Habari kuhusu Maandamano kutoka Januari, 2013
Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain
Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.
Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.
Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.
Kuhusiana na Vuguvugu la Mabadiliko ya Umma
Gaurav Mishra anachambua nguvu ya vuguvugu la mabadiliko linaloanzia kwa watu wa kawaida na namna inavyofanya kazi kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa vyombo vikuu vya habari kwa kutumia vyombo...
Waandamanaji wa Hangari Wafunga Daraja, Wanafunzi Watatu Watiwa Nguvuni.
Harakati za maandamano ya wanafunzi zinaendelea nchini Hangari. Usiku wa Jumatano, waandamanaji walizingira daraja la Budapest na wanafunzi watatu waliishia kuwekwa kizuizini na polisi.