· Januari, 2011

Habari kuhusu Maandamano kutoka Januari, 2011

Tunisia: Anonymous Dhidi ya Ammar – Nani Atashinda Vita ya Kuchuja Habari?

Kichuja habari cha Tunisia, kinachojulikana kama Ammar, kinaeendelea kutishia kuziharibu na kuzifunga anuani za wanaharakati wa mtandaoni, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikishuhudia wimbi la maandamano tangu katikati ya mwezi Desemba. Ni leo tu, wanaharakati wamedai kwamba serikali imeingilia anuani zao za barua pepe,na kuziingilia blogu na mitandao yao ya kijamii, na kuzizuia zisifanye kazi. Hatua hii inaonekana kuja kama kulipiza kisasi kwa shambulio lililofanywa na kikundi cha wanaharakati wa mtanda0ni wanaojulikana kama Anonymous, ambalo lililenga njia na mitandao ya muhimu ya Serikali ya Tunisia.