Irani: Redio Zamaneh, Redio ya Mabloga

Redio Zamaneh ni redio ya lugha ya kipersia yenye makao yake huko mjini Amsterdam. Zamaneh ni neno linalomaanisha “wakati” katika lugha hiyo. Redio Zamaneh (RZ) ni chombo huru cha utangazaji kilichosajiliwa kama asasi isiyo ya kiserikali huko Uholanzi, kikiwa na studio na makao yake makuu mjini Amsterdam. Mratibu wa redio hiyo ni Asasi isiyo ya kiserikali ya Kidachi ijulikanayo kama Press Now. Redio hiyo ilizinduliwa yapata miaka miwili iliyopita na imejipachika lahaja kwa jina la “redio ya mabloga”.

Bloga na mpiga picha Kamran Ashtray, ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano na maendeleo anaeleza changamoto, matumaini, na mafanikio ya nyanja ya uanahabari wa kiraia wa Irani.

RZ inajiita Redio ya mabloga. Kwa nini kauli mbiu hiyo? Ni kwa kuiwango gani mabloga wameweza kushawishi muelekeo wa wa RZ?

Waandishi wengi wa habari nchini Irani wameanza kublogu kwa sababu magazeti mengi yanaendelea kughasiwa na kufungwa. Wengi wa wachangiaji wa Redio Zamaneh walikuwa na bado ni mabloga. Mkurugenzi wetu, Mehdi jami, alianza kublogu kwa miaka kadhaa kabla ya kujiunga na Redio Zamaneh.
Kwa kuwa sera ya habari ya Redio Zamaneh imejikita kewenye uandishi wa kiraia, kuwafikia mabloga ilikuwa ni jambo la wazi. Kuanzia mwezi wa Agosti 2006, wakati Redio Zamaneh ilipoanzishwa, tumewahusisha na kuwatangaza mabloga katika tovuti yetu na katika programu za redio yetu. Wengi wao walihusika katika maendeleo ya RZ.

Redio Zamaneh ina uhusiano na mabloga katika njia nyingi. Jaribu kuangalia orodha ya blogu iliyoko kwenye tovuti. Redio Zamaneh inalenga kuwa na mawasiliano ya njia mbili. Hilo ndilo jambo ambalo mabloga wanajulikana kwalo. Hiyo ndiyo sababu ya tovuti yetu kufanya kazi kana kwamba ni seti ya blogu. Kila mchangiaji ana ukurasa wake/blogu na wasomaji wanaweza kuchangia maoni katika kila kurasa.

Kuna tovuti mbalimbali za habari, nje ya Irani, kama vile Deustche Welle (DW) Idhaa ya Kipersia, ambayo huweka blogu za Ki-Irani. Je kuna tofauti katika jinsi ya RZ inavyozichukulia blogu hizo na jinsi vyombo vingine vinavyochukulia?

Hatutundiki habari za mabloga tu, bali sisi ni mabloga na mtindo wetu ni wa kiana-blogu: ukaribu, bila ukiritimba, tofauti, kila moja na mtindo binafsi na mchanganyiko. Kublogu ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunaongea ndani ya blogu na kunukuu kutoka kwenye blogu. Tunaziona kama vyanzo vya habari vya jinsi watu wanavyofikiri kuhusu masuala ya siasa na jamii. Tunaona utamaduni wa vijana wa Ki-Irani kama utamaduni ambao unakuzwa kwenye blogu na tunafanya juhudi kuwezesha mtindo usio na ukiritimba wa kublogu uwe ni mtindo wa utengenezaji habari. Redio Zamaneh inatokana na, na kuhamasishwa na kublogu. Hivyo ni tofauti kabisa kutoka kwenye kunukuu blogu kama ilivyo katika vyombo vingine vya habari.

Ni vipi mabloga wa Ki-Irani walivyoichukulia RZ? Kwa kujishirikisha au kwa kuilaumu?

Tafiti katika Technorati, itakuonyesha kwamba kuna zaidi ya viungo 30,000 vinavyounga habari zinazobandikwa kwenye tovuti yetu.

