Tunisia: Mwanaharakati wa FEMEN Akabiliwa na Mashtaka Mapya

Kesi ya Amina Tyler, mwanaharakati wa FEMEN raia wa Tunisia, ambaye alikamatwa Mei 19 baada ya kuchora neno FEMEN kwenye ukuta wa makaburi ya Kairouan, kilomita 184 kutoka mji mkuu wa Tunis, itaendelea Juni 5.

Mnamo Mei 30, mahakama ilimtoza Amina faini ya dinari 300 za Tunisia (150 euro) kwa “kumiliki kifaa hatari kisichoruhusiwa” -kemikali za kupulizia. Wanasheria wa Amina walisema kwamba alikuwa na kifaa hicho kwa sababu ya kujilinda, kufuatia vitisho vya kuuawa alivyopata mwezi Machi, baada ya yeye kuwa ameweka picha inayomwonyesha bila nguo kifuani kwenye mtandao wa Facebook. Ingawa alikwepa kifungo cha miezi sita jela kwa mashtaka hayo, Amina bado yuko chini ya ulinzi na sasa anakabiliwa na mashtaka mapya: “kupuuza maadili ya jamii”, “kudharu eneo la makaburi” na “kuwa mwanachama wa shirika la kihalifu” [FEMEN]. Madai haya yanaweza kumfunga jela kwa miaka kadhaa msichana huyu wa miaka 19.

Tarehe 31 Mei, Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitoa wito kwa utawala wa Tunisia kumwachia Amina. Shirika hilo liliyaelezea mashtaka hayo kama “masuala ya kisiasa yanayomlenga [Amina] kwa sababu ya harakati zake za kutetea haki za wanawake”.

Kimya cha wanaojiita “Wanademokrasia”?
Kukosekana kwa msaada kwa ajili ya Amina kutoka kwa Chama cha Upinzani kisicho cha kidini nchini Tunisia, kulikosolewa. Woga wa kupoteza kura za wapiga kura wahafidhina kwa siku za mbeleni, inaonekana kwamba wanasiasa wa mrengo wa kushoto waliona ni bora kubaki kimya. Hii si mara ya kwanza vyama vya siasa vya mrengo wa kushoto kukabiliwa na madai ya kudumaza tunu zake za kimaendeleo. Kwa mfano, pia walituhumiwa kwa kuchagua msimamo dhaifu kwenye kesi ya Ghazi Beji na Jabeur Mejir, ambao walipatikana na hatia na kufungwa kwa miaka saba na nusu jela mwaka jana, kwa uchapishaji wa maudhui mtandaoni yaliyoonyesha kukashifu Uislamu.

Katika hati ya Avaaz ya kushinikiza kuachiwa kwa Amina, kamati ya msaada kwa mwanaharakati huyo kijana wa FEMEN ilisema [fr]:

Retour à la case prison pour Amina !
Nous avons toutes et tous été leurré(e)s par l’annonce de la relaxe d’Amina pour détention d’explosif. Amina, la prisonnière de l’hypocrisie politique tunisienne, du mutisme de celles et ceux qui veulent s’affirmer démocrates, mais qui n’osent prendre part à la lutte qui se joue actuellement.

Amina amerudi gerezani!
Sisi wote tulipumbazwa na tangazo kwamba Amina aliachiliwa kwa mashitaka ya kumimiliki kifaa hatari. Amina ni mfungwa wa unafiki wa kisiasa nchini Tunisia na kimya cha wale wanaojidai kuwa wanademokrasia lakini hawajaribu kuonyesha msimamo katika vita hivi vinavyoendelea.

Mwandishi wa Tunisia Gilbert Naccache pia alikosoa [fr] msimamo wa wanademokrasia uliotangazwa:

La démocratie a vraiment du mal à se frayer un chemin jusqu’à nos cerveaux ! Les mêmes qui se disent prêts à se battre jusqu’au bout pour les libertés (…) hurlent à l’intolérable provocation quand Amina s’exprime(…)

Les justifications de la condamnation d’Amina, même par ceux qui l’accusent de donner un prétexte à détourner l’attention des vrais problèmes, de contribuer à diviser davantage les Tunisiens, ne sont en fin de compte qu’une façon de ne pas assumer son devoir qui est de défendre Amina contre la calomnie et les mensonges (…) et de défendre le droit de tous à s’exprimer à sa façon…

Ni vigumu sana kwa demokrasia kupata nafasi kwenye akili zetu! Wale waliodai kuwa tayari kupambana mpaka mwisho kwa ajili ya uhuru, (…) wanakemea uchochezi usiovumilika wakati Amina alipojielezea (…)

Hila zilizotumika kumhukumu Amina, pia kwa wale ambao walimtuhumu kwa kuhamisha usikivu [wa umma] kutoka kwenye matatizo halisi au kugawa zaidi wa-Tunisia, kwa kweli ni kutafuta njia tu si kubeba wajibu wao ambao ni kumsaidia Amina dhidi ya uzushi na uongo, (…) na kusaidia haki ya kila mtu kujieleza katika njia yake mwenyewe.

Wanaharakati wengine watatu wa FEMEN, Wafaransa wawili na Mjerumani mmoja pia wanatarajiwa kujibu mashtaka Juni 5. Wanatarajiwa kufungwa kifungo cha miezi sita kwa kufanya maandamano wakiwa na vifua wazi nje ya makao ya mahakama ya Tunis mnamo Mei 29 kumuunga mkono Amina.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.