· Februari, 2014

Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Februari, 2014

Caribian: Namna Vyombo vya Habari Vinavyoathiri Mitazamo

  28 Februari 2014

Venezuela na Haiti zimekuwa zikikabiliwa na maandamano ya kupinga serikali. Hata hivyo, ukuzaji wa mgogoro wa Venezuela unaofanywa na vyombo vya habari vya kimataifa na ukimya wake kwa mgogoro wa Haiti, unaibua maswali muhimu kuhusu kuyumba kwa Marekani katika kuimaisha tunu ya haki za binadamu na demokrasia. Kevin Edmonds anatoa...

Vyombo Vikuu vya Habari Vyaihujumu Facebook

  24 Februari 2014

Mwanablogu wa Teknolojia Amitha Amarasinghe anadai kwamba mtandao wa Facebook unapewa taswira hasi na vyombo vikuu vya habari nchini Sri Lanka kwa vichwa vya habari kama “Mwanafunzi ajiua shauri ya picha iliyowekwa Facebook”, “Mapenzi ya Facebook yaishia na kifo” na kadhalika. Ghafla tu, kuna mwongezeko mkubwa wa maudhui yanayotoa taswira...

Waandishi wa Habari za Kiraia, Jiandikishe Kupata Video Bure

  23 Februari 2014

Jukwaa linalokusanya video kadri zinavyowekwa mtandaoni linaloitwa Ustream linalota fursa ya kujiandikisha kufungua anuania mpya na pia kuzitangaza kwa ajili ya kuzitumia video hizo kwa ajili ya habari zinazotokea, uanaharakati na hata kwa matumizi ya mengine ya faida kwa jamii. Hivi karibuni Ustream imesaidia chaneli tatu za moja kwa moja...

Maandamano ya Venezuela: ‘Vyombo vya Habari vya Kimataifa: Ingilieni Kati!’

  21 Februari 2014

Mpendwa Mhariri wa Kimataifa: Sikiliza na uelewe. Hali ya mambo imebadilika nchini Venezuela usiku wa kuamkia leo. Kile kilichokuwa kinaonekana kuwa hali ya kutokuelewana iliyokuwepo kwa miaka sasa imebadilika ghafla. Kile tulichokishuhudia asubuhi hii si habari ya Venezuela uliyodhani unaielewa. Kwenye blogu ya Caracas Chronicles Francisco Toro anashutumu kutokuwepo kwa vyombo...