Mazungumzo ya GV: Kipi Kinafuata Nchini Ukraine?

Kipi kinafuata kwenye vuguvugu la maaandamano ya Ukraine? Maandamano na umwagaji damu ulisababisha kung'oka kwa rais anayetuhumiwa kuwa fisadi. Lakini sasa, wakati Urusi ikijiandaa kijeshi na Crimea ikifikiria kujitenga, yapo maswali mengi yasiyoisha kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini Ukraine pamoja na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya. Vyombo rasmi vya habari nchini Urusi na Ukraine vinachochea misuguano, wakati waandishi na wanaharakati wa mtandaoni wanatumia mtandao wa intaneti kupambana dhidi ya upotoshaji wa taarifa na propaganda.

Tunazungumza na waandishi wetu wa Global Voices walioko Ukraine Tetyana Lokot na Tetyana Bohdanova kujua zaidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.