Kadhalika, katika blogu Didish Report ya bloga wa Ki-Irani aishiye nchini Kanada Arashi Kamangir ambayo hutafiti tovuti zenye viungo kuelekea tovuti nyingine, inaonyesha kiudhabiti kuwa tupo juu kwenye orodha ya tovuti inayopata viungo kuwaelekea. Hiyo inaonyesha kwambakwamba mabloga wengi wanavutiwa na RZ na wanatuunganisha kwa viungo hivyo. Wengi wao wanafanya kazi na sisi kwa namna tofauti-tofauti na wengine hutuchambua vikali. Mabloga hawadharau kazi tunayofanya.

Tunakaribisha ushirikiano pamoja na kukosolewa. Kwa hakika, mmoja wa wanahabari wetu anafikiri kuwa tunaweza kuwatumia vizuri wale watu wanaotukejeli.

Tunakaribisha ukosoaji wa Redio Zamaneh hata tukafika hatua ya kudhamini shindano la kuchambua tovuti yetu. Shindano hilo lilituwezesha kuwatambua wenzi wetu. Redio Zamaneh ina historia madhubuti ya kuchapa maoni yanayotofautiana.

Tovuti ya RZ ina orodha ya mabloga kwenye ukurasa wake wa kwanza. Kuna wengine wanaoilaumu RZ kwa kuorodhesha mabloga wenye “siasa laini” na siyo zile ambazo zinatofautiana ana Jamhuri ya Kiislamu. Je uwajibu vipi hawa?

Kituo cha Berkman kilichoko Chuo Kikuu cha Harvard kinaripoti kuwa, zaidi ya blogu 60,000 ndani ya Irani huwa zinaongezwa habari mara kwa mara. Hivyo hatuwezi kuziunganisha zote kwenye tovuti yetu.

Redio Zamaneh haina nia ya kutangaza mabloga kulingana na mitazamo yao ya kisiasa. Wakati tunajitahidi kubaki huru, tunaunganisha blogu zenye miizamo mikali ya kisiasa, pamoja na zile ambazo huonekana kama zenye kushabikia au kupingana na utawala. Tunasoma blogu nyingi na hatujiwekei kikomo ili kuzijumuisha blogu chache teule. Baada ya kusema hivyo, tovuti ya Redio Zamaneh inajaribu kuziunga blogu zenye mahusiano na makundi ya kisiasa au makundi ya wale wenye siasa kali.

Baadhi ya tovuti za habari zinaogopa kuvipa sauti vyombo vya habari vya kiraia kwa sababu vinavichukulia kuwa ni vyanzo vya habari visivyoaminika. Je wewe unafikiriaje?

Ni vigumu kuachia madaraka. Kwa bahati, wengi wetu tumeshawahi kuwa mabloga, kwa hiyo tunaweza kuona pande zote mbili. Kutoka kwenye blogu huwa tunapata maoni, na sio habari. Habari zozote katika blogu ni lazima zihakikishwe kwa kutumia vyanzo vingine vya habari. Blogu zinaweza kuwa ni chanzo cha habari, lakini hatuzitegemei kuwa vyanzo vyetu pekee vya habari. Kadhalika tunajaribu kuendesha mafunzo pamoja na kufanya kazi na wanahabari wa kiraia ili kwamba waweze kutuletea habari zenye kuweza kutumainiwa kwamba ni za kweli. Hivi sasa tunatayarisha tovuti ya mafunzo kwa ajili ya waandishi wa kiraia, tovuti ambayo itakuwa ni kwa ajili ya wanamtandao wetu na kwa ajili ya watumiaji maalum walioandikishwa.

Nje ya Irani blogu nyingi zinazoandika juu ya siassa kama vile DW au Gozzar zina safu ya blogu. Ndani ya Irani, ni vyombo vichache mno vya habari vyenye tovuti ambazo zina safu kama hiyo. Kwa nini kuwepo na tofauti kama hiyo?

Ndani ya Irani wanataka kuwa na udhibiti zaidi kuhusiana na nini watu wanachoweza kukisoma. Hawana tu tabia ya kuwakilisha mitizamo ambayo hawawezi kuidhibiti. Tuktaka kuwa wakweli, hata vyombo vya habari vya magharibi vimechelewa kuwakumbatia mabloga vile vile. Siyo kawaida kwa shirika la habari kuunganisha vyanzo mbalimbali vya habari.

