Habari kutoka 31 Julai 2010
Lebanoni: Utawala wa Dinosauri
Punde baada ya matukio ya unyanyasaji ya hivi karibuni nchini Lebanon, Msemo wa “Utawala wa Dinosauri” ulianza kutumika na wanaharakati wa mtandaoni kwenye kampeni dhidi ya uvamizi wa namna hii katika mitandao yao. Mwanablogu wa Lebanon Tony anaeleza maana ya msemo huo.
Brazil: Ukatili Dhidi ya Wanawake Kila Siku
Nchini Brazil, wanawake 10 huuwawa kila siku. Mauaji ya hivi karibuni na anasadikiwa kuwa mzazi wa mtoto wake, mlinda mlango nyota aneyetarajiwa, yamewasha cheche za majadiliano katika uwanja wa blogu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake.
Niger: Njaa ya Kimya Kimya
Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005.