· Novemba, 2009

Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Novemba, 2009

Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini

  23 Novemba 2009

Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.

Misri na Aljeria: Pambano la Twita

Katika sehemu nyingi duniani, hakuna linalounganisha zaidi – au wakati mwingine kutenganisha – zaidi ya pambano la mpira wa miguu. Washabiki wa Misri na Aljeria, katika ulimwengu wote wa Waarabu na zaidi, walilidhihirisha hilo Jumamosi hii wakati timu zao zilipokwenda sambamba wakati wa kuwania kuingia fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.