Je ni faida gani ambayo RZ imeviongezea vyombo vya habari vya Irani?

RZ imeonyesha kwamba inawezekana kuwakilisha maoni huru kuhusu Irani na habari. Inawapa sauti wale ambao ni vigumu kusikika, na inawapa mwangaza makundi yaliyotengwa katika Irani: waandishi, watu wa madhehebu ya Sunni, wanawake, mabloga, Wa-Armenia, Wa-Zoroastria, na makundi mengine ya kikabila au ya kidini. Redio Zamaneh inachapa, inatoa mwangaza, inaunga makala zilizoandikwa kwenye mtandao na wakosoaji wa siasa za ndani ya Irani, ambazo huwekwa kando na vyombo vya habari vya ndani ya Irani.

Pia, sisi huendesha programu ambazo huchachafya miiko ya jamii ya Irani kama ile inayohusiana na mahusiano na ngono. Wakati mwingine, changamoto huhusiana na msimamo wa kiserikali kisiasa, na wakati mwingine changamoto huhusiana na mitizamo mgando inayoshikiliwa na wengi, ndani na nje ya Irani.

Je ni changamoto zipi zenye umuhimu zaidi?

Kama tunataka kuwa na umuhimu na kuweza kuwashikilia waasomaji na wasikilizaji wetu, inatupasa kudumisha mawasiliano baina yetu na wao. Inakupasa uwe na mkondowazi wa mawasiliano. Inabidi tuwape moyo wasomaji na wasikilizaji kujishirikisha zaidi. Inatupasa kufungua masikio yetu. Inatupasa tujipe uhai mpya kila siku na pia tuwe wakosoaji wa kazi zetu wenyewe, na inatupasa tufanye kazi kwa nguvu ili kuweza kuendelea kuwa wakweli na huru.

Watu wangependa tufungamane na mirengo fulani fulani, ama iwe kuipinga serikali ya Irani au kuwaunga mkono wao, lakini sisi tumekuwa tukijitahidi kubakia huru bila kuhusisha imani zozote ambazo tunazo.

Changamoto kuu kwetu ni namna ya kuendelea na kutengeneza chombo cha habari endelevu. Tunaamini kuwa ili kuwa na jamii za kiraia endelevu ndani ya Irani tunahitaji kuwa na vyombo vya habari vya kidemokrasia vilivyo ndani ya na kwa ajili ya Irani.

RZ inakabili vipi uchujaji wa habari?

Ni mchezo wa paka na panya. Inatubidi tuendelee kutafuta mashimo ya kujificha. Tumebadilisha jina la tovuti yetu mara 5! Tunatuma kijarida chetu kila siku kwa watu wengi ambao wanataka kuzoma RZ ambao hawana namna ya kusoma tovuti yetu moja kwa moja. Lakini hatuwezi kusema kuwa tunaweza kuepuka uchujwaji wa habari. Kurasa nyingi zimezuiliwa. Pamoja na hivyo, zaidi ya asilimia 60 ya wasomaji wetu wapo ndani ya Irani.

Mara nyingine habari huchapwa na bloga aliyeko mikoani au na bloga aliyeko ndani ya jiji. Je kuna tofauti kati ya bloga aliye mikoani na yule aliye Teherani?
Kwa namna mbalimbali wale walioko nje ya mji mkuu hujisia wapweke na kutotiliwa maanani. Kwa wengi, Irani inamaanisha Teherani. Teherani ni muhimu sana, lakini hatuwachi kuipa umaanani miji iliyopo Kurdistan, Khorasan, Azarbayjan, Khuzistan, Fars, na nchi nzima kwa ujumla. Tunajaribu kuwajuisha wote na kuwapa sauti, uhakika na msaada.

Tunayo programu inayolenga kuwapata mabloga wazuri walioko mikoani na kuwakuza kwa kuwanukuu au kwa kuongea nao. Tunakaribisha michango kutoka mikoani hata kama hatuwezi kutumia muda mwingi kuwanukuu kama ambavyo tunafanya kwa wale walioko mji mkuu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.