Habari kuhusu Maandamano kutoka Februari, 2013
Bulgaria: Gharama Kubwa za Nishati Zasababisha Maandamano
Ruslan Trad anataarifu kuwa, siku ya Jumapili tarehe 17 Februari, makumi ya maelfu ya watu katika mji mkuu wa Bulgaria, Sofia pamoja na majiji mengine waliendelea na maandamano kupinga bei kubwa za nishati ya umeme pamoja na gharama za kupasha joto.
Bangladeshi: Raia Wakutana Kudai Haki Itendeke
Kidogo kidogo, makutano ya Shahbag katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka yamefurika watu wenye lengo la kutaka haki kufuatia ukatili uliofanywa mnamo mwaka 1971 wakati wa harakati za vita vya kutafuta uhuru pamoja na kudai hukumu ya kifo kwa wahalifu wa vita.Drop by drop, the Shahbag intersection in Bangladesh's capital city Dhaka has become an ocean of people, demanding justice for the atrocities committed during the country's 1971 liberation war and death penalty for war criminals.
Wakati Papa Anajiuzulu, Warusi Wajiuzulu kwa Putin
Pasipokutaka kujua matokeo ya kujiuzulu kwa Papa Benedict na athari yake kwa imani ya Kikatoliki au tafsiri ya hatua hiyo kufuatia kashfa ya udhalilishaji iliyowakabili kwa watawa, RuNet walioweka habari hiyo kwenye safu za vichekesho.