Waandamanaji wa Hangari Wafunga Daraja, Wanafunzi Watatu Watiwa Nguvuni.

Waandamanaji watatu walitiwa kizuizini usiku wa jumatano siku ambayo wanafunzi walipojazana katika daraja la Budapest. Umoja wa wanafunzi wa kuanzia ngazi ya chini kabisa (HaHa) ulithibitisha [hu] kuwa walikuwa ni wanafunzi waliokuwa wakiongoza mjadala uliofanyikia katika daraja hilo. Makumi ya waandamanaji walikuwa wakisubiri katika kitengo cha polisi cha Budapest hadi saa nane usiku wa Alhamisi wakisubiri kuachiwa kwa wenzao. Wanafunzi hao waliachiwa huru huku wakipewa onyo la kisheria kufuatia matukio ya uvunjaji wa sheria yaliyokuwa yakifanywa na raia.

Siku ya Jumatano, wanafunzi wa sekondari na wale wa vyuo vikuu waliandamana nchini Hangari wakipinga kupunguzwa kwa idadi ya wanaopata nafasi ya elimu ya juu pamoja na kupunguzwa kwa stahili zao. Katika shule nyingi za sekondari, wanafunzi walifanya migomo ya kukaa, walitumia dakika kadhaa kwa kukaa kimya na kupigania hatma ya maisha yao ya baadae. Kituo cha Mawasiliano X (XKK) kilipakia mtandaoni [hu] ramani pamoja na orodha ya matukio; zifuatazo ni baadhi ya picha:

Siku ya mwisho ya maandamano mjini Budapest ilimalizika kwa matukio mawili ya wanafunzi washiriki kutembea hadi kwenye daraja ambalo majadiliano lifanyikia ilikumkaribisha [hu] waziri wa rasilimali watu pamoja na Waziri Mkuu ili wathibitishe kuwa madai yao yameshatekelezwa. Waandamanaji walipoanza kutoka katika daraja hilo, polisi waliokuwa wakisindikiza matembezi waliwatia kizuizini [hu] wanafunzi watatu ambao hapo kabla walikuwa wakiongoza majadiliano kwa kutumia kipaza sauti.

Mwanafunzi akitumia kipaza sauti katika kutamka kauli mbiu mbalimbali wakati wa maandamano ya Budapest siku ya jumatano. Picha na Peter Nemeth, haki miliki © Demotix (19/12/2012).

Pamoja na kuwa waliachiwa masaa machache baadae, watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti, waliweka bayana ‘ukweli wa utani’ kuwa Waziri Mkuu Viktor Orbán aliwahi pia kutiwa kizuizini kwa kupigania haki za kidemokrasi wakati wa kipindi cha mpito cha demokrasia ya Hangari. Blogu ya Milioni Moja kwa Uhuru wa Habari nchini Hangari, ambayo pia hujulikana kama Milla, iliweka [hu] ujumbe huu kwa kutumia picha ya Orbán aliyetiwa nguvuni mwaka 1998 na picha ya mmoja wa wanafunzi walitiwa nguvuni hivi sasa:

Serikali ya Hangari ilionekana kuwa tayari kukubaliana na matakwa ya wanafunzi , kama ilivyotangazwa siku ya jumatano mchana kuwa vigezo vya udahili kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza mwaka 2013 vingebaki kuwawanafunzi 55,000 [hu] badala ya idadi ya 10,480 iliyokuwa imetangazwa awali mbele ya waandamanaji. Wanafunzi waliweka wazi maeneo mengi ambayo walifahamu kuwa hayakuhitaji kutozwa ada katika elimu ya juu ya Hangari, lakini walisisitiza kuwa maamuzi haya ya haraka hayakuwa ya kitaalamu na pia kurekebisha mfumo wa elimu ya juu ya Hangari ilihitaji maandalizi ya kutosha.

HaHa iliitaka [hu] serikali kufanya maamuzi kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa elimu na kisha kuja na mkakati mzuri wa matumizi ya fedha ili kuwa na uhakika wa ustawi vya vyuo vikuu mara baada ya mahitaji ya udahili kupitiwa upya ili kuboreshwa zaidi.
Siku ya jumatano, msemaji wa serikali alisema kuwa, vigezo vya alama wakati wa udahili vingetangazwa kabla ya Sikuu ya Noeli [hu]. Alama za udahili zinakokotolewa kwa kila mwanafunzi wa shule ya sekondari kwa kuzingatia ngazi ya mwanafunzi ya ufaulu, mitihani ya mwisho pamoja na vigezo vingine. Hata hivyo, siku ya Alhamisi mchana, Wizara ya Rasilimali Watu ilitangaza [hu] kuwa wasingeweka bayana vigezo kwa mwaka huu (2012). Elimu ya watu wazima, elimu ya rasilimali watu, masomo ya utumizi uchumi, masomo ya mawasiliano na vyombo vya habari, masomo ya uchumi wa kimataifa na masomo ya sheria bado si kipaumbele cha serikali; na hivyo hakutakuwepo msamaha wa ada ya masomo [hu] kwa ajili ya wanafunzi watakaosoma masomo yaliyotajwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.