· Juni, 2013

Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Juni, 2013

Mtu Mmoja Afariki Kwenye Maandamano Yanayoitikisa Brazil

  28 Juni 2013

Kijana mdogo aliuawa baada ya kugongwa na gari huko Ribeirao Preto na dazeni ya watu wengine walijeruhiwa pale waandamanaji walipokuwa wakikabiliana na polisi katika majiji ya Brasilia, Rio de Janeiro na Salvador kufuatia watu zaidi ya milioni moja kujitokeza katika mitaa ya majiji makubwa na madogo nchini kote Brazil katika maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miongo miwili.

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

  8 Juni 2013

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...

Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano

Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa maandishi haya [en] yaliyoandikwa katika ukurasa wa kundi la Kimasedonia kwenye mtandao wa Facebook yaliyopewa kichwa cha habari cha “Waandishi wa...