21 Septemba 2008

Habari kutoka 21 Septemba 2008

Msumbiji: Mgogoro wa Kisiasa Katika Jimbo la Kati la Beira

Waunga mkono wa Renamo wenye hasira walimwagika katika mitaa ya Beira ili kupinga uamuzi wa chama wa kumbadilisha Meya aliyeko madarakani Bwana Davis Simango na kumuweka Manuel Pereira kama mgombea wa kiti cha serikali ya manispaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Mwezi Novemba 2009. Mwanahistoria Egidio Vaz anaandika barua ya wazi kwa Rais wa Renamo, Bwana Alphonso Dhlakama katika blogu yake.

Irani: Redio Zamaneh, Redio ya Mabloga

  21 Septemba 2008

Redio Zamaneh ni redio ya lugha ya kipersia yenye makao yake huko mjini Amsterdam. Zamaneh ni neno linalomaanisha “wakati” katika lugha hiyo. Redio Zamaneh (RZ) ni chombo huru cha utangazaji kilichosajiliwa kama asasi isiyo ya kiserikali huko Uholanzi, kikiwa na studio na makao yake makuu mjini Amsterdam. Mratibu wa redio...