Juni, 2013

Habari kutoka Juni, 2013

Hivi Bado Tunaye Rais Nchini Madagaska?

Patrick Rajoelina anahoji [fr] kisheria, ikiwa rais wa mpito Andry Rajoelina bado anataka kugombea katika uchaguzi ujao wa raia nchini Madagaska, basi hatakuwa na sifa tena za kuwa rais, kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini na vyama vyote vya nchi hiyo mwaka 2011. Waziri Mkuu wa sasa Beriziky alitoa tamko tarehe...

Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi

Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.