Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Disemba, 2010
Urusi: Habari ya Putin-Berlusconi Kwenye WikiLeaks
Kwenye The Daily Beast, Julia Ioffe anatoa maoni juu ya masuala yaliyowekwa wazi katika Wikileaks kuhusu uhusiano kati ya Waziri Mkuu wa Urusi na mwenzake wa Italia Silvio Berlusconi.
Brazil: Leo Rais, Kesho Mwanablogu
Rais wa Brazil anayeondoka madarakani Luis Inácio Lula da Silva (Lula) alihojiwa na wanablogu wapenda maendeleo (au wenye mlengo wa kati kuelekea kushoto) kwa mara ya kwanza wiki hii, tukio ambalo limechukuliwa na wengi kama hatua muhimu katika msukumo uliopo unaotaka mfumo wa habari wa kidemokrasia zaidi nchini Brazil.