Habari kuhusu Maandamano kutoka Agosti, 2012
Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru
'Nilitishiwa kufanyiwa vitendo vya ngono na kutendewa vibaya mara kadhaa katika siku ile. Wakati mmoja hata na ofisa wa ngazi za juu wa #NISS.' Mwezi Juni, Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudani liliwakamata maelfu ikiwa ni pamoja na mwanaharakati anayetumia Twita Usamah Mohamed Ali.
Mauritania: Wafanyakazi wa Migodini Wapinga ‘Aina Mpya ya Utumwa’
Zaidi ya wafanyakazi 2,300 wako kwenye mgomo nchini Mauritania katika mji wa kaskazini wa Zouerat, jambo ambalo limesababisha kuzorota kwa maeneo mengine kumi ya Kampuni la Taifa la Madini na Viwanda, huku kazi zikiwa kwenye mvurugiko mkubwa. Madai yamejikita katika suala zima la maslahi bora ya wafanyakazi.
Syria: Mafunzo ya Silaha na Namna ya Kupigana Katika Mtandao wa Intaneti
Waasi nchini Syria wameanza kutumia YouTube ili kupeana mafunzo hasa kupitia 'Free Syrian Army Help' yaani 'Msaada wa Jeshi la Kuikomboa Syria'. Chaneli hiyo ina picha za video zipatazo 80 zikiliezea mbinu kama vile vita ya uso-kwa-uso, jinsi ya kutengeneza mabomu ya kutupwa kwa mkono, na jinsi ya kuwavizia maadui.
Morocco: Wanafunzi Wadai Marekebisho kwenye Mfumo wa Elimu
Mwezi Julai, kikundi cha wanafunzi wa nchini Morocco kilizindua ukurasa wa Facebook ulioitwa "Umoja wa Wanafunzi wa Morocco kwa ajili ya Mabadiliko ya Mfumo wa Elimu". Pungufu ya mwezi mmoja, kikundi hiki kilivuta uungwaji mkono mkubwa hasa kupitia mitandao ya kijamii.