· Julai, 2012

Habari kuhusu Maandamano kutoka Julai, 2012

Tanzania: Mgomo wa Walimu Watikisa Nchi

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika zoezi la sensa, walimu nchini Tanzania wako katika mgomo kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao pamoja na kuboresha mishahara yao. Hatua hiyo imevuta hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanaojadili madhara ya mgomo huo.

Ethiopia: Maandamano ya Waislamu Yashika Kasi

Jeshi la Polisi nchini Ethiopia waliamua kutumia nguvu kupambana na wanaharakati wa ki-Islamu, likituhumiwa kufanya vitendo haramu katika maeneo yanayochukuliwa kuwa matakatifu katika misikiti, kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na ukurasa wa kikundi cha waislam katika mtandao wa Facebook uitwao Dimtsachin Yisema (Iache Sauti Yetu Isikike). Tangu mwezi Mei, Wa-Islamu wa ki-Ethiopia wamekuwa wakiandamana kupinga serikali kuingilia mambo yao ya kidini.

Hispania: Maandamano ya Wachimbaji Madini Yaungwa Mkono na Wananchi

  16 Julai 2012

Maelfu ya wananchi wa Uhispania wameungana na maandamano ya wachimbaji wa madini nchini humo, wakati waandamanaji hao walipowasili nchini Madrid baada ya kutembea kilometa 400 wakitokea kaskazini mwa nchi hiyo. Wachimbaji hao walishangazwa na kiwango cha hamasa kilichoonyeshwa, ambacho kiliongeza chachu ya kile ambacho sasa chaitwa 'usiku wa wachimbaji madini'

Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa

  7 Julai 2012

Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.