Habari kutoka 6 Oktoba 2013
Hong Kong: Video Inayosambazwa Mtandoni Yamwonyesha Jamaa Akipigwa Makofi Mara 14 na Rafiki Yake wa Kike
Kama inavyoelezwa na Tom Grundy, mpita njia aliwaita polisi na mwanamke huyo aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumpiga vibao rafiki yake wa kiume aliyekuwa amepiga magoti mbele yake akimwomba msamaha...
Hong Kong: Pinga Biashara ya Pembe za Ndovu
Muungano wa watu binafsi na Asasi Zisizo za Serikali zinazoguswa na tatizo la ujangili wa tembo, Hong Kong kwa Tembo, uliandamana Oktoba 4, wakiitaka Hong Kong kuteketeza hifadhi yake ya tani 25 za pembe za ndovu.
Gambia Yajitoa Jumuiya ya Madola, Yaiita Jumuiya Hiyo ‘Ukoloni Mambo-Leo’
"Gambia haitakuwa mwanachama wa taasisi yoyote ya ukoloni mambo-leo," nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitangaza katika tamko lake la wiki hii.