· Juni, 2013

Habari kuhusu Maandamano kutoka Juni, 2013

Mtu Mmoja Afariki Kwenye Maandamano Yanayoitikisa Brazil

Kijana mdogo aliuawa baada ya kugongwa na gari huko Ribeirao Preto na dazeni ya watu wengine walijeruhiwa pale waandamanaji walipokuwa wakikabiliana na polisi katika majiji ya Brasilia, Rio de Janeiro na Salvador kufuatia watu zaidi ya milioni moja kujitokeza katika mitaa ya majiji makubwa na madogo nchini kote Brazil katika maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miongo miwili.

28 Juni 2013

PICHA: Mamia Wakamatwa Nchini Brazil kwa Kupinga Ongezeko la Nauli za Mabasi

Polisi wanakabiliana kwa vurugu na kwa kutumia moshi wa machozi dhidi ya waandamanaji wanaopinga ongezeko la nauli ya usafiri wa umma katika maandamano ya yalioyodumu kwa siku ya nne mfululizo huko Sao Paulo. Maandamano haya ni sehemu ya Harakati za Kudai Usafiri wa Bure ambazo tayari zimeshasambaa katika miji mikuu mingine yote nchini Brazil.

22 Juni 2013

Maandamano ya Kudai Uhuru Yafanyika Kwenye Miji ya Saudi Arabia.

Makundi madogo madogo ya wanawake wa Saudi Arabia kwa wakati mmoja yaliitisha “mikutano ya kudai uhuru” katika maeneo mbalimbali ya majiji ya Saudi Arabia mnamo tarehe 10 Juni, 2013, maandamano yaliyoratibiwa na kundi lisilojulikana la mawakili @almonaseron [ Waungaji mkono] linaloshinikiza kuachiwa huru kwa ndugu zao wanaoshikil

16 Juni 2013

Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi

Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.

1 Juni 2013