· Novemba, 2009

Habari kuhusu Maandamano kutoka Novemba, 2009

Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video

  23 Novemba 2009

Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli. Wanaharakati hawa wa mtandaoni watatumikia vifungo vya miaka miwili na mwingine miaka miwili na nusu gerezani baada ya mashitaka ambayo...

Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini

  11 Novemba 2009

Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.

Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena

Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba uliendesha maandamano makubwa ambapo maandamano hayo yalikabiliwa na matumizi makubwa ya nguvu ya kuyazuia yaliyofanywa na vikosi vya usalma. Kama ambavyo sasa inatarajiwa, uandishi wa habari wa kiraia nchini Irani haukukosa kitu kwani ulirekodi 'historia' hiyo kupitia simu zao za mikononi.