Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Juni, 2009
Uganda: Mradi wa Katine Wawafikisha Wanakijiji Kwenye Ulimwengu wa Blogu
Inakadiriwa kuwa matumizi na uenezi wa intaneti nchini Uganda ni kwa kiwango cha asilimia sita tu, idadi ambayo inazuia sehemu kubwa ya watu kujiunga na ulimwengu wa blogu nchini Uganda au kuweza kuwasiliana na ulimwengu wa blogu duniani. Mradi wa Katine unaoendeshwa na Guardian and Observer unafanya kazi kubadilisha hali hiyo katika kijiji kimoja.
Malawi: Wasikilize wanablogu wa uchaguzi Malawi
Wamalawi wanapiga kura katika uchaguzi wa Raisi na Bunge. Baadhi ya wanablogu walipatiwa mafunzo na PenPlus Bytes, Taasisi ya kimataifa ya Uandishi wa TEKNOHAMA kwa ushirikiano na New Media Insitute kwa lengo la kuangalia na kutoa maoni yao kuhusu uchaguzi huo kwa kutumia blogu, teknolojia ya twita na simu za viganjani. Hebu na tuziangalie blogu zao, ambazo zimehifadhiwa katika Potal ya chaguzi za Afrika. Poto hii hutoa taarifa za kutosha kuhusu chaguzi mbalimbali katika nchi za kiafrika.