Mpendwa Mhariri wa Kimataifa:
Sikiliza na uelewe. Hali ya mambo imebadilika nchini Venezuela usiku wa kuamkia leo. Kile kilichokuwa kinaonekana kuwa hali ya kutokuelewana iliyokuwepo kwa miaka sasa imebadilika ghafla.
Kile tulichokishuhudia asubuhi hii si habari ya Venezuela uliyodhani unaielewa.
Kwenye blogu ya Caracas Chronicles Francisco Toro anashutumu kutokuwepo kwa vyombo vya habari vya kimatafa kutangaza ghasia na matukio yanayoendelea kukua tangu Februari 19.
Francisco anaonyesha picha za kurasa za habari za mashirika makubwa ya habari kama BBC, The New York Times, CNN, The Guardian, Al Jazeera idhaa ya Kiingereza, na Fox News asubuhi ya Februari 20 —yote hayana habari zozote kuhusu matukio ya ghasia tangu siku iliyopita.
Anahitimisha:
Kiwango cha kupuuzia hali ya mambo inayoendelea Venezuela kinashangaza sana.
Kufungiwa kwa vyombo vya habari vya ndani kunasindikizwa na “kususiwa” na vile vya kimataifa, ambavyo wala hakuna anayewafuatilia isipokuwa tu kupuuza na kuona kama yanayoendelea hayawahusu. Ni vigumu kueleza hisia za kutokusaidiwa unapotazama kurasa hizi na kutokuona chochote. Venezuela inawaka moto; hakuna anayejali.
Hebu niliweke hili wazi. Nyote mnahitaji kuingilia kati. Muda wa kutupilia mbali kile mlichodhani mnakielewa kuhusu Venezuela ndio huu.
Unaweza kuangalia ukurasa wa habari zetu maalumu kuhusu maandamano yanayoendelea Venezuela hapa.