Habari kutoka 10 Machi 2010
Naijeria: Ghasia Zalipuka Huko Jos Kwa Mara Nyingine
Huko Jos, machafuko yanaelekea kujitokeza katika mizunguko inayozidi kuwa midogo: machafuko mabaya yaliukumba mji huo mwaka 1994, 2001, 2008, na – hata miezi miwili iliyopita – mnamo mwezi Januari 2010. Mgogoro wa sasa unasemekana kuwa ulianza katika tukio la kisasi kilichotokana na uharibifu uliotokea mwezi Januari, na, kama ilivyokuwa kwenye machafuko yaliyopita, mapambano ya sasa huko Jos yamekuwa yakipiginwa katika misingi ya kidini.