Habari kuhusu Maandamano kutoka Mei, 2014
Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia
Ghasia, zilizofumuka baada ya kuuawa kwa kijana wa miaka 19, zilisababisha misuguano kati ya watu wenye asili ya Albania na Masedonia kwenye jiji la Skopje.
Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu
Katika maeneo kadhaa nchini Chile, maandamano ya wanafunzi kudai elimu ya bure na kushirikishwa kwenye mabadiliko yanayoendelea nchini humo yalifanywa Mei 8, 2014. Hata hivyo, yalikabiliwa na bughudha za hapa na pale.
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
Mzee wa Kimasedonia Apambana Kurejeshewa Mali Yake
Mwanablogu wa Kimasedonia anayeitwa Dushko Brankovikj, ambaye mali zake zimetaifishwa mara mbili, ameshinda kesi, lakini serikali haijaweza kumrudishia mali zake.
China Yamweka Kizuizini Mwanasheria wa Haki za Binadamu Pu Zhiqiang
Hii si mara ya kwanza kwa Pu Zhiqiang kuwekwa kizuizini. Akiwa mkosoaji maarufu wa sera za serikali ya China, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama wa nchi hiyo.
PICHA: Waandamanaji Nchini Taiwani Wageuza Uzio wa Polisi kuwa Mapambo
Polisi waliweka uzio wa kuwapa tahadhari waandamanaji kuzunguka majengo ya serikali katika jitihada za kuwazuia waandamanaji kukusanyika. Wataiwani wakawajibu kwa kile kinachoonekana kuyageuza mabango hayo ya tahadhari kuwa mapambo.
Madai ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu Wakati wa Mgomo wa Kilimo Nchini Colombia
Tovuti ya ‘kongamano la watu’ imeshutumu hadharani [es] uvunjifu wa haki za binadamu unayoendelea katika mgomo wa kilimo [es] nchini Colombia. Wanaripoti madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika...
Mazungumzo ya GV: Maandamano ya ‘Alizeti’ Taiwan
Je, harakati za kupigania demokrasia nchini Taiwani zina demokrasia ndani yake? Tunazungumza na waandishi wetu wa Taiwani kuhusu maandamano hayo pamoja na uwezekano wa mamlaka kamili ya nchi hiyo kutoka China.
Caribbean Yajiunga na Kampeni ya #BringBackOurGirls
Kama watoto wetu wangetoweka tungelipenda dunia yote kusimama na kuja kutusaidia kuwatafuta wao. Sisi … tunauliza kwamba … kwa nini mara nyingi miili ya wanawake huwa uwanja wa vita ambapo...