Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Mpango wa Kimataifa wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umeamua kuongeza hatua za dharura Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005, baa la njaa la mwaka huu ambalo ni matokeo ya upungufu wa mvua mwaka jana.

Waume wakielekeza nyuso zao katika Jangwa la Sahel imepigwa na Nawal _kwa leseni ya Creative commons kwenye Flickr
D. Evariste Ouédraogo aliandika yafuatayo kuhusu namna wanasiasa wanavyojaribu mara zote kupindisha mabaa ya chakula nchini Naija kwa namna ambayo huwaweka wao katika mwanga mzuri zaidi [Kifaransa]:
En 2005, les autorités avaient toujours tenté de convaincre l’opinion que la menace de famine était une simple rumeur malveillante, déshonorante. [..] Quelques jours après, son Premier ministre (PM), dans des propos non moins fallacieux, appelait pourtant à l’aide, la Communauté mondiale, pour cause de …famine [..] Aujourd’hui, la vérité est toute nue : dix jours seulement après le changement de régime au Niger, on apprend, dans une déclaration télévisée du chef de la junte au pouvoir, que la famine “menace l’existence de millions de Nigériens dans quasiment toutes les régions”. Le déficit en vivres est alors estimé à 400 000 tonnes. Tout le contraire donc des péroraisons de Mamadou Tandja, qui était allergique à l’idée de risques de pénurie alimentaire.
Grioo.com inauliza kwa sauti kubwa swali gumu lakini lililo bayana kwamba Wanaija wengi wanashangazwa kuhusu: ““fedha zilizopatikana kutoka kwenye biashara ya madini ya Uranium zilikwenda wapi?” ” [Kifaransa]:
Qu’on se rappelle les tiraillements entre l’ex-chef de l’Etat du Niger et les premiers responsables d’AREVA à propos du renouvellement des contrats d’exploitation de l’uranium. [..] On ne dénoncera jamais assez ces slaloms qui permettent à des délinquants à col blanc d’extorquer impunément les fonds publics qui devraient servir à sauver de nombreux concitoyens en manque de nourriture, d’eau et de soins de base. Les masses d’argent tirées des ressources minières ne profitent généralement pas à la majorité silencieuse. Un paradoxe africain qui n’étonne guère. Mais aussi un scandale qui doit prendre fin en ce début de millénaire. A croire que les ressources minières n’apportent que misère aux populations africaines. Et il en sera tojours ainsi tant qu’elles ne seront pas utilisées à développer les cultures céréalières.
Kathryn Richards at Care anatushirikisha mawazo machache na ushuhuda wa “majira ya njaa” kadri idadi kubwa ya watu wa vijijini wanavyojikuta wakiwa kwenye uhitaji mkubwa wa mifugo ya kuchunga::
Naija ni nchi ya vinyume. Tajiri katika madini na mafuta yaliyogunduliwa siku za hivi karibuni lakini watu wake ni masikini wa kutisha. [..] Chakula kinapatikana katika soko –lakini kwa bei iliyopaa sana ambayo ni watu wachache tu wanaweza kuimudu. Familia zinauza mifugo yao kwa bei ya chini ili kununua chakula. Mohammed Gusnam alikuwa mmoja wa watu hawa: “ Ni vigumu . Kama wafugaji tulikuwa kama wana wa mfalme, wenye kiburi. Sasa ardhi ya kuchungia inapotea na tumekwama huko kijijini. Kijiji ni kama gereza kwangu.”
Mwitiko wa sasa wa janga la chakula, hata hivyo, unaonekana kuwa na kasi kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2005. Cyprien Fabre, kiongozi wa kitengo cha eneo maalumu wa Tume ya Ulaya ya Misaada ya Kibinadamu (ECHO) anatoa tathmini ifuatayo [fr]:
Des mécanismes d’alerte précoce et d’intervention sont en place dans la plupart des pays touchés, et des fonds ont été alloués rapidement. Les opérations sont en bonne voie au Niger, au Burkina Faso et au Mali. Le Tchad a besoin de plus d’acteurs pour une intervention efficace.
Bado mashirika mengi yanaamini kwamba vitendea kazi bado vinawasili kwa uchelevu sana. Mashirika hayo yanabainisha sababu mbili za uchelevu huo: 1) kuhakikisha kwamba wafadhili wanakuja na fedha za ufadhili na 2) changamoto za kuifikia idadi kubwa zaidi ya watu katika maeneo yasiyofikika kirahisi. Wengi wanafikiri kwamba kutoa fedha taslimu inaweza kuwa ni njia ya haraka na ya ufanisi zaidi katika kipindi kifupi kuliko kutuma (misaada hiyo kwa namna ya) chakula [Kifaransa]:
Au cours de discussions avec les membres des communautés, davantage de personnes ont dit préférer les espèces aux semences. Les communautés ayant accusé les pertes de récoltes les plus importantes ou qui vivent plus loin des marchés tendent à opter pour les semences ; celles qui ont accès aux marchés, ont accusé des pertes de récoltes moins graves, ou ont un accès limité aux terres tendent au contraire à privilégier le cash.