Hong Kong: Pinga Biashara ya Pembe za Ndovu

Muungano wa watu binafsi na Asasi Zisizo za Serikali zinazoguswa na tatizo la ujangili wa tembo, Hong Kong kwa Tembo, uliandamana mnamo Oktoba 4 katikati ya jiji wakiitaka serikali ya Hong Kong kuteketeza hifadhi yake ya tani 25 za pembe za ndovu.

Mkutano huo ni hatua ya kuunga mkono Matembezi ya Kimataifa kwa ajili ya kupigania tembo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Wanyamapori wa David Sheldrick chini ya kampeni ya iworry.

Lucy and Christine are acting as the spokesperson for the anti-ivory trade campaign in Hong Kong. Photo from Avaaz.org

Lucy na Christine wakiigiza kama wasemaji wa kampeni ya kupinga biashara ya pembe za ndovu mjini Hong Kong. Picha ya Avaaz.org

Hatua hiyo ya kupinga biashara ya pembe za ndofu ilizinduliwa na tamko la Lucy Lan Skrine mwenye umri wa miaka 11 na Christina Seigrist mwenye miaka 8 kwenye wavuti ya Avaaz.org katikati ya mwezi Septemba likitoa mwito wa kuteketezwa kwa pembe za ndofu zilizokamatwa ili kutuma ujumbe mzito kwa wateja wa bidhaa hiyo nchini China kuwa shughuli hiyo haifai na ni kinyume cha maadili. Watoto wawili wa shule wanaosoma Hong Kong, njia kuu ya biashara hiyo haramu kwa bishaa zinazotoka Afrika ili kuingizwa China. Katika mahojiano [zh] na mtandao wa inmediahk.net, wanasema wanapenda wanyama na kuwa wangependa kuwasaidia [wanyama hao] kusema ili kumaliza kuuawa kwa tembo. Wasichana hao wawili wamekuwa wasemaji wa Tembo nchini Hong Kong.

Activists demonstrated outside the Chinese Arts and Crafts Department Store on October 4. Photo by Mara McCaffery shared in International March for Elephants' event page.

Wanaharakati wakiandamana nje ya JUmba la Sanaa la Kichina na Ghala la Idara ya Vito Oktoba 4. Picha ya McCaffery imewekwa kwenye ukurasa wa matukio ya Matembezi ya Kimataifa kutetea Tembo.

Pamoja na hatua kali dhidi ya wahalifu wa pembe za ndovu zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong na Idara ya Forodha katika kutekeleza Tamko la Biashara ya Kimataifa la Viumbe Waliohatarini Kutoweka (CITES), imekuwa vigumu kwa mamlaka kuwatambua na kuwashitaki waingizaji wa bidhaa hiyo. Zaidi, biashara ya ndani ya bidhaa zinazotokana na pembe za ndovu inaruhusiwa nchini Hong Kong na hata bara China. Wakati bidhaa haramu za pembe za ndovu zikiingizwa China kupitia Hong Kong, zinanunuliwa kwa jumla na wazalishaji wa vito pamoja na wabunifu, na kugeuzwa kuwa bidhaa za thamani na kuingizwa kwenye mzunguko katika soko la ndani kupitia biashara zenye leseni na hata kwenye soko bubu.

Ni kwa sababu hiyo kampeni za kupinga bishara ya pembe za ndovu kimataifa, kama hiyo ya Waokoe Tembo Wote, zinatoa wito wa kumalizwa kwa biashara ya vito vinavyotokana na pembe hizo nchini China:

China ni kichocheo cha biashara ya pembe za ndovu, lakini hata hivyo inadai haihusiki na uwindaji haramu wa tembo. Ni viwanda vyake vingi vya utengenezaji wa vito vya thamani vinavyotengeneza bidhaa zote zinazonunuliwa na watu. Utengenezaji wa bidhaa hiyo ni sababu ya bishara hiyo. China inategemea pembe za ndovu kuzalisha bidhaa hizo. Kwa hiyo ni lazima wawajibishwe, na nyie, wanaharakati, ndio mnaopaswa kuchukua hatua, za kuitaka serikali yenu kuitaka China kumaliza viwanda hivyo ili Tembo wapate haki yao ya kuishi.

Hili ni lengo la muda mrefu la kampeni hiyo ya Hong Kong Itetee Tembo. Mnamo Oktoba 4, kiasi cha wanaharakati 30 waliandamana kupitia barabara ya Nathan huko Tsim Sha Tsui, eneo maarufu kwa utalii nchini Hong Kong. Walipopita eneo la Sanaa na Ubunifu wa ki-China , duka maarufu la idara ya vito vya thamani vya ki-China ambapo bidha zinazotokana na pembe za ndovu hupatikana kwa wanunuzi, waliwataka wanunuzi wa ki-China kuacha kununua bidhaa hizo.

Mbali na kukuza uelewa wa jamii, muungano huo utawsilisha saini zilizokusanywa kutokana na tamko la mtandaoni kwa serikali ya Hong Kong na umeandaa mkutano na Idara ya Kilimo, Uvuvi na Hifadhi kujadili tamko lao la kuteketezwa kwa shehena ya pembe za ndovu zilzokamatwa. Kwa mujibu wa ushirikiano huo, kutekelezwa kwa shehena hiyo ni mwanzo tu, lengo lao ni kupigwa marufuku biashara ya pembe za ndovu:

Christine wants consumers aware that buying of ivory products is equal to killing of elephants. Photo from Hong Kong for Elephants.

Christine anataka wateja waelewe kuwa kununua bidhaa zinazotokana na pembe za ndovu ni sawa na kuua tembo. Picha ya kampeni ya Hong Kong Itetee Tembo.

Tunaitaka serikali ya China kupiga marufuku biashara hiyo ya tembo ndani ya nchi hiyo, kuyafunga maduka yote yanayouza bidhaa za pembe za ndovu na kufunga viwanda 37 vinavyomilikiwa na serikali vinavyotengeneza bidhaa hizo nchini kote.

Lakini kwanza tunakutaka wewe kusaini tamko letu kuiomba serikali ya Hong Kong kuteketeza shehena ya pembe za ndovu. Tunaitaka Hong Kong kutuma ujumbe kwa dunia kwamba pembe a ndovu hazikaribishwi nchini humu na hatutaruhusu jiji letu kuwa sehemu ya bishara hii ya kikatili na haramu. Hebu tafakari kuhusu tembo waliokufa ili kupata shehena ya tani 25 ya pembe za ndovu. Ni lazima tufanye kile kinachowezekana ili kuhakikisha tembo hawafi bure…

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.