Habari kuhusu Maandamano kutoka Julai, 2013
Tamko la Kurekebisha Sheria Zinazokwaza Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Vietnam
Zaidi ya wanablogu 60 wa Ki-vietinam walitia saini tamko la pamoja kuitaka serikali ya Vietnam kuboresha rekodi ya haki za binadamu na ahadi wanapowania uanachama katika Baraza la Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu:...
Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi
Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo...
Wanawake Watatu Wauawa katika Maandamano ya Kumtetea Morsi
Waandamanaji wanaomuunga mkono Morsi wameshambuliwa na mahuni huko Mansoura, tukio lililopelekea wanawake wasiopungua watatu kuuawa pamoja na makumi mawili wengine kujeruhiwa. Watumiaji wa mtandao wameonesha hisia zao kufuatia shambulio hilo.
Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China
Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.
Wakazi wa Jiangmen Nchini China Wapinga Ujenzi wa Mtambo wa Uranium
Siku ya tarehe 12 Julai, 2013, mamia kadhaa ya wakazi wa Jiangmen, jiji lililo jirani na Guangzhou ya Kusini nchini China, walifurika mtaani na kuandamana kupinga mpango wa kuanzisha mtambo wa kuchakata Urani.
Rais wa Zamani wa Misri Morsi Aibukia Kwenye Mtandao wa Twita
Rais Mohamed Morsi si rais tena wa Misri. Badala yake, ameibukia kwenye mtandao wa twita kupitia anuani yake iliyothibitishwa ya @EgyPresidency.
Misri yasema: “HAYAKUWA mapinduzi ya kijeshi”
Hatua ya Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Misri - habari zinazotangazwa mashirika ya habari, hususani CNN, kuhusu siasa zinavyoendelea Misri - zilikumbana na moto jana usiku. Kung'olewa kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi baada ya kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu madarakani kuliamsha shamra shamra nchi nzima, pamoja na vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi.
Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi
Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."
Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani
Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.
Mwandamanaji Amtaka Morsi Kuondoka Kwa Lugha ya Mafumbo
Maandamano makubwa ya kumtaka rais wa Misri Mohamed Morsi ajiuzulu yanaendelea nchini Misri kwa siku ya tatu sasa. Kwenye mtandao wa Twita, Assem Memon anaweka picha iliyopigwa kwenye maandamano: @AssemMemon: Bango...