriki katika shughuli za kujitolea”, Jokowi aliwaomba watumiaji wa Facebook kupiga kura na kuchagua mawaziri 34 ambao wanadhani anapaswa kuwaingiza katika Baraza la Mawaziri la serikali yake.

Picha za Mabaki ya Ndege ya Shirika la Algeria AH5017 Nchini Mali Yaonyesha Ghasia, Kuanguka kwa Ghafla

PICHA ZA KWANZA za ndege ya AH5017 ya Shirika la Ndege la Algeria ikianguka, kupitia @AirLiveNet

Kipande cha kwanza cha video cha ajali ya ndege sasa kinapatikana. Tunamshukuru mwanajeshi wa Burkina Faso aliyekuwa eneo la tukio la ajali karibu na Gossi, Mashariki mwa Mali. Hakuna mtu aliyeokoka katika abiria 118 waliokuwa kwenye ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na raia 50 wa Ufaransa. Tovuti la Aljeria Algérie Focus imeripoti kwa Kifaransa kwamba:

Cette vidéo montre des débris éparpillés et broyés. La zone sablonneuse a été noircie par le crash. Sur cette vidéo, il est pratiquement impossible de repérer les pièces maîtresses de l’avion au milieu des débris.

Video inaonyesha vipande vya ndege hiyo vikiwa vimetawanyika. Udongo wa eneo hilo uligeuka kuwa mweusi. Katika video hiyo, si rahisi kutambua sehemu yoyote ya ndege hiyo kwenye mabaki hayo.

Tafakuri Baada ya Kombe la Dunia la FIFA 2014 Nchini Brazili

14260796868_09f22f412d_c

Picha kutoka kwenye mtandao wa Flickr, yenye leseni ya CC.

Mwanafunzi wa Mexico Álvaro anablogu kuhusu hisia na maoni yake kuhusu Kombe la Dunia la FIFA 2014 nchini Brazil. Anatafakari kuhusu kufanya vibaya kwa timu za mataifa ya Mexico na Brazili, lakini anasaili kile anachokiita kushindwa kwa mkakati wa Rais wa Brazili Dilma Rouseff.

Días antes del comienzo del mundial, Dilma se imaginaba este lunes 14 de Julio como el día en que ganaría anticipadamente las elecciones presidenciales de octubre, un Brasil campeón en su tierra hubiera sido suficiente para sofocar las protestas civiles que se han alzado en contra de su gobierno, o al menos hubiera logrado distraerlas por un rato.[…] Sin embargo, es evidente que el plan no salió según lo esperado, sino todo lo contrario; de manera similar a lo ocurrido en Sochi, Rusia para las Olimpiadas de Invierno, el enfoque mundial sobre Brasil solo sirvió para exponer los graves problemas que enfrenta el país en todo ámbito. No hubo escasez de reportes de la prensa internacional sobre el mal estado de las calles, las acomodaciones, la gente y hasta los estadios, mismos que se derrumbaron o que ni siquiera pudieron terminarse antes del evento.

Siku chache kabla Kombe la Dunia halijaanza< Dilma alikuwa akidhani kwamba Jumatatu hii ya Julai 14 ingekuwa siku ambayo angeshinda kabla hata uchaguzi wa Rais haujafanyika Oktoba, kwamba kwa Brazil kuchukua ubingwa kwenye ardhi yao ingetosha kutulixa maandamano ya kiraia dhidi ya utawala wake, au basi hata angalau ingetosha kuwapotezea malengo kwa muda [...] Hata hivyo, ni wazi kwamba mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa, na yakawa kinyume chake; kama ilivyotokea Sochi, Urusi wakati wa Mashindano ya Olympiki ya majira ya maridi. Yaliyotokea Brazili yalianika matatizo makubwa ambayo nchi hiyo inakabiliana nayo. Kulikuwa na taarifa nyingi za vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu barabara mbaya, malazi yasiyoridhisha, watu na hata viwanja ambavyo vilianguka au hata havikukaika kabla mashindano hayajaanza.

Unaweza kumfuatlia Álvaro kwenye akaunti yake ya Twita.

 Makala haya ni sehemu ya kumi na moja ya #LunesDeBlogsGV,(Jumatatu ya blogu kwenye GV) siku ya Julai 14, 2014. 

Dondoo 13 za Kulinda Taarifa zako Kwenye Kompyuta Zinazotumiwa na Watu Wengi

ordenadores-publicos-300x234

Picha kutoka blogu ya profesoradeinformatica.com, imetumiwa kwa ruhusa.

