Habari kuhusu Maandamano kutoka Juni, 2009
Iran: Video za Maandamano ya Upinzani Zazidi Kumiminika
Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.
Irani: Maandamano na Ukandamizaji
Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Husein Mousavi huku wakiipuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.
Irani: Kimbunga cha Maandamano Baada Ya Uchaguzi
Maelfu ya watu waliandamana mjini Tehran, Mashdad na kwenye miji mingine mikubwa ya Irani ili kupinga ushindi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa. Washindani wawili wanamageuzi pamoja na mashabiki wao wanasisitiza kwamba palitokea udanganyifu.