· Oktoba, 2012

Habari kuhusu Maandamano kutoka Oktoba, 2012

Misri: Ushauri kwa Waandamanaji wa Kuwait

Wakati watu wa Kuwait walipoanzisha maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea ya kuonesha waziwazi kutokukubaliana na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaliyopitishwa chini ya mtawala wa kurithi kufuatia kuvunjwa kwa bunge, watu wa Misri wametumia muda wao mwingi katika Twita wakitoa ushauri kwa watu wa Kuwait kuhusiana na yapi ya kufanya na yapi ya kutokufanya.

27 Oktoba 2012

Kuwait: Ni Maandamano Makubwa Kabisa Kuwahi Kutokea?

Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Maandamano hayo yaliyofanyika siku ya Jumapili, na kuratibiwa kupitia katika mtandao wa Twita na yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.

27 Oktoba 2012

India: Mgogoro wa Mtambo wa Nyuklia wa Kudankulam Waendelea.

Mradi wa Nguvu za Nyuklia mjini Koodankulam katika wilaya ya Tirunelveli iliyo katika Jimbo la kusini la Tamil Nadu nchini India umeanza kufanya kazi mwezi uliopita lakini maandamano ya kuupinga mradi huo umeendelea na kamata kamata inasababisha waandamanaji kuishia jela. Juma hili limeshuhudia maandamano yakienea India yote kwa ushirikiano na watu wanaopinga matumizi ya Mtambo wa Nyuklia.

22 Oktoba 2012

Tunisia: Mgomo Waanza jijini Thala

Kupitia mtandao wa twita, Tounsia Hourra (m-Tunisia huru) anasema [ar] kuna mgomo mkubwa umeanza jijini Thala, kwenye jimbo la Kasserine, leo [Oktoba 8, 2012]. Mgomo huo umekuja kama hatua ya...

8 Oktoba 2012