Habari kuhusu Maandamano kutoka Februari, 2010
Nijeria: Baada ya miezi miwili bila uongozi, kaimu Rais mpya
Baada ya wiki za mivutano ya kisiasa, Baraza la Seneti lilimthibitisha Goodluck Jonathan kama kaimu Rais. Wengi kwenye ulimwengu wa blogu waliliona tukio hilo kama sababu ya kusherehekea… lakini wengine waliliona kama jambo la kutia hofu, wakieleza kwamba japokuwa kutwaa madaraka kwa Jonathan kunaweza kuwa ni ulazima wa kisiasa, kutwaa huko hakujaruhusiwa wazi na katiba ya Naijeria.
Misri: Mwanablogu apoteza kazi kwa kufichua ukweli kuhusu habari ya bikra za bandia
Mwanablogu ambaye pia ni mwanahabari wa Kimisri Amira Al Tahawi amefukuzwa kazi kwa kufichua ukweli kuhusu habari ya uongo juu ya bikra za bandia zinazotengenezwa China katika makala alioyoichapa kwenye yake, ndivyo wanavyodai wanablogu. Yafuatayo ni baadhi ya maoni kutoka kwenye ulimwengu wa blogu za Kimisri kuhusu kisa hicho.
Urusi: Maandamano ya Kupinga Serikali Yaripotiwa na Wanablogu, Yasusiwa na Vyombo Vikuu vya Habari

Wakati maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali nchini Urusi katika muongo uliopita yanazidi kudharauliwa na vyombo vikuu vya habari nchini humo, ulimwengu wa blogu unachemka na makala kadhaa juu ya maandamano hayo na athari zinazoweza kutokea.