· Machi, 2014

Habari kuhusu Maandamano kutoka Machi, 2014

Ufisadi Nchini Nepal: Umeanza Kuwa Tabia Inayokubalika Kijamii?

  26 Machi 2014

Watu wana hasira na wamechoka, na mashirika ya habari mara nyingi huchapisha habari kuhusu uhusiano kati ya viongozi wa kisiasa na wezi wa mali za umma lakini hakuna anayezungumzia kuingia mtaani kuandamana kupinga ufisadi -hali isiyotarajiwa kwenye nchi ambayo watu hugomea kila kisichokwenda sawa Siromani Dhungana anaandika uchambuzi kwenye blogu...

Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa

  21 Machi 2014

Mamia ya watafsiri wamejipanga kupitia mtandao wa facebook kutafsiri habari kuhusu maandamano ya raia wanaojikusanya kwenye Bunge la nchi hiyo kupinga hatua ya chama tawala nchini humo kupitisha mkataba wa kibiashara wenye utata na nchi ya China.

Mazungumzo ya GV: Kipi Kinafuata Nchini Ukraine?

  7 Machi 2014

Kipi kinafuata kwenye vuguvugu la maaandamano ya Ukraine? Maandamano na umwagaji damu ulisababisha kung'oka kwa rais anayetuhumiwa kuwa fisadi. Lakini sasa, wakati Urusi ikijiandaa kijeshi na Crimea ikifikiria kujitenga, yapo maswali mengi yasiyoisha kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini Ukraine pamoja na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.