Habari kuhusu Maandamano kutoka Novemba, 2012
Mkanganyiko wa Makubaliano ya OIC Kuanzisha Ofisi Nchini Myanmar
Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) limependekeza kuanzisha ofisi nchini Myanmar kwa lengo la kukisaidia kikundi kidogo cha Waislamu nchini humo. Serikali ilishakubaliana na mpango huu lakini ilibadili uamuzi huu mara baada ya kutokea maandamano ya kupinga uamuzi huo katika maeneo mengi ya nchi.
Chile: Mahabusu wa Mapuche Wamaliza Mgomo wa Kutokula Uliodumu kwa Siku 60
Baada ya siku 60 za mgomo wa kutokula, mahabusu wanne wa Mapuche wamesitisha mgomo wao mara baada ya Mahakama Kuu ya Chile kukubaliana na baadhi ya madai yao. Juhudi hizi pia zimepelekea kuwepo kwa migowanyiko kiasi kuhusiana na mgogoro miongoni mwa watu wa Chile.
Mradi wa Tafsiri: Kauli ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni

Katika siku saba zijazo, Wafasiri wa Kujitolea wa Mradi wa Lingua wa taasisi ya Global Voices watakuwa wakitafsiri makala maalumu ambayo ni harakati ya utetezi unaofanywa na umma mtandaoni na...