Brazil: Leo Rais, Kesho Mwanablogu

Rais wa Brazil anayeondoka madarakani Luis Inácio Lula da Silva (Lula) alihojiwa [pt] na wanablogu wapenda maendeleo (au wenye mlengo wa kati kuelekea kushoto) kwa mara ya kwanza wiki hii, tukio ambalo limechukuliwa na wengi kama hatua muhimu [pt] katika msukumo uliopo unaotaka mfumo wa habari wa kidemokrasia zaidi [pt]nchini Brazil.

Mahojiano hayo ya masaa mawili yalirushwa moja kwa moja kwenye mtandao, na kuwawezesha wanablogu kushiriki kupitia kamera za kwenye mtandao kwenye tovuti ya Twita.

Maa mbalimbali [pt] zilipitiwa, pamoja na mageuzi ya kisiasa nchini Brazil, utoaji mimba, elimu, rushwa, na sera za mambo ya nchi za kigeni.

Suala la marekebisho ya vyombo vya habari lilikuwa juu kwenye ajenda,na Lula alithibitisha,

Eu sou o resultado da liberdade de imprensa neste país. A maior censura que existe é acreditar que a mídia não pode ser criticada.

Mimi ni matokeo ya uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hii. Uzuiaji mkubwa wa uhuru huo ambao bado upon i kuamini kuwa vyombo vya habari haviwezi kukosolewa.

Alijipanga dhidi ya uenezwaji wa taarifa za uongo na kutaka sheria kali zaidi za vyombo vya habari nchini Brazil. Alivishutumu vyombo vya habari vikuu nchini Brazil kwa kuamsha hofu kwa kutia chumvi kwenye suala la upeo wa athari za mgogoro wa kifedha duniani, na kwa kuripoti sababu za uongo zilizopelekea kuanguka kwa ndege ya shirika la TAM mwaka 2007.

Vyombo vikuuvya habari nchini Brazil bado vimo mikononi mwa familia chahce zinazotawala, kubwa kati ya hizo ikiwa familia ya Marinho, ambayo inamiliki mtandao mkubwa wa utangazaji, Rede Globo [pt]. Kihistoria kwa kushirikiana kwa karibu na utawala wa kiimla wa jeshi (1964-1984), Globo Globo ilijiweka katika nafasi nzuri ya kuimarisha na kushunikiza udhibiti wake kwenye televisheni, filamu, redio na uchapishaji.

Mara kwa mara magazeti yamejikuta yakilaumiwa kwa kutumikia maslahi ya kisiasa, na havi karibuni zaidi wakati wa uchaguzi wa rais, ambamo rais mteule wa sasa, Dilma Rousseff, alionekana kuwa muathirika [pt] wa mauaji ya kimbari ya vyombo vya habari. Magazeti makubwa ya kila siku na majarida mjadala wa kura za mara ya pili za kutatua matokeo ya uchaguzi, huku wakijengea mtaji kwenye masuala tata, kama vile utoaji mimba na dini, ambayo huiacha Brazil ikiwa imegawanyika vibaya.

Rais huyo anayeondoka madarakani aliulizwa maswali juu ya mapendekezo yaliyotolea mwaka jana wakati wakati wa Kongamano la Taifa la Mawasiliano [pt]. ]. Udhibiti mkubwa zaidi, ushiriki wa raia na udhibiti wa kijamii ndani ya vyombo vikuu vya habari yalikuwa miongoni mwa mahitaji yaliyokuwemo ndani ya rasimu ya mapendekezo katika kongamano, huku Lula akiwahakikishia wanablogu kuwa mapendekezo hayo yangewasilishwa katika bunge la Brazil. Aliongeza kuwa mdahalo huo hivi sasa umo mikononi mwa Dilma, ambaye uhuru mkubwa zaidi wa habari nchini Brazil wakati wa hotuba ya kukubali matokeo ya uchaguzi tarehe 31 Oktoba

Rais Lula akiongea na mwanablogu Conceição Oliveira kupitia Twitcam wakati wa mahojiano yake ya kwanza na wanablogu wa Brazil. Picha na Ricardo Stuckert/PR, kutoka kwenye akaunti ya Flickr ya blogu ya Blog do Planalto. imechapwa hapa chini ya leseni ya Creative Commons.