Kama uko mbioni kwenda kwenye mapumziko na unafikiri kuchukua kompyuta yako na kuiunganisha na mtandao wa intaneti wa Siwaya (Wi-Fi) au kutumia kompyuta ambazo zinapatikana kwenye hoteli au kwenye eneo lolote la umma, unahitaji kusoma makala hii yenye dondoo 13 za kulinda taarifa zako, kama ilivyochapishwa na Andrea kwenye blogu yake:

¿Conoces los riegos de utilizar ordenadores públicos?

Desconoces el “estado de salud” de estos ordenadores, es decir estos pueden tener virus o programas maliciosos instalados para robar tu información (malwares). Entonces si no quieres que el estrés post-vacacional sea más agudo por problemas con tu información, lee con atención.

Unajua hatari ya kutumia kompyuta za umma?

Unapuuza ‘hali ya usalama wa kiafya’ wa kompyuta, na zinaweza kuwa na virusi au hata programu maalumu za kuiba taarifa zako. Kwa hiyo kama kutaki kuja kuchanganyikiwa baada ya kumaliza likizo yako na unataka kuwa makini zaidi na taarifa zako, soma kwa makini.

Hakuna wasiwasi kuhusu suala hili, sasa, namba 13 itakuwa ndiyo namba ya bahati zaidi.

Makala hii ilikuwa sehemu yetu ya saba ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV) ya tarehe 16 Juni, 2014. 

Je, Ujumbe wa Shirika la Ndege la Singapore Baada ya Ndege MH17 Kuanguka Haukuwa wa Kiugwana??

A Singapore Airlines flight on March 29, 2014. Photo by Flickr user Aero Icarus. CC BY-NC-SA 2.0

Ndege ya Shirika la Ndege la Singapore Machi 29, 2014. Picha na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Aero Icarus. CC BY-NC-SA 2.0

Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita:

Wateja wanaweza kuendelea kufahamu kuwa ndege za Shirika la Ndege la Singapore hazitumii anga la Ukraine

Watumiaji wengi wa mtandao walililaumu shirika hilo la ndege kwa kutokuwa na uungwana. Sophie Chang alitoa maoni kwenye mtandao wa Facebook kwamba “namna nzuri kwa shirika la ndege kufanya ni kutoa pole kwanza.” Lakini Stephen Chapman anaamini kwamba kauli hiyo “ilikusudia kuleta utulivu kwa maana pana.” Ryan Ik alikubaliana na ufafanuzi huo lakini alijisikia “kukosa maneno ya kutoa pole, habari hizo hazikuwa za kiungwana.”

Iwe ni kweli ama la kwamba ujumbe huo ulikosa uungwana, lakini tangu uwekwe mtandaoni umekuwa ukisambaa kwa kasi ndani ya masaa machache.

Madege ya Kijeshi ya ki-Palestina Yaruka kwenye Anga la Israel

Brigedi ya Palestina ya Al Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, lilionyesha miundo mitatu ya madege ya kijeshi leo, ikisema kuwa yalirushwa kwenye anga la Israel.

Mwandishi Dima Khatib anatwiti:

Brigedi ya Al Qassam inasema walitengeneza aina tatu za madege ya kijeshi ya Ababil: A1A, A1B, A1C picha @QudsN ya A1B wakati wa zoezi hilo la kijeshi

Madege hayo, yaliyotengenezwa Palestina, yanaitwa Ababil – jina la ndege waliotajwa kwenye Quran tukufu, walioilinda Mecca wakati wa vita na Yemen mwaka 571.

Mwanablogu wa Gaza Jehan Alfarra aliandika:

Nimeshangazwa na matumizi ya madege ya kijeshi yanayofanywa na Mamlaka ya Palestina kwenye ukanda wa Gaza. Tuko kwenye hatari

Ombi kwa Papa Francis Kuchukua Hatua Kupinga Madikteta wa Afrika

Abdoulaye Bah, mchangiaji wa Global Voices na mwanablogu wa Konakry Express ameanzisha ombi la mtandaoni kumwomba Papa Francis kuchukua hatua dhidi ya madikteta wa Afrika. Bah, ambaye aliwahi kuandika namna anavyokubaliana na baadhi ya misimamo ya kisiasa ya Papa, anapinga sifa zilizotolewa na Papa kwa viongozi watano wa Afrika kwa kuwakaribisha jijini Vatican. Ombi hilo linaomba kutokewa kwa adhabu kwa madikteta kama ilivyosemwa na wanachama wa Mafia wakati Papa Francis alipotembelea Calabria.

