Kufuatia Shambulizi la Garissa, Jamii ya Wazungumzaji wa Kifaransa Waungana na Wakenya

Twitter users show support for Garissa victims via Arnaud Seroy on twitter

Watumiaji wa Twita waonesha mshikamano wao na wahanga wa tukio la Garisa kupitia Arnaud Seroy katika Twita

Kwa mujibu wa Kituo cha Kitaifa cha Kukabiliana na Majanga cha nchini Kenya (KRCS), mnamo Aprili 2, 2015, watu wasiopungua 147 waliuawa kwa kufyatuliwa risasi katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya. Kituo hicho pia kilitaarifu kuwa  watu 79 walijeruhiwa na wengine 587 walifanikiwa kutolewa kutoka katika eneo la tukio.

Mtuhumiwa mkubwa wa mauaji haya ya halaiki ni kikundi cha wanamgambo wa Al-Shabaab kilicho na maskani yake nchini Somalia kilichotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Maelezo kutoka kwa wahanga wa tukio hili zilichochea watu kuonesha mshikamano wao kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kote. Jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kifaransa, bado wakiwa na kumbukumbu ya shambulizi la Charlie Hebdo, walionesha mshikamano wao na wahanga wa shambulizi la Garissa kupitia mitandao ya kijamii katika kiungo habari #JesuisKenyan (kama taswira ya kiungo habari cha hashtag #JesuisCharlie). Hii ilikuwa ndio mada ya pili kwa mvuto kuliko nyingine yoyote katika Twita nchini Ufaransa mnamo Aprili 3.

Yafuatayo ni baadhi tu ya machapisho hayo:

Watu 147 wamepoteza maisha katika shambulizi la kutisha la kigaidi dhidi ya wanachuo vijana wa taifa la kesho. Tuoneshe mshikamano wetu#JesuisKenyan

Haitoshi kuzungumzia shambulio hili la kigaidi lililotokea katika chuo kikuu cha Kenya kwenye mitandao ya kijamii, watu 147 ni wachache?! Inatisha sana #JesuisKenyan

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.