Mchora Katuni wa Algeria Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 18 Jela kwa Kumdhihaki Rais

[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa za lugha ya Kifaransa.]

Jina lake ni Djamel Ghanem, na mchora katuni kijana wa Kialjeria. Kazi yake si ya kujifurahisha tu kwenye nchi ambako ufuatiliaji na kushitakiwa ni kawaida kuwangojea wote wale wanaothubutu kusema wazi wazi kile wanachofikiri. Ghanem anakabiliwa na kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kuchora kikaragosi ambacho hata hivyo hakikuchapishwa cha Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kilichohesabiwa na mamlaka za dola nchini humo kuwa ni matusi that was deemed offensive. 

Djamel Ghanem

Djamel Ghanem kupitia jarida la Algérie Focus. Imetumiwa kwa ruhusa

Kwa hakika, Rais Bouteflika hakutajwa wazi wazi katika katuni hiyo ambayo hata hivyo haikuwa imechapishwa. Mchoro huo unawaonyesha raia wawili wakidhihaki kipindi cha nne ambacho rais wa sasa anakitafuta baada ya kuwa ameitawala Aljeria kwa miaka 15 mfulizo. Katuni hiyo inakifananisha kipindi cha nne na nepi za mtoto. Kwa mchoro huo, Ghanem alitaka kutuma ujumbe kuwa Wa-Aljeria wamefanywa kama watoto.

Kwa hilo pekee, [mchoraji huyo] alichusimamishwa kizimbani na kutishiwa kifungo. Mwanasheria wa wilaya ya  Oran, mji wa pili kwa ukubwa nchini Aljeria, alimtaka mchoraji huyo kukiri kuwa alikuwa na lengo la kumdhihaki rais. Lakini Ghanem kwa ujasiri kabisa alikana kuwa na nia hiyo. 

Si Bouteflika wala washauri wake walifungua mashitaka dhidi ya Ghanem. Alikuwa ni mwajiri wa zamani wa Ghanem, La Voix de l'Oranie (Sauti Oran), gazeti la kila siku linalofahamika kwa tahariri zenye mrengo wa kuipamba serikali, ndilo lililomshitaki kwa katuni yake hiyo ambayo hata hivyo haijawahi kuchapishwa kwenye vyombo vya habari. 

Akiwa ameshitakiwa na gazeti lake mwenyewe, Ghanem alijikuta mpweke asiye na msaada wowote wa chombo chochote cha habari nchini Aljeria. Akihojiwa na Algerie-Focus, Ghanem alieleza kuwa pamoja na changamoto nyingine, ilikuwa vigumu kumpata mwanasheria wa kumtetea dhidi ya mashitaka hayo: 

Le directeur de publication d’un autre quotidien a été menacé si jamais il me recrutait. Je suis devenu persona non grata. A travers moi, ils veulent abattre l’opposition algérienne qui dit non à un quatrième mandat

mkurugenzi wa gazeti jingine alishauriwa kutokuniajiri. Nikawa mkiwa asiye na rafiki, Kupitia mimi, walitaka kuwatisha wapinzani wa mpango huo wa kutafuta kuchaguliwa kwa kipindi cha nne cha uraist.

Baada ya kusikilizwa kwa mshitaka hayo kwa mara ya kwanza, majaji walipendekeza kifungo cha miezi 18 dhidi ya Ghanem. Hukumu ya mwisho inatazamiwa kusikilizwa mwezi ujao tarehe 4 Machi. Wakati huo huo, watumiaji wa mtandao wameendelea kupaza sauti zao kumwuunga mkono na kuungana kumsaidia Ghanem. Kuna tamko la mtandaoni linalotaka Ghanem aachiliwe huru:

Si les médias et l’opinion se taisaient sur cette atteinte à la liberté d’expression et ces violations des droits d’un citoyen dans les bureaux d’un juge, les tribunaux pourraient demain condamner un journaliste pour avoir pensé du mal du président de la république, d’un gradé de l’armée, d’un ministre ou d’un élu. Nous signataires de cet appel exigeons l’arrêt des poursuites judiciaires engagées contre Djamel Ghanem

Kama vyombo vya habari na maoni huru ya watu yanabaki kimya kulaani uvunjifu huu wa uhuru wa kujieleza na uvunjifu wa haki za binadamu, basi kesho mahakama yoyote inaweza kumshitaki mwandishi kwa kumkosoa rais wa jamuhuri, au afisa wa jeshi, waziri au hata naibu waziri. Kwa hati hii ya kudai kuachiliwa huru kwa Ghanem, tunadai kusitishwa kwa mashitaka dhidi ya Djamel Ghanem.

Kwa kumkinga rais dhidi ya ukosoaji wa aina yoyote, utawala wa nchi hiyo unajaribu kuimarisha sera ya uimla dhidi ya raia wa nchi hiyo. Uhuru wa maoni uko shakani Algeria. Kesi ya Ghanem ni mfano hai wa namna hali ilivyo ngumu kwa wachora katuni na watu wengine wasioficha maoni yao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.