Papa Mtakatifu hivi karibuni alimpokea Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Eduardo dos Santos wa Angola, Rais Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta, Rais Paul Biya wa Kameruni, na Rais Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo. Marais hawa watano walivunja rekodi ya dunia kwa kubaki madarakani kwa muda mrefu. Kwa kufanya hivi, wamejenga himaya zinazovuna raslimali za nchi, kuua watu wasio na hatia, kubaka wanawake, kutesa wapinzani na watetezi wa haki za binadamu. Himaya hizi zinafisidi taasisi, zinaharibu matumaini ya watu wao kwa kuharibu uchaguzi, na kugawa watu wao kwa kutengeneza chuki na kusababisha harakati za kuwapinga.

Kuhusu Kuwa Kijana, Mweusi na Mgeni nchini Afrika Kusini

Leila Dee Dougan anaweka video ya muziki inayotoka kwenye toleo la hivi karibuni la msanii wa Afrika Kusini Umlilo:

Umlilo (ambaye hapo awali aliandikwa kwenye tovuti ya Africa is a Country) anaendelea kupunguza mipaka ya kijamii, akivunja vunja mila zinazohusu masuala ya jinsia na mapenzi kwa kutumia albamu yake ya hivi karibuni iliyotoka mwezi Julai 2014. Tazama video yake ya muziki na sikiza mawazo yake kuhusu tamaduni hizo, yeye akiwa mgeni wa nchi hiyo na namna muziki ulivyofanyika kuwa uhuru wake.

Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17

Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” Teknolojia ya Twita ya @RuGovEdits, ambayo bila kuongozwa kufuatilia uhariri wowote unaofanywa kwenye kurasa za Wikipedia kupitia alama za utambulisho wa kompyuta za serikali ya Urusi, ilibaini majaribio saba tofauti yaliyofanywa na kompyuta za “mashushushu” wa FSO asubuhi hii kuhakikisha kuwa neno “waasi” linabaki kwenye kumbukumbu. JItihada hizo zilikwama. Wahariri wa Kamusi Elezo ya Wikipedia kwa Kijerumani walirudisha maandishi ya awali yaliyokuwepo kwenye makala hiyo, kila mara.

Uhariri wa Kamusi elezo ya Wikipedia Kijerumani kuhusu MH17 kama unavyoletwa kwako na serikali ya Urusi.

Sababu za Kusafiri Mara Moja Moja

Equipaje

Picha ya mtumiaji wa mtandao wa Flickr larshuj (CC BY 2.0).

Kwenye blogu yake iitwayo Historias de una mujer lobo (Hadithi ya mbwamwitu wa kike), Natalia Cartolini anatafakari kuhusu sababu za kwa nini kusafiri kunaweza kuwa na faida kama, kwa maoni yake, “kutembelea maeneo mapya au kukutana na watu wapya wenye mtazamo mwingine ni muhimu wakati wote. Haijalishi kama unatoka kutembea ndani ya mji unamoishi au kwenye maeneo yanayouzunguka mji, muhimu ni kufungua macho yako ili uweze kuona mtazamo mpya wa maisha. Fanya jambo tofauti. […] Kadri unavyozidi kwenda mbali na kile ulichozoea, ndivyo unavyozidi kujitambua, kwa sababu unatambua kwamba wewe ndiye uliyehitaji kuendelea kuishi.”

Anamalizia tafakuri yake kwa kusema:

Entonces, imagínate escuchar tu música instrumental favorita mientras caminas por la calle. Todo se transforma. Ahora tú eres el protagonista.
Por un momento eres un Gatsby, en otras, un vaquero o un montañista. ¿Quién detiene a la imaginación? Sólo tú. Sal de tu sitio y aprovecha lo que tienes alrededor tuyo. Porque es tuyo.

Kwa hiyo, fikiria unasikiza muziki uupendao wa ala unavyotembelea mtaani. Kila kitu kinabadilika. Na inatokea sasa unakuwa ndiye mhusika mkuu. Kwa muda kidogo, unajifanya Gatsbu, wakati mwingine muuza maziwa na wakati mwingine mpanda mlima. Nani anaweza kukufanya uache kufikiri zaidi? Ni wewe. Toka unakoishi na katembelee vile vilivyo pembeni mwako. Kwa sababu unavimiliki vyote.

