Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa

Against Black-box Cross-Strait Trade Agreement. Protest icon from CSSTAtranslategroup.

Mkataba wa kupinga makubaliano ya kibishara yaitwayo Black-box Cross-Strait. Alama ya maandamano kutoka kwenye kundi la Facebook liitwalo CSSTAtranslategroup.

Waandamanaji mjini Taiwan waliandika historia mnamo Machi 18 kwa  kukaa kwenye viunga vya bunge la nchi hiyo  wakipinga chama tawala kupitisha Mkataba wa Kibiashara unaoruhusu wafanyabiashara kupita mpakani bila kizuizi (CSSTA) , makubaliano yaliyofikiwa baina ya nchi hiyo na China bila kufuata utaratibu wa  kupitia kufungu kwa kifungu. 

Waandamanaji walipata Uungwaji mkono kutoka kwenye makundi mbalimbali, huku mamia ya watafsiri wakijipanga kupitia mtandao wa Facebook kwneye kundi liitwalo #CSSTAtranslategroup (Kundi la Kutafsiri mkataba huo) ili kuweza kutafsiri habari zinazohusiana na tukio hilo. Kundi hilo linaelezea malengo yake kuwa ni:

1. Malengo yamuda mfupi: kusambaza taarifa kwa vyombo vya habari ambazo zinakuwa zimetafsiriwa katika lugha mbalimbali ili kwenda kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na mashirika ya serikali;
2. Lengo la muda wa kati: kufuatilia kwa karibu hatua inayofuata baina ya Serikali za China na Taiwani na kutafsiri habari zinazojiri kwa Kiingereza na lugha nyinginezo.

Makala yanayotafsiriwa yanachapishwa kwenye blogu ya  Taiwan, haiuzwi. Taarifa kwa vyombo vya habari neno kwa neno kwa sasa inapatikana kwa lugha ya Kichina/a>, Kiingereza na Kijerumani. Vilevile kuna toleo la Kidenishi kwa muhtasari.

Ili kuweza kuvuta hisia za dunia nzima kwenye maandamano hayo, mwanaharakati mwanafunzi Yeh Jiunn Tyng ametafsiri ujumbe ufuatao katika lugha tofauti 31 kwenye wasifu wake wa mtandao wa Facebook:

Raia wa Taiwan hivi sasa wanakusanyika kwenye viwanja vya Bunge la Nchi hiyo (Yuan), wakipinga kupitishwa kwa Mkataba usio wa haki wa kuruhusu wafanyabiashara kupita bila kukaguliwa. Polisi wanakusanyika nje ya jengo na wanajiandaa kuwatawanya waandamanaji.
Wakati huu ni muhimu kwa ajili ya mustakabali na demokrasia ya Taiwan, kwa hivyo tunahitaji kusikilizwa. Tafadhali sambaza habari hizi kwa kila unayemfahamu, na tafsiri habari hizi kwa lugha nyinginezo.(Tafadhali tuma tafsiri yako kwenye sehemu ya maoni ya bandiko hili, na nitaiongeza kwenye orodha). Mungu ibariki Taiwan.

Posti yake imependwa mara 9,000 na imesambazwa zaidi ya mara 15,000.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.