Kwa wale ambao walihudhuria, kipindi hicho kiliashiria kufunguliwa kwa mkondo mpya wa mawasiliano ya kimaendeleo kati ya wafanya maamuzi na nguvu za habari ambazo si za vyombo vikuu vya habari. Mtumiaji mmoja wa mtandao, ambaye alishiriki kwa kutumia Twitcam, alikielezea kipindi hicho kama “kilichozua hisia kali” [pt]. Mwanablogu wa siasa anayejulikana Rodrigo Vianna [pt], wakati akiwakumbusha wasomaji kuwa ‘Vyombo vya habari vya zamani’ vitaendelea kuwepo, alisema,

Não sei se os leitores têm dimensão do que isso significa: quebrou-se o monopólio. Internautas puderam perguntar, via twitter. O mundo da comunicação se moveu. Foi simbólico o que vimos hoje.

Sijui kamawasomaji wanaelewa ukubwa wa jambo hili unavyomaanisha: umiliki wa jumla umevunjwa. Kwa kutumia Twita, watumiaji wa intaneti wanaweza kuuliza maswali. Ulimwengu wa mawasiliano umepiga hatua. Tulichokiona leo kulikuwa ni ishara (ya jambo hilo).

Renato Rovai, mhariri wa gazeti la kiliberali la Revista Forum [pt], kadhalika alikuwa alikuwa na mtazamo chanya [pt]:

Ela entra para a história da cobertura política brasileira.

Mahojiano yale yaliingia kwenye historia ya uandishi wa siasa za Brazil.

Kundi la wanablogu walioalikwa pia lilikuwana muhimu, anaandika mshiriki Leandro Fortes [pt]:

Esse mesmo grupo foi chamado por Serra, no auge da baixaria da campanha eleitoral, de representantes de “blogs sujos”, uma referência nervosa a um tipo de mídia que pegou o tucano, uma criatura artificialmente sustentada pela velha mídia corporativa, no contrapé. Nem Serra, nem ninguém na velha direita brasileira estavam preparados para o poder de reação, análise e crítica da blogosfera e das redes sociais. Matérias falsas, reportagens falaciosas, discursos hipócritas, obscurantismo religioso e a farsa da bolinha de papel, tudo, tudo foi desmontado em poucas horas dentro da internet. Chamar-nos de “sujos” nem de longe nos alcançou como ofensa, pelo contrário. Nós, os “sujos” fizemos a história dessa eleição. Serra e seus brucutus terceirizados sumiram no ralo virtual.

Kundi hili hili liliitwa na Serra, wakati wa kilele cha kampeni potofu za uchaguzi, sauti za ‘wanablogu wa hovyo’, akitoa angalizo la kuvunja mishipa la aina ya uandishi uliomkamata toucan [jina la Serra], kiumbe bandia anayeungwa mkono na vyombo vya habari vya zamani akiwa bado hajajitayarisha. Si Serra wala mtu mwingine yeyote katika kambi ya mlengo wa kulia nchini Brazil aliyetarajia nguvu ya mwitiko ule, uchambuzi na ukosoaji katika ulimwengu wa blogu na katika mitandao mingine ya kijamii. Makala za uongo, taarifa za kubuni zisizo na mantiki, mitizamo ya kinafiki, udini wa kihafidhina pamoja na aibu ya bolinha de papel viliwekwa wazi katika intanerti ndani ya saa chache. Sisi, ‘wanablogu wa hovyo’ tulitengeneza historia ya uchaguzi huu. Serra pamoja marafiki zake wa zama za kale walitokomea katika mtaro anuai.

Hata hivyo, washiriki walikuwa wepesi kuonyesha mapungufu ya kipindi kile. Vianna aliona kwamba masuala yanayoshinikiza ya haki za binadamu, marekebisho ya sheria ya ardhi, sheria na huduma za afya havikupitiwa kwa undani wa kutosha, vilizidiwa badala yake na mazungumzo juu ya mawasiliano. Kadhalika kutokuwepo kwa wanablogu wanawake pia kulilalamikiwa, japokuwa Conceição Oliveira, wa blogu ya Maria Fro [pt] (ambaye pia hublogu kama Conceição Lemes katika Vi o Mundo) [pt]  alishiriki kupitia Twitcam.

Lula alionekana kushawishika na nguvu ya kuwafikia wananchi kwa kupitia mitandao ya kijamii, na kuahidi kuwa atablogu na kutwita huko mbeleni. Brazil ni ya pili kwa kuwa na watumiaji wa Twita wengi zaidi duniani baada ya Marekani, na watumiaji wake wa intaneti wapo kati ya milioni 67 mpaka milioni 73. Tovuti za kijamii kama vile Orkut na kwa kiwango cha chini , Facebook, pia bado zinaendelea kupata umaarufu mkubwa.

Thiana Biondo alichangia kuandika makala hii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.