PICHA: Wapelestina Wanatufundisha Namna ya Kuishi

Mpalestina Sayel anatwiti kwa wafuasi wake 1,800 kwenye mtandao wa Twita picha ifuatayo ya wakazi wa Gaza wakipanda maua kwenye maganda ya silaha za Israeli. Anasema:

Wapalestina wa Gaza wanapanda maua kwenye maganda ya silaha yanaokotwa kwenye nyumba zao zinazoshambuliwa na Israel. Tunafundisha namna bora ya kuishi!

Leo ni siku ya 19 ya mashambulizi ya Israel kwenye makazi ya Wapalestina, ambayo yamepoteza maisha ya watu wasiopungua 1,000 na kujeruhi wengine 6,000.

Picha: Mwonekano wa Maroketi Yakiruka Kwenye Anga la Gaza Kutoka Angani

Kutoka kwenye anga la mbali, mwanaanga Alexander Gerst anatazama namna Gaza inavyowaka moto. Anatwiti:

Picha mbaya sana hii. Kutoka ISS tunaweza kuona milipuko na maroketi yakipaa gaza na Israel

Picha hii imechapishwa kwa mara nyingine kwa zaidi ya mara 33,000 mpaka sasa.

Namna ya Kuwa Baba Mwema

padreehijo

Picha ya Lon Queta kwenye mtandao flickr (CC BY-NC-SA 2.0).

Raia wa Panama Joel Silva Díaz anafafanua kile ambacho kinawashangaza watu wengi, hususani wanaume: namna ya kuwa baba mwema. Kwenye blogu yake anaeleza changamoto alizokutana nazo na baba yake mwenyewe na kuhusianisha na malengo yake kama baba:

…Recuerdo que veía como un juego el buscar un tema de conversación, debido a mi falta de interés en el deporte, nunca tuvimos una conversación de más de 5 líneas (legítimamente contadas por más de 10 años), pero conociendo otros casos e historias, por lo menos tuve un padre.
[…]
Y es eso lo que quiero mejorar, quiero ser un padre que no haga las cosas sin enterarse, quiero abrazar, quiero besar a mis hijos, presentarle siempre la opción de tomar las mejores decisiones y apoyarlos cuando no tomen las mejores, nunca dudar en mostrarles mi amor y cariño, mucho menos dudar cuando se ganen un coscorrón.
[…]
Pero mi parte no quiero que se quede en un apellido, o un cheque en la quincena, mi parte ha de ser presente, determinante y quiero que mi hijo o hija tenga por lo menos un solo recuerdo lindo impregnado en su corazón, como los domingos de Salsa y el olor a grama recién cortada de los domingos en mi casa.

Nakumbuka mchezo wa kuangalia cha kusema, shauri ya kutokupenda kwangu michezo hatukuwahi kuwa na mazungumzo ya zaidi ya mistari mitano (kwa uhakika kabisa nakumbuka kwa zaidi ya miaka kumi), lakini kwa kufahamu mahusiano yetu katika maeneo mengine, angalau naweza kusema nilikuwa na baba.
[…]
Na hicho ndicho ninachotaka kukifanya vizuri zaidi, nataka kuwa baba anayefanya bila hata kutambua, nataka kuwakumbatia, kuwabusu, kuwapa fursa bora za kufanya maamuzi bora na kuwasaidia wanapokuwa hawajafanya chema, sichelewi kuwonyesha upendo na kuwajali, hata kama kuna nyakati naweza kweli kuwafinya.
[…]
Kwangu, nisingependa jina la mwisho liishie, wala kuwachungulia kila baada ya majuma mawili, napaswa kuwepo, kuamua, na ninataka watoto wangu wawe na angalau kumbukumbu moja nzuri akilini mwao, kama mwanangu Salsa anavyokumbuka harufu nzuri ya majani yanapokuwa yamekatwa siku za Jumapili nyumbani.

Je, wewe ni, au unapanga kuwa baba mwema?

Unaweza kusoma zaidi anayoyaandika Silva Diaz kwa kumfuatilia kwenye akaunti yake ya G+ au Twita

Makala haya ni sehu ya kumi na moja ya #LunesDeBlogsGV, (Jumatatu ya blogu kwenye GV) siku ya Julai 14, 2014.

Trinidad & Tobago: Je, Kuishi kwenye Enzi za Kidijitali Kunahatarisha Haki yako ya Faragha??

