Habari kutoka 18 Agosti 2012
Syria: Mafunzo ya Silaha na Namna ya Kupigana Katika Mtandao wa Intaneti
Waasi nchini Syria wameanza kutumia YouTube ili kupeana mafunzo hasa kupitia 'Free Syrian Army Help' yaani 'Msaada wa Jeshi la Kuikomboa Syria'. Chaneli hiyo ina picha za video zipatazo 80 zikiliezea mbinu kama vile vita ya uso-kwa-uso, jinsi ya kutengeneza mabomu ya kutupwa kwa mkono, na jinsi ya kuwavizia maadui.
Morocco: Wanafunzi Wadai Marekebisho kwenye Mfumo wa Elimu
Mwezi Julai, kikundi cha wanafunzi wa nchini Morocco kilizindua ukurasa wa Facebook ulioitwa "Umoja wa Wanafunzi wa Morocco kwa ajili ya Mabadiliko ya Mfumo wa Elimu". Pungufu ya mwezi mmoja, kikundi hiki kilivuta uungwaji mkono mkubwa hasa kupitia mitandao ya kijamii.