· Machi, 2014

Habari kuhusu Maandamano kutoka Machi, 2014

Video: Usambazaji Vyakula katika Kambi ya Yarmouk-Syria

  5 Machi 2014

Shirika la habari la FAJER liliweka mtandaoni video ya kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus wakati wa kupokea mgawo wa chakula cha kuwalisha wakazi 18,000 wa kambi waliobaki, ambao wamelazimishwa kula wanyama waliopotea ili kuokoa maisha yao wakati huu ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula. Video ni ya tarehe...

Kwa nini Maandamano Hayatasababisha ‘Mapinduzi ya Cambodia’

  4 Machi 2014

Faine Greenwood anaandika kuhusu mhadhara wa Stanford uliotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Cambodia Ou Virak. Aliuliza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Cambodia, Ou Virak alieleza kwa nini hayatasababisha ‘mapinduzi ya kisiasa': Sidhani kuwa mapinduzi ya Cambondia yatatokea, na wala sidhani yanahitajika…Hatuna hata neno muafaka kwa...

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.