Blogu ya ICT Pulse inapitia taarifa iliyochapishwa hivi karibuni iliyoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu juu ya haki ya faragha katika enzi hizi za dijitali.

Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine

So much for "knowing that feel," when it comes to polemics surrounding the downed Malaysian airliner. Images mixed by Kevin Rothrock.

Kuna namna nyingi “kujua mtu anavyojisikia,” ukifuatilia matamshi yanayotolewa baada ya kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia. Picha zimechanganywa na Kevin Rothrock.

Maafisa, wanasiasa na waandishi maarufu wa Kirusi walikuwa wepesi kutoa maoni kuhusiana na ajali ya Ndege ya Malaysia MH17, iliyoanguka Mashariki mwa Ukraine siku ya Alhamisi, Julai 17. Mamlaka za Kyiv, Moscow, na Donetsk zimekuwa zikishutumiana, kubebeshana lawama kwa kutunguliwa kwa ndege hiyo ya abiria na kuua watu wote karibu 300 waliokuwemo ndani yake. Wakati hisia zikiendelea kuongezeka, matamko machache yaliyotolewa na watu mashuhuri mjini Moscow na Donetsk yamevutia hisia ya watumiaji wa Intaneti mtandaoni. 

1. Katika hili, hatukufanya.

Waziri Mkuu aliyejitangaza mwenyewe wa Jamhuri ya watu wa Donetsk, Aleksandr Boroday, hakuwa na uhakika kuhusiana na uhusika wa waasi katika tukio hili:

Bahati mbaya, hii ni nukuu ya siku. [Maneno yanasomeka, “Kama ni kweli ni ndege ya abiria, basi haikuwa sisi,” Alexandr Boroday.]

2. Ina maana yoyote kujua nani alifanya kitendo hiki?

Leonid Kalashnikov, naibu mwakilishi wa kamati ya Bunge la Urusi ya mambo ya kimataifa, aliiambia TV Rain haikuwa na maana yoyote kujua nani wa kumlaumu kwa kuiangusha ndege hiyo:

“Вам что, легче станет, если узнаете, кто сбил самолет?”

“Nini, utajisikia nafuu kaa utamjua aliyeiangusha ndege hiyo?”

3. Uovu wa hali ya juu

Akiwa ameumizwa na kile waasi wa Urusi na ‘waendesha propaganda’ wa Ukraine walichokirudia mara kwa mara hisia zile zile (kwamba walikosoa serza ya Urusi kwa Ukraine), Konstantin Rykov wa chama tawala cha siasa Urusi alikuwa na haya ya kusema:

Katika nyakati kama hizi ni wazi kuna watu wanatarajia kitu na wanacho wanachokitaka…wapigania uhuru wetu na wapiga propaganda wa Ukraine wanashindania kile kile…

4. Ni rahisi: hakuna wa kumlaumu

Mkuu wa shirika la Russia TodayMargarita Simonyan alionyesha namna janga hilo lilivyo na faida kwa wa-Soviet wasio na akili:

Kw amuda mrefu nimekuwa nikifanyia kazi taarifa kadhaa za habari zinazotokea, na nimehitimisha kuwa siamini kabisa namna watu wanavyojaribu kuunganisha matukio kujengea hoja imani zao. Lkaini ninaamini kuwa Usoviet ina matatizo. 

5. Waasi? Waasi gani?

Mwisho lakini si kwa uzito ni mwitikio wa Vladimir Putin mwenyewe, aliyeliambia shirika la habari la ITAR-TASS kwamba Kyiv inawajibika kwa anga la Ukraine mashariki inayodhibitiwa na waasi.

“Безусловно, государство, над территорией которого это произошло, несет ответственность за эту страшную трагедию. […] Этой трагедии не произошло бы, если бы на этой земле был мир, не были бы возобновлены боевые действия на юго-востоке Украины”

“Kwa hakika, nchi ambayo mpaka wake ndiko tukio hili limetokea inawajibika kwa janga hili […] Janga hili lisingetokea kama pangekuwa na amani kwenye nchi hiyo, kama mapigano yasingeibuka tena Kusini Mashariki mwa Ukraine.”

Wa-Indonesia Wawasha Mishumaa Elfu Moja Ishara ya Amani kwa Palestina

Raia wa Indonesia walikusanyika katikati ya Jakarta, mji mkuu wa nchi hiyo, kuwasha mishumaa 1,000 kupinga mashambulio ya Israel katika ukanda wa Gaza. Indonesia ni moja ya nchi maarufu zaidi kwa wingi wa waumini wa dini ya Kiislam.

Indonesians pray for the  Palestinians who were killed in the airstrikes launched by Israel. Photo by Abdullah Arief Siregar. Copyright @Demotix (7/11/2014)

Wa-Indonesia wakisoma dua kwa ajili ya Wapalestina waliouawa kwenye mashambulio yaliyoanzishwa na Israel. Picha na Abdullah Arief Siregar. Haki Miliki @Demotix (7/11/2014)

Wanawake wa Kichina Waandamana Kupinga Kombe la Dunia

12 women staged an anti-World Cup protest on 7 of July in Shanghai. Photo from Weibo via Offbeat China.

Wanawake 12 walifanya maandamano ya kupinga kombe la dunia tarehe 7 Julai jijini Shanghai. Picha na Weibo Offbeat China.

Offbeat China alieleza kwa nini wanawake hao wana hasira na jinsi Kombe la Dunia linavyoharibu mahusiano ya kifamilia nchini China.

Wanapinga mambo mawili makubwa: 1) wapenzi wao kupuuza majukumu yao ya kifamilia kwa sababu ya kuangalia mpira usiku wa manane; 2) tabia za kucheza kamari kwa mashindano hayo.

Waandishi wa kimataifa Wakashifu Israeli kwa Kuendelea kwa Ujenzi wa Makazi

Waandishi kumi na sita wa kimataifa ambao walishiriki katika Tamasha la Wapalestina la Fasihi, lililofanyika katika miji kadhaa Palestina kuanzia Mei 31 hadi Juni 5, walitoa taarifa kukashifu Israeli kwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi na kupongeza juhudi za kususia kampeni ya Boycott Divest and Sanction (BDS). Taarifa, kupitia mtandao wa Facebook, inasema:

“Baada ya kushuhudia kibinafsi ukosefu wa haki kwa watu wa Palestina katika maeneo yaliyonyakuliwa na Israeli, ni kwa huzuni kubwa na kusikitishwa kwamba sisi – waandishi wa kimataifa na wasanii tuliotia saini hapa chini – twakumbuka idhini ya Benjamin Netanyahu ya wiki hii ya vitengo vingine vipya vya makazi haramu 1500 katika Ukanda wa Magharibi. Hii ni hasa ya kusikitisha kwa wakati ambao Wapalestina wameunda serikali ya umoja ambayo imetambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Makazi ya Israeli katika maeneo ya nchi nyingine kwa muda mrefu yametajwa kuwa kinyume cha sheria za kimataifa. Na makazi ya Israel kwenye maeneo ya Palestina ni kinyume cha sheria, na imetangazwa hivyo na jumuiya ya kimataifa kupitia maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

Makazi ya ziada yanaweza kuonekana tu kama kitendo cha uchokozi, kuonyesha kupuuza si tu kwa haki za binadamu na kiraia ya watu wa Palestina, lakini kwa sheria za kimataifa.

Tunapongeza juhudi isiyo na vurugu ya kampeni ya BDS (www.bdsmovement.net) na kuonyesha mshikamano wetu na mahitaji yake kwamba Israeli inapaswa kuzingatia maagizo ya sheria za kimataifa kwa:

1. Kukomesha ujenzi wa makazi na ukoloni wa ardhi yote ya Kiarabu na kubomolewa kwa Ukuta
2. Kutambua haki za msingi za raia wa Kiarabu na Palestina wa Israeli kwa usawa kamili; na
3. Kuheshimu, kulinda na kukuza haki za wakimbizi wa Kipalestina kurudi makwao na kwa mali yao kama ilivyoainishwa katika azimio la Umoja wa Mataifa 194

Kwa hivyo twatoa wito kwa serikali ya Israeli kuheshimu sheria za kimataifa na kugeuza idhini ya nyongeza ya makazi elfu moja na katika West Bank.

Sisi zaidi twatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kushawishi Israeli kuzingatia kanuni za msingi za sheria za kimataifa.

Imetiwa Saini na:

Sharif Abdel Khouddous
Susan Abdulhawa
Teju Cole
Nathan Hamilton
Nathalie Handal
Brigid Keenan
Sabrina Mahfouz
Michael Ondaatje
Ed Pavlic
Eliza Robertson
Sapphire
Kamila Shamsie
Ahdaf Soueif
Linda Spalding
Janne Teller
Haifa Zangana

Juni 6